Waziri wa Kilimo Japhet Hasunga akiongoza kikao cha menejimenti ya
wizara yake kinachofanya ukumbi wa wizara jijini Dodoma kuhusu maandalizi ya
sera mpya ya kilimo ya mwaka 2019.
Sehemu ya wajumbe wa Menejimenti,Taasisi na Bodi za Mazao zilizopo chini
ya wizara ya kilimo wakifuatilia kikao kazi cha Waziri wa Kilimo leo jijini
Dodoma.
Katibu Mkuu wizara ya Kilimo Mhandisi Mathew Mtigumwe akishiriki kikao
cha menejimenti ya wizara kinachofanyika ukumbi wa Kilimo IV jijini Dodoma
Revocatus Kassimba, Wizara ya Kilimo-Dodoma
Waziri
wa Kilimo Japheti Hassunga leo amekutana
na Menejimenti ya wizara,wakuu wa Taasisi na
Wenyeviti wa Bodi za Mazao zilizopo
chini ya Wizara.
Lengo
la mkutano huu wa siku mbili unaofanyika
katika ukumbi wa wizara Jijini Dodoma ni kujadili maandalizi ya sera mpya ya kilimo
ya mwaka 2019 na kuondoa mapungufu yaliopo katika sera ya mwaka 2013.
Akiongea
katika kikao kazi hicho Waziri Hasunga
ameeleza umuhimu wa kuwa na sera mpya ya kilimo ni kufanya kilimo kuwa na tija
na cha kibiashara ,hivyo kuleta maendeleo makubwa katika sekta ya kilimo.
“Tunataka
sera mpya ya kilimo ilenge kukifanya kilimo kuwa shughuli kuu ya kiuchumi
itakayochangia kukuza uchumi wa nchi na kuongeza ajira” alisisitiza Waziri
Hasunga.
Waziri Hasunga amebainisha kwamba sera
mpya inatakiwa kukamilika kabla ya mwisho wa mwaka huu ili kutoa fursa kwa
Bunge kutunga sheria na kanuni za kilimo.
Aidha
katika mkutano huu wizara ya kilimo itajadili na kupitia taarifa ya utekelezaji
wa shughuli kwa mwaka 2018/2019 na kuweka mkakati madhubuti wa utekelezaji
mipango utendaji kazi ya wizara kwa mwaka 2019/2020.
Kikao
hicho kinahudhuriwa na Manaibu Waziri Hussein Bashe na Omary Mgumba,Katibu Mkuu
Mhandisi Mathew Mtigumwe na Naibu Katibu Mkuu Prof. Siza Tumbo.
Mwisho
0 comments:
Post a Comment