Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akijiandikisha kwenye
Daftari la orodha ya Mpiga kura kwa ajili ya Uchaguzi wa Serikali za
Mitaa katika Kituo cha Kujiandikisha Shule ya Msingi Kilimani iliyopo
jijini Dodoma
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akizungumza na Waandishi
wa Habari mara baada ya kujiandikisha kwenye Daftari la orodha ya Mpiga
kura kwa ajili ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa katika Kituo cha
Kujiandikisha Shule ya Msingi Kilimani iliyopo jijini Dodoma
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt.
Binilith Mahenge,akitoa taarifa fupi kwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan,ambaye alienda
kujiandikisha kwenye Daftari la Orodha ya Mpiga kura kwa ajili ya
Uchaguzi wa Serikali za Mitaa katika Kituo cha Kujiandikisha Shule ya
Msingi Kilimani illiyopo jijini Dodoma.
………….
Na.Alex Sonna,Dodoma
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan,amewataka wananchi
kujitokeza kwa wingi kujiandikisha kwenye daftari la orodha ya mpiga
kura kwa ajili ya uchaguzi wa Serikali za mitaa utakaofanyika Novemba 24
mwaka huu na kuhakikisha wanajiandikisha.
Akizungumza baada ya kujiandikisha
kwenye daftari hilo katika Kituo cha Kujiandikisha Shule ya Msingi
Kilimani illiyopo jijini Dodoma,Mama Samia amewataka watanzania kwa
ujumla kujitokeza kujiandikindisha ili waweze kuchagua viongozi
watakaowaletea maendeleo katika mitaa yao na kusisitiza wananchi
wanapaswa kuchagua viongozi waadilifu na wenye uzalendo katika
kuwatumikia wananchi hasa wanyonge.
” Mimi leo nimeamua kutumia fursa
hii kuja kujiandikisha katika mtaa wangu wa Salmini na najua ni haki
yangu kuchagua Mwenyekiti wa Mtaa wangu na viongozi wangu kwa sababu
najua makazi yangu hapo Dodoma na hawa ndio watakaosimamia mambo yangu
kwenye mtaa wangu”amesema Mama Samia
”Hii ni fursa pekee ya kuhakikisha
mnapata nafasi ya kumchagua kiongozi ambaye atasaidia kuleta maendeleo
kwenye mtaa au kijiji chako kwa kipindi cha miaka mitano hivyo wakazi
wote nawaomba mjitokeze kwa wingi kujiandikisha
Hivyo amewataka watanzania
kuchagua viongozi waadilifu wenye kujali maslahi ya wananchi, wenye
maadili ya kuwatumikia watanzania na wenye kutunza rasimali za wananchi
wao na ambao watawasaidia viongozi wa ngazi za juu katika kuwatumikia
watanzania.
Awali Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dk
Benelith Mahenge,amesema kuwa zoezi la uandikishaji ndani ya Mkoa huo
limeanza jana na kwamba matarajio yao ni kuandikisha wananchi Laki Tisa.
” Idadi ya vituo ndani ya Mkoa
wetu ni 3, 679 na toka jana tumeandikisha watu 156,000 hivyo tunaamini
mpaka siku saba ziishe ambazo ni za uandikishaji tutakua tumezidi hata
idadi kwa kuwa wananchi wengi pia wanaenda makazini hivyo siku za
Jumamosi na Jumapili watapatikana kwa wingi,” Amesema Dk Mahenge.
0 comments:
Post a Comment