
Katibu Tawala wa Mkoa wa Simyu,
Bw. Jumanne Sagini akizungumza na watumishi na madiwani wa Halmashauri
ya Wilaya ya Busega katika kikao cha Baraza Maalum la madiwani, Septemba
24, 2019 kwa lengo la kupokea taarifa ya uchunguzi wa matumizi ya fedha
za mkopo shilingi 100,000,000/= kutoka wizara ya Ardhi, Nyumba na
Maendeleo ya Makazi.

Mwenyekiti wa Halmashauri ya
Wilaya ya Busega, Mhe. Vumi Magoti akifungua kikao cha Baraza Maalum la
madiwani kilichofanyika Septemba 24, 2019 kwa lengo la kupokea taarifa
ya uchunguzi wa matumizi ya fedha za mkopo shilingi 100,000,000/= kutoka
wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi.

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri
ya Wilaya ya Busega, Bw. Anderson Njiginya akizungumza kabla ya
kumkaribisha Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo, Mhe. Vumi Magoti kufungua
kikao cha Baraza Maalum la madiwani kilichofanyika Septemba 24, 2019
kwa lengo la kupokea taarifa ya uchunguzi wa matumizi ya fedha za mkopo
shilingi 100,000,000/= kutoka wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya
Makazi.

Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya
ya Busega wakifuatilia kikao cha Baraza Maalum la madiwani
kilichofanyika Septemba 24, 2019 kwa lengo la kupokea taarifa ya
uchunguzi wa matumizi ya fedha za mkopo shilingi 100,000,000/= kutoka
wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi.

Baadhi ya watumishi wa Halmashauri
ya Wilaya ya Busega wakifuatilia kikao cha Baraza Maalum la madiwani
kilichofanyika Septemba 24, 2019 kwa lengo la kupokea taarifa ya
uchunguzi wa matumizi ya fedha za mkopo shilingi 100,000,000/= kutoka
wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi.

Mwenyekiti wa Halmashauri ya
Wilaya ya Busega, Mhe. Vumi Magoti akiteta jambo na Katibu Tawala wa
Mkoa wa Simyu, Bw. Jumanne Sagini katika kikao cha Baraza Maalum la
madiwani kilichofanyika Septemba 24, 2019 kwa lengo la kupokea taarifa
ya uchunguzi wa matumizi ya fedha za mkopo shilingi 100,000,000/= kutoka
wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi.


Baadhi ya viongozi wakifuatilia
kikao cha Baraza Maalum la madiwani kilichofanyika Septemba 24, 2019
kwa lengo la kupokea taarifa ya uchunguzi wa matumizi ya fedha za mkopo
shilingi 100,000,000/= kutoka wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya
Makazi.

Diwani wa Kata ya Mkula,
Mhe.akichangia hoja katika kikao cha Baraza Maalum la madiwani
kilichofanyika Septemba 24, 2019 kwa lengo la kupokea taarifa ya
uchunguzi wa matumizi ya fedha za mkopo shilingi 100,000,000/= kutoka
wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi.
……………………..
Na Stella Kalinga, Simiyu
Uongozi wa Mkoa wa Simiyu umebaini
Ubadhilifu wa kiasi cha shilingi 55,580,000/= ambazo ni sehemu ya
mkopo uliotolewa na Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa
Ajili ya utekelezaji wa Mradi wa Urasimishaji wa makazi (Viwanja) 3700
katika kata nne za Halmashauri ya Wilaya ya Busega uliofanywa na
Watumishi wanne wa Halmashauri hiyo.
Hayo yamebainishwa na Katibu
Tawala wa Mkoa, Bw. Jumanne Sagini wakati akiwasilisha taarifa ya
uchunguzi wa matumizi ya fedha za mradi huo katika kikao cha Baraza
Maalum la madiwani kilichofanyika Septemba 24, 2019 Busega Septemba
06,2019 Nyashimo Busega.
Sagini amewataja watumishi
waliohusika katika ubadhilifu huo kuwa ni Mkurugenzi wa Halmashauri,
Anderson Njiginya, Mkuu wa Idara ya Ardhi, Magesa Magesa, msimamizi wa
mradi Raymond Mahendeka na mhasibu wa mradi,Augustina Kitau na kuwataka
kurejesha fedha hizo mara moja na kushauri mamlaka zao za nidhamu
kuwachukulia hatua kwa mujibu wa sheria
Sagini ameongeza kuwa timu ya
uchunguzi imebaini mapungufu mbalimbali katika matumizi ya fedha hizo
ikiwa ni pamoja na ukikwaji wa sheria, kanuni na taratibu za fedha,
ukiukwaji wa masharti ya mkataba, ukiukwaji wa sheria kanuni na taratibu
za manunuzi ya Umma, udanganyifu na uzembe na usimamizi dhaifu wa
Mradi.
“Kutokana na mapungufu
yaliyobainishwa katika uchunguzi huu Uongozi wa mkoa unaelekeza
watumishi waliohusika warejeshe fedha hizo haraka ili mradi utekelezwe
kama ilivyokusudiwa na tunashauri mamlaka za nidhamu zichukue hatua
stahiki kwa watumishi hao kwa mujibu wa sheria na taratibu za Utumishi
wa Umma,” alisema Sagini.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya
Wilaya ya Busega, Mhe. Vumi Magoti amewashukuru viongozi wa Mkoa kutuma
wataalam wa Mkoa kufanya uchunguzi wa matumizi ya fedha za mradi na
kumuagiza Mkurugenzi kuanzisha utaratibu wa kuwachukulia hatua watumishi
waliohusika walio chini ya mamlaka yake kama viongozi wa mkoa
walivyoelekeza.
Diwani wa Kata ya Mkula, Mhe,
Goodluck Nkalango amesema madiwani wa Halmashauri ya Busega wakiwemo
wajumbe wa kamati inayoshughulikia masuala ya ardhi hawakushirikishwa
katika utekelelezaji wa mradi wa urasimishaji, makazi jambo ambalo
lilipelekea wananchi kutokuwa na taarifa sahihi za mradi ikiwemo
utaratibu wa kuchangia gharama za upimaji.
Kwa upande wake Naibu Mkuu wa
TAKUKURU Mkoa wa Simiyu, Bw. Alex Mpemba amesema TAKUKURU imepokea
taarifa ya Kamati ya Uchunguzi na itaanza kuifanyia kazi mara moja kwa
lengo la kuthibitisha makosa ya jinai kwa waliohusika.
“Tumeipokea taarifa ya
uchunguzi kupitia kikao cha baraza la dharura na kwa sababu wenzetu wa
ukaguzi wamemaliza kazi yao na sisi tutaanzia pale walipoishia kwa lengo
la kuthibitisha makosa ya jinai,” alisema Mpemba.
Halmashauri ya Wilaya ya Busega
ilipokea mkopo wa shilingi 100,000,000/=kutoka Wizara ya Ardhi
kutekeleza Mradi wa urasimishaji wa makazi viwanja 3700 katika kata za
Mwamanyili, Mkula, Kiloleli na Lamadi; kwa mujibu wa taarifa ya
Uchunguzi hadi kufikia Septemba 06, 2019 utekelezaji wa mradi ulikuwa
umefikia asilimi 8.5 na fedha zilizokuwa zimetumika ni asilimia 98.
0 comments:
Post a Comment