Mgeni rasmi-Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) akisisitiza jambo wakati wa ufunguzi wa mkutano mkuu wa mwaka wa wanachama wa chama cha wakulima Tanganyika (TFA) Jijini Arusha, jana tarehe 30 Machi 2019. (Picha Zote Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo)
Sehemu ya washiriki wa mkutano mkuu wa mwaka wa wanachama wa chama cha wakulima Tanganyika (TFA) wakifuatilia hotuba ya Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) wakati wa ufunguzi wa mkutano huo Jijini Arusha, jana tarehe 30 Machi 2019.
Mkurugenzi Mtendaji wa TFA Ndg Ezrah Sirikwa akimkabidhi kadi namba moja ya uanachama wa TFA Mgeni rasmi-Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) mara baada ya ufunguzi wa mkutano mkuu wa mwaka wa wanachama wa chama cha wakulima Tanganyika (TFA) Jijini Arusha, jana tarehe 30 Machi 2019.
Mgeni rasmi-Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) akiwa katika picha ya pamoja na viongozi na wadau wa mkutano mkuu wa mwaka wa wanachama wa chama cha wakulima Tanganyika (TFA) Jijini Arusha mara baada ya ufunguzi wa mkutano huo, jana tarehe 30 Machi 2019.
Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo-Arusha
Serikali
imesema kuwa ina mpango wa kuwa na Bima ya mazao ili kuwanufaisha wakulima
kutokana na changamoto wanazokabiliana nazo punde kunapokuwa na matatizo ya ukame.
Kutokana
na uchache wa mvua za msimu zinazoendelea Bima ya mazao ni sehemu ya kuwanusuru
wakulima kutona na mabadiliko ya tabia nchi yanayopelekea kuwa na mvua za
wastani.
Waziri
wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) ameyasema hayo leo tarehe 30 Machi 2019
wakati wa ufunguzi wa mkutano mkuu wa mwaka wa wanachama wa chama cha wakulima
Tanganyika (TFA) Jijini Arusha.
Kadhalika, aliipongeza TFA kwa kuwa na
mtandao mkubwa wenye matawi 16 wa kuwasaidia wakulima nchini, katika mikoa ya Ruvuma, Songwe, Mbeya, Iringa, Morogoro,
Dar es Salaam, Tanga, Kilimanjaro, Arusha na Manyara ambapo amewataka kuwa
na mkakati wa kuongeza matawi zaidi maeneo ya kanda ya ziwa, kanda ya kati na
kanda ya kusini.
Alisema huduma zitolewazo na TFA zinaunga
mkono serikali ya Awamu ya Tano katika mipango yake ya kutoa msukumo mkubwa
kwenye mazao ya kimkakati kama Chai, Kahawa, Korosho, Pamba na Tumbaku.
Mhe Hasunga amewataka wataalamu wa kilimo
katika ngazi mbalimbali nchini kushirikiana na TFA kuhakikisha kuwa wakulima,
wanatumia pembejeo zenye ubora na sahihi kwa wakati ili kuongeza tija kilimo na
kuepuka kutumia pembejeo ambazo hazikidhi viwango.
Mhe
Hasunga amezipongeza baadhi ya huduma zinazotolewa na TFA kama kuuza zana bora
za Kilimo, Mbolea, Viuwatilifu mbalimbali na kutoa
ushauri wa kitaalamu kwa wakulima zinazohusika kwa ueledi mkubwa.
Alisema kuwa katika juhudi za kumsaidia mkulima wa Tanzania, Serikali ya
Awamu ya Tano kupitia Wizara ya Kilimo itaendelea na utaratibu wa kununua
mbolea hapa nchini kupitia mfumo wa pamoja (Bulk Fertilizer Procurement).
Amesema, mfumo huo unalenga kupunguza kero ya upatikanaji na ulanguzi
katika bei za mbolea. Kupitia mfumo huo,
Serikali inaamini matumizi ya mbolea hapa nchini yataongezeka kwa kiasi kikubwa
ikilinganishwa na miaka iliyopita hivyo kuongeza tija katika kilimo.
Katika
hatua nyingine Waziri Hasunga ameeleza kuwa wananchi wanapaswa kuendelea kulima
mazao kwa wingi kwa kuzingatia mbinu bora za kilimo cha kisasa kwani serikali
ina mkakati kabambe wa kuimarisha soko la ndani nan je ya nchi.
Akizungumzia
hatua za serikali katika kuongeza weledi katika kuwasaidia wakulima kuwa na
pembejeo bora za kilimo alisema kwa sasa Wizara ya Kilimo kupitia Bodi za mazao
imeanza mchakato wa kuwasajili wakulima nchini.
“Kuwasajili
wakulima kutatufanya tuwe na uwezo mkubwa wa kuwahudumia ikiwa ni pamoja na
kutambua ukubwa wa mashamba yao na mazao wnayoyalima” Alikaririwa Mhe Hasunga
Katika
hatua nyingine Waziri Hasunga amekabidhiwa kadi namba moja ya uanachama wa TFA
ambapo amesisitiza ulazima wa wanachama waliopora mali zote za TFA kuzirudisha
haraka.
MWISHO
0 comments:
Post a Comment