Na Georgr Binagi-GB Pazzo
Serikali
imewataka wakurugenzi wote wa Halmashauri nchini kushughulikia madai ya waalimu
ikiwemo madeni stahiki ili kuhakikisha yanalipwa kwa wakati.
Waziri wa Nchi,
Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI, Mhe. Selemani
Jafo alitoa kauli hiyo Novemba Mosi mwaka huu kwenye Maadhimidho ya Siku ya
Mwalimu Duniani yaliyofanyika kitaifa katika uwanja wa CCM Kirumba Jijini
Mwanza.
Waziri Jafo
ambaye alimwakilisha Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa aliyekuwa mgeni rasmi,
alisema serikali inatambua madai ya waalimu na tayari imeanza kulipa madeni
stahiki ambayo yamefanyiwa uhakiki na kwamba mengine yanaendelewa kuhakikiwa.
Awali
akisoma risala ya waalimu, Katibu Mkuu Chama cha Waalimu Tanzania (CWT), Mwl.
Deus Seif alisema madai ya waalimu ambayo yamefanyiwa uhakiki ni zaidi ya shilingi
bilioni 60 hivyo ni vyema serikali ikalipa madeni hayo kwa wakati.
Aidha
aliomba serikali kushughulikia changamoto za waalimu ikiwemo kupandishwa
madaraja, uhaba wa nyumba za waalimu pamoja na kulipa posho ya kufundishia
(Teaching Allowance), kwani waalimu wanatumia muda mwingi kazini.
Rais wa CWT,
Mwl. Leah Ulaya alisema waalimu wanayo matumaini makubwa na serikali hivyo
wanaamini madeni yao yatashughulikuwa kwa wakati jambo ambalo litaongezea ari
ya ya kufanya kazi kwa bidii.
Naye Mkuu wa
Mkoa Mwanza alitumia fursa hiyo kuwapongeza waalimu kwa kasi yao ya utendaji
kazi na kuwaahidi ushirikiano zaidi huku akionya kwamba “atakayemgusa mwalimu
sisi tunakufa naye”.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI, Mhe. Selemani Jafo, akizungumza kwenye maadhimisho ya Siku ya Mwalimu Duniani 2018 kitaifa Jijini Mwanza.
Rais wa Chama cha Waalimu Tanzania, Mwl. Leah Ulaya akizungumza kwenye maadhimisho hayo.
Katibu Mkuu Chama cha Waalimu Tanzania (CWT), Mwl. Deus Seif akisoma risala kwa niaba ya waalimu kwenye maadhimisho hayo.
Taswira Maadhimisho ya Siku ya Mwalimu Duniani 2018 Jijini Mwanza
Rais wa CWT, Mwl. Leah Ulaya akimkabidhi Waziri Jafo akipokea picha ya Waziri Mkuu Kassim Majaliwa aliyopiga wakati akiwa kiongozi wa chama hicho.
Waziri Jafo akionesha picha hiyo.
Rais wa CWT, Mwl. Leah Ulaya akimkabidhi Waziri Jafo hundi ya shilingi milioni 10 kama mchango wa chama hicho kama rambirambi baada ya ajali ya kivuko cha MV. Nyerere.
Waziri Jafo akimkabidhi Kaimu Katibu Tawala Mkoa Mwanza hundi ya shilingi Milioni 10 aliyopokea kutoka CWT.
Waziri Jafo akisalimiana na Mkuu wa Mkoa Mwanza John Mongella.
Taswira ya picha mbalimbali za mgeni rasmi na viongozi mbalimbali
Tazama video hapa chini
HAPA SERIKALI ITATUE JAMBO MOJA LA MSINGI WALIMU WAPANDISHWE MADARAJA, INAKUWAJE TANGU 2013 HADI LEO YUPO C AJABU MAENEO MENGINE WA 2013 WAMEPANDA JE KWANINI INTEK YOTE ISIPANDE PAMOJA? INAUMIZA SANA.
ReplyDeleteHAPAPO MAHALA PA KUMLAUMU MWALIMU NA IKIZINGATIA WAJIBU WAKE JEANACHUKULIWAJE. MH WAZIRI NA SERIKALALI PAMOJA NA HOJA ZA MSINGI ZOTE KUHUSU BAJETI ONLY ONE THING TO SOLVE TEACHERS PROBLEM IS PROMOTION, OVER
ReplyDeleteKweli kabisa wapandishe madaraja kwanza. Ivi ajira ya 2014 wanastahili kupanda.?
Delete