METDO Tanzania

METDO Tanzania

Tuesday, October 8, 2019

DC KASESELA AWATAKA WAKAZI WA WILAYA YA IRINGA KUJIANDIKISHA KWENYE DAFTARI LA MPIGA KURA

Mkuu wa wilaya ya Iringa Richard kasesela akipata maelezo kutoka kwa muandikishaji wa kituo cha kinondoni 1 manispaa ya Iringa Revina Kongore
 Mkuu wa wilaya ya Iringa Richard kasesela akinadikisha mbele ya muandikishaji wa kituo cha kinondoni 1 manispaa ya Iringa Revina Kongore
NA FREDY MGUNDA,IRINGA.
 
Mkuu wa wilaya ya Iringa amewataka wakazi wa wilaya ya Iringa kujitokeza
kwa wingi kujiandikisha kwenye daftari la mpiga kura kwa ajili ya uchaguzi wa
serikali za mitaa utakao fanyika tarehe 24-11-2019 na kuhakikisha wanajitokeza
kugombea nafasi mbalimbali za uongozi wakati ukifika.
 
Akizungumza wakati alipokuwa anajiandikisha kwenye daftari za mpiga kura
katika kituo cha Kinondoni 1 manispaa ya Iringa,mkuu wa wilaya ya Iringa,Richard kasesela
amesema kuwa kila mkazi wa wilaya ya iringa wanahaki wa kujitokeza
kujiandikisha na kupata haki ya kumchagua kiongozi wanaemtaka.
 
“Hii ni fursa pekee ya kuhakikisha unapata nafasi ya kumchagua kiongozi
ambaye atasaidia kukuletea maendeleo kwenye mtaa au kijiji chako kwa kipindi
cha miaka mitano hivyo wakazi wote nawaomba mjitokeze kwa wingi kujiandikisha”
alisema Kasesela
 
Aidha Kasesela aliwakumbusha vijana kuhakikisha wanajitokeza kwa wingi
kujiandikisha na kugombea nafasi mbalimbali za kiuongozi kwa kuwa nao wanahaki
ya kuwa viongozi wa kuongoza mitaa ambayo wanaishi kwa maendeleo ya jamii.
 
Kwa upande wake muandikishaji wa kituo cha kinondoni 1 manispaa ya
Iringa Revina Kongore amewahimiza wakazi wa mtaa huo kuendelea kufika katika
kituo na kujiandikisha kwenye daftari la mpiga kura ili kuja kutumia haki yao
ya msingi wakati wa uchaguzi wa serikali za mitaa ambao utafanyika Tarehe 24
mwezi wa 11 mwaka 2019
Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com