PICHA ZOTE NA FRIDAY SIMBAYA
Wafamasia
na wafanyabiashara wenye maduka binfasi ya dawa za binadamu na mifigo
wameombwa kuzingatia sheria, kanuni na taratibu za uuzaji dawa.
Hayo
yalisemwa jana na Mganga Mkuu wa Mkoa wa Iringa Dkt. Robert Salim
katika maadhimisho ya ‘Siku ya Famasi’ yaliyoandaliwa na chama cha
wanafanzi wa famasi –Tanzania (TAPSA), tawi la Chuo Kikuu Katoliki cha
Ruaha (RUCU) kwa ufadhili wa shirika la Austrian Leprosy Relief
Association kwa kushirikiana shirika la Action Medeor.
Maadhimisho hayo ambayo yalienda sambamba na kaulimbiu isemayo, ‘MAPAMBANO DHIDI YA USUGU WA DAWA NI YA KILA MMOJA WETU.’
Dkt.
Salim alisema kuwa wafamasia na wafanyabiashara wanatakiwa kuuza dawa
kwa kuzingatia sheria, kanuni na taratibu kwa mfano, kuuza dawa za moto
kwa prescription na kutunza dawa vizuri.
Alisema kuwa serikali ya awamu ya tano ina lengo la kuifikisha nchi katika uchumi wa kati kupitia sekta ya viwanda.
Mganga
mkuu huyo aliviomba vyuo vyote nchini vya famasi viwaandae vijana
kufungua viwanda vya dawa na vifaa tiba kwa vile malighafi nyingi zipo
hapa Tanzania.
“Kuna mistu, pamba, gypsum na kadhalika ambazo ni hazina kubwa ya dawa za tiba asili,” alisema Dk. Salim.
Pia,
aliwataka wanafunzi wanaosomea masomo ya famasia wa kimaliza masomo yao
waanzishe viwanda vidogo vidogo vya dawa, ili kutimiza adhima ya
serikali ya awamu ya tano ya sera ya viwanda ambapo kutasaidia kupunguza
tatizo la ajira kwa vijina.
Naye,
Mwenyekiti wa TAPSA-RUCU Ndamo Adam alisema kuwa usugu wa dawa ni janga
la kifaifa husuani nchi ambazo zipo katiak ukanda jangwa la sahara
kusini.
Alisema
kampeni ya kupambana na usugu wa dawa ni jukumu la kimoja kwa vile dawa
zote zinazotumika kutibu magonjwa ya kuambukiza huweza kuathiriwa na
usugu wa dawa.
Adam
alifafanua kuwa usugu wa dawa ni hali ya dawa kushindwa kuua au kuzuia
ukuaji wa vimelea vya magonjwa na vimelea vya magonjwa ndivyo hujenga
usugu dhidi ya dawa.
“Dawa
zinazotumika mara kwa mara kama vile Ampicilin, Ciprofloxacin,
Tetracycilin, Erythromycin, Metronidazole, Amoxicilin, Chloramphenicol
na Griseofulvin zinaathiriwa zaidi,” alisema Adam.
Alisema
kuwa moja ya usugu wa dawa ni kutotumia ‘dozi’ sahihi ya dwa na kwa
muda ulioelekezwa pamoja na kutumiaantibayotiki kutibu magonjwa
yasiohitaji antibiotiki.
Kwa
upande wake, Mfamasia na mwalimu wa Famasia katika chuo kikuu katoliki
cha Ruaha (RUCU) Gasper Baltazary alisema kuwa kampeni dhidi usugu wa
dawa iwe endelevu.
Alisema
kuwa kuna umuhimu mukubwa wa usimamia ugunduzi sahihi wa magonjwa (kwa
vipimo), utoaji dawa kwa dozi sahihi (vipimo), muda sahihi, kuzingatia
masharti ya daktari pamoja na kutoa dawa ambazo hazijaisha muda wake wa
matumizi.
Baltazary
alisema kuwa siku ya famasi ni moja kati ya majukumu ya chama cha TAPSA
ambapo lengo ni kuwaleta wanafunzi na wataalamu mbalimbali wa kada ya
afya ili kujadili viti ambavyo vinahusu afya.
Alisema
kuwa ukosefu wa elimu ndio chanzo kikubwa cha uwepo ya usugu wa dawa,
hivyo basi jamii na wafanyabiashara waache kutumia dawa bila kufanya
vipimo na kuuza dawa kwa lengo la kupata tu pesa.
Mwisho
0 comments:
Post a Comment