Bodi ya korosho Tanzania, inapenda
kuwaarifu wadau wote wa Tasnia ya Korosho nchini kuwa Mkutano Mkuu wa Wadau wa
Mwaka2019 utafanyika tarehe 03 Oktoba, 2019 kuanzia saa 2:30 asubuhi katika
ukumbi wa mikutano wa Benki kuu Tanzania(BOT) Jijini Dar es Saalam.
Mgeni Rasmi katika mkutano huo
anatarajiwa kuwa Waziri wa Kilimo Mhe. Japhet Ngailonga Hasunga(Mb).
Pamoja na mambo mengine katika mkutano huo,mada mbalimbali zitawasilishwa
zikiwemo zinazohusu maendeleo ya Tasnia ya Korosho hapa nchini.
Waalikwa wanaombwa wajigharanie
kuhudhuria Mkutano huo muhimu kwa usafiri,malazi,chakula na kadhalika.Bodi ya
Korosho Tanzania itagharamia chakula na viburudisho wakati wa Mkutano.
Barua rasmi za mwaliko zitatumwa kwa
waalikwa wote. Wadau waliopata mwaliko rasmi ndiyo wanaokaribishwa Mkutano huo.Wale
ambao hawana mwaliko rasmi wa Bodi ya Korosho Tanzania hawataruhusiwa kushiriki
kwenye Mkutano na Bodi haitahusika na usumbufu utakaowapata
Hivyo inasisitiza kuwa, kila mshiriki
afike na barua yake ya mwaliko.
Tagazo hili limetolewa Na;
KAIMU MKURUGENZI MKUU,
BODI YA KOROSHO TANZANIA
S. L.P 533,
MTWARA
0 comments:
Post a Comment