Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa
akizindua Urasimishaji wa Lugha za Alama Tanzania katika Kilele cha
Maadhimisho ya Wiki ya Viziwi Duniani kwenye uwanja wa Kichangani,
Kihesa mjini Iringa, Septemba 28, 2018. Kushoto ni Naibu Waziri Ofisi
ya Waziri Mkuu, Stella Ikupa na kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Ally
Happy. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa
akionyesha nakala za andiko la Urasimishaji wa Lugha za Alama
Tanzania aliouzindua katika Kilele cha Maadhimisho ya Wiki ya Viziwi
Duniani kwenye uwanja wa Kichangani, Kihesa mjini Iringa, Septemba 28,
2018. Kushoto ni Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Stella Ikupa na
kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Ally Happy. (Picha na Ofisi ya Waziri
Mkuu
Baadhi ya washiriki wa Maadhimisho
ya Kilele cha Wiki ya Viziwi Duniani wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim
Majaliwa wakati alipowahutubia kwenye uwanja wa Kichangani, Kihesa
mjini Iringa, Septemba 28, 2019. (Picha na OIfisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa
akiwapungia washiriki wa Kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Viziwi
Duniani kabla ya kuhutubia kwenye uwanja wa Kichangani, Kihesa mjini
Iringa Septemba 28, 2019. Kulia ni Mkalimani wa Lugha ya Alama,
Jonathan Livingstone. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
0 comments:
Post a Comment