Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe
Magufuli akivuta utepe kuashiria uzinduzi wa Rada mbili za kuongozea Ndege
katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa
Julius Nyerere na Uwanja wa Ndege wa
Kimataifa wa KIA katika Sherehe zilizofanyika katika Uwanja wa Ndege
wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini
Dar es Salaam. Viongozi wengine kwenye picha ni Spika wa Bunge la Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Job Ndugai, Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano
Isack Kamwelwe, Mkurugenzi Mkuu wa TCAA Hamza Johari pamoja na Balozi wa
Ufaransa hapa nchini Fredrick Clavier
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe
Magufuli akiwa pamoja na viongozi mbalimbali akikata utepe kuashiria uzinduzi
wa Rada mbili za kuongozea Ndege katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere na Uwanja wa
Ndege wa Kimataifa wa KIA katika Sherehe
zilizofanyika katika Uwanja wa Ndege wa
Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe
Magufuli akikagua moja ya vitendea kazi katika kituo cha Mfumo wa Rada cha
Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.
Na Dianarose Shirima-Maelezo
Rais wa Jamuhuri ya Muungano
wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli amezindua RADA za usafiri wa Anga
katika uwanja wa ndege wa Mwalimu Julius Nyerere (JNICA) na uwanja wa ndege
Kilimanjaro(KIA) ikiwa ni mwendelezo wa mradi uliokuwa umeanzishwa na serikali
ya awamu ya tano kufuatia kuhamasisha safari za ndege na kuendeleza shirika la
ndege la Tanzania(ATCL) uzinduzi huo umefanyika jijini Dar Es Salaam katika
uwanja wa ndege wa Mwalimu Julius Nyerere (JNIA).
Akizungumza na wananchi waliohudhuria katika
uzinduzi huo, Dkt. Magufuli amewapongeza wakandarasi toka Ufaransa waliopewa
mradi huo na kuukamilisha mapema kama alivyohimisa hapo awali.
Balozi wa Ufaransa nchini
Tanzania, Frederic Clavier, amesema
Ufaransa inaunga mkono katika maendeleo ya uchumi wa Tanzania kupitia viwanda
na kusema kuwa Ufaransa ipo tayari kushirikiana na Tanzania katika kuleta
maendeleo na kufikia uchumi wa kati kwa maslahi mapana ya taifa la Tanzania.
Balozi pia akampongeza Rais Dkt. Magufuli pamoja na watanzania kwa jinsi
walivyoungana kwa pamoja ili kuleta maendeleo nchini kwa kasi.
Katika uzinduzi huo, Dkt.
Magufuli amewakaribisha nchi za Afrika na Ulaya kupitisha ndege zao katika anga
la Tanzania kwa kuwathibitishia usalama katika anga la Tanzania na kuwataka
wasiogope wao wapite katika anga la Tanzania na wataongozwa vizuri, Rais
Magufuli amesema kuwa licha ya kuanzisha safari Mumbai, India serikali imelenga
kuanzisha na nchi zingine pia duniani, ikiwemo China na London na kusisitiza
kuwa zingine zitafuata.
Aidha, Rais Magufuli
amewataka watanzania kutokukata tamaa pale zinapotokea changamoto katika
harakati za kuleta maendeleo, akasema
kuwa hata ndege iliyokamatwa huko Afrika
Kusini ni moja ya changamoto katika maendeleo, hivyo watanzania wanatakiwa kuwa
na umoja hata pale changamoto zinapotokea bila kuangalia tofauti zao za kisiasa
kwani maendeleo ya Tanzania hayana chama bali yatafaidisha kila mmoja hata
wajukuu wa kizazi kilichopo sasa.
Rais Magufuli amempongeza
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga, Hamza Johari, kutokana na
uchapakazi mahiri aliouonesha katika nafasi hiyo, pia akasema kwa mwaka wa
fedha uliopita, Mamlaka hiyo ilikusanya mapato ya Billioni 71 kutoka Billion
40 na kwamba mwaka ujao wa fedha
wanatarajia kukusanya kiasi cha shilingi Billioni 82.
0 comments:
Post a Comment