Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Mhe.
Festo Kiswaga (aliyemwakilisha Mkuu wa mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony
Mtaka), akizungumza na wananchi katika ufunguzi wa Maonesho ya tatu ya
mifuko/programu za uwezeshaji na vikundi vya kifedha vya kijamii,
uliofanyika Oktoba 16, 2019 katika Uwanja wa Halmashauri ya mji wa
Bariadi mkoani Simiyu.
Baadhi ya wananchi wa Bariadi
mkoani Simiyu wakimsikiliza Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Mhe. Festo
Kiswaga (aliyemwakilisha Mkuu wa mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka),
katika ufunguzi wa Maonesho ya tatu ya mifuko/programu za uwezeshaji na
vikundi vya kifedha vya kijamii, uliofanyika Oktoba 16, 2019 katika
Uwanja wa Halmashauri ya mji wa Bariadi mkoani Simiyu.
Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Mhe.
Festo Kiswaga akimsikiliza Afisa kutoka Mamlaka ya Masoko ya Mitaji na
Dhamana, katika ufunguzi wa Maonesho ya tatu ya mifuko/programu za
uwezeshaji na vikundi vya kifedha vya kijamii, uliofanyika Oktoba 16,
2019 katika Uwanja wa Halmashauri ya mji wa Bariadi mkoani Simiyu.
Katikati ni Mkuu wa Wilaya ya
Bariadi, Mhe. Festo Kiswaga (aliyemwakilisha Mkuu wa mkoa wa Simiyu,
Mhe. Anthony Mtaka), akizungumza na wananchi katika picha ya pamoja na
baadhi ya viongozi na Watumishi wa BarazalaTaifa la uwezeshaji wananchi
kiuchumi katika Maonesho ya tatu ya mifuko/programu za uwezeshaji na
vikundi vya kifedha vya kijamii, uliofanyika Oktoba 16, 2019 katika
Uwanja wa Halmashauri ya mji wa Bariadi mkoani Simiyu..
Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Mhe.
Festo Kiswaga akimsikiliza mmoja wa wanufaika wa mikopo kutoka SIDO
katika ufunguzi wa Maonesho ya tatu ya mifuko/programu za uwezeshaji na
vikundi vya kifedha vya kijamii, uliofanyika Oktoba 16, 2019 katika
Uwanja wa Halmashauri ya mji wa Bariadi mkoani Simiyu.
……………..
Na Stella Kalinga, Simiyu RS
Mkuu wa Wilaya ya Bariadi Mhe.
Festo Kiswaga ametoa wito kwa Mifuko na programu za uwezeshaji wananchi
kuangalia jinsi ya kuwezesha wananchi wengi zaidi kupata mitaji ya
kuanzisha viwanda, ili uchumi wa nchi ukue na kupunguza changamoto
zinazokabili jamii.
Kiswaga ameyasema wakati
akimwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka katika uzinduzi
wa Maonesho ya tatu ya mifuko/programu za uwezeshaji na vikundi vya
kifedha vya kijamii, uliofanyika Oktoba 16, 2019 katika Uwanja wa
Halmashauri ya mji wa Bariadi mkoani Simiyu.
“Sote tunafahamu kwamba Tanzania
inalenga kufikia uchumi wa katika ifikapo mwaka 2025 na viwanda ni
nyenzo itakayowezesha nchi kufika huko; viwanda vina mchango mkubwa sana
katika kukuza uchumi wa nchi kwa kuwa vinanufaisha jamii kwa kutoa
ajira, kulipa kodi, kununua malighafi kutoka kwa wakulima na mengine
mengi,” alisema Kiswaga.
Aidha, Kiswaga alitoa wito kwa
wananchi wa mikoa ya kanda ya ziwa na maeneo mbalimbali nchini kufika
katika maonesho haya kupata maelezo kutoka kwa wawakilishi wa mifuko
/programu za uwezeshaji za Serikali, kuonesha bidhaa, kunua bidhaa za
wajasiriamali na kupata uelewa wa masuala ya uwezeshaji wananchi.
Naye Afisa Maendeleo ya Biashara
wa Taasisi ya kusaidia sekta binafsi na Kilimo, (PASS) Kanda ya Ziwa,
Faustine Mungo amesema wameandaa mpango mkakati wa miaka mitano ambapo
wanatarajia kutoa ajira 700,000 ambao unatarajia kuzifikia familia zaidi
ya 200,000.
Kaimu Mkurugenzi wa Uwezeshaji na
Ushiriki wa Watanzania katika Uwekezaji, Bi.Esther Mmbaga kutoka Baraza
la Taifa la Uwezeshaji wananchi Kiuchumi(NEEC), amesema malengo ya
maonesho haya ni pamoja na kukuza uelewa wa wananchi kuhusu uwepo,
majukumu na vigezo katika kutoa huduma za mikopo na programu za
uwezeshaji.
Bi. Mmbaga ameongeza kuwa malengo
mengine ni kuhamasisha wananchi ili waweze kunufaika na fursa zilizopo
katika mifuko na programu za uwezeshaji na kuhamasisha wananchi kujenga
utamaduni wa kuweka akiba na kuwekeza katika miradi yenye tija.
Maonesho ya tatu ya
mifuko/programu za uwezeshaji na vikundi vya kifedha vya kijamii,
yenye Kauli Mbiu “Mitaji ni Chachu ya Kujenga Uchumi wa Viwanda”ambayo
yanaendelea katika uwanja wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi yanatarajiwa
kufungwa rasmi Oktoba 20, 2019 .
0 comments:
Post a Comment