
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri
Mkuu anayeshughulikia Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu
Mhe. Jenista Mhagama akisalimiana na Mkuu wa Wilaya ya Chemba, Mhe.
Saimon Ondunga mara baada ya kuwasili wilayani hapo kwa lengo la
kutembelea Vitalu nyumba vilivyojengwa katika wilaya hiyo pamoja na
kukagua maendeleo ya mafunzo kwa vijana kupitia Teknolojia ya kilimo cha
Kitalu Nyumba (Green House).

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri
Mkuu anayeshughulikia Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu
Mhe. Jenista Mhagama akizungumza na Viongozi wa Wilaya ya Chemba mara
baada ya kuwasili Walayani hapo kwa lengo la kukagua maendeleo ya
mafunzo kwa vijana kupitia teknolojia ya Kitalu Nyumba.

Mkuu wa Wilaya ya Chemba, Mhe.
Saimon Ondunga akieleza jambo kwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu
(Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama
alipofanya ziara katika wilaya hiyo.

Baadhi ya Viongozi wa Wilaya ya
Chemba wakimsikiza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia
Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama
(hayupo pichani) alipofanya ziara ya kukagua maendeleo ya mafunzo kwa
vijana kupitia teknolojia ya Kitalu Nyumba katika wilaya hiyo.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri
Mkuu anayeshughulikia Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu
Mhe. Jenista Mhagama akizungumza na wanagenzi walionufaika na mradi wa
Kitalu Nyumba pamoja na wakazi wa Kata ya Kambi ya Nyasa kuhusu programu
ya ukuzaji ujuzi kupitia teknolojia ya Kitalu nyumba.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri
Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista
Mhagama akikagua sehemu ya kuvuta maji kutoka kwenye chanzo cha maji
alipofanya ziara ya kukagua mafunzo kwa vijana kupitia teknolojia ya
Kitalu Nyumba. Kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Chemba, Mhe. Saimon Ondunga.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri
Mkuu anayeshughulikia Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu
Mhe. Jenista Mhagama akizungumza na vijana walionufaika na mradi huo
katika Kata ya Mnenia alipofanya ziara ya kukagua maendeleo ya mafunzo
kwa vijana hao.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri
Mkuu anayeshughulikia Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu
Mhe. Jenista Mhagama akikagua miche ya Nyanya pamoja na mfumo wa
umwagiliaji wa matone katika Kitalu Nyumba kimoja wapo kilichojegwa
katika Kata ya Mnenia, Halmashauri ya Kondoa Mjini. Kushoto ni Diwani wa
Kata hiyo Bw. Adam Ieria.

Afisa Kilimo wa Halmashauri ya
Kondoa Bw. Juvenal Mvumi akipokea maagizo kutoka kwa Waziri wa Nchi,
Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira
na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama kuhusu mradi huo alipotembea kwa
lengo la kujionea maendeleo ya vijana waliopatiwa mafunzo ya kilimo
kupitia teknolojia ya Kitalu Nyumba.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri
Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista
Mhagama akiwa kwenye picha ya pamoja na Vijana walionufaika na Programu
ya ukuzaji ujuzi kupitia teknolojia ya Kitalu Nyumba.
PICHA ZOTE NA OFISI YA WAZIRI MKUU
(KAZI, VIJANA, AJIRA NA WENYE ULEMAVU)
………………..
Na; Mwandishi Wetu
Serikali kupitia Ofisi ya Waziri
Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu imefanikiwa kuwawezesha
vijana wapatao 18,000 kunufaika na mafunzo ya Kilimo cha kisasa kwa
teknolojia ya kitalu nyumba (Green house).
Hayo yamesemwa na Waziri wa Nchi,
Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira
na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama alipotembelea na kukagua maendeleo
ya mafunzo hayo kwa vijana katika Wilaya ya Chemba na Kondoa, Jijini
Dodoma.
Alisema kuwa Serikali kupitia
Ofisi ya Waziri Mkuu iliamua kuanzisha Programu ya kukuza ujuzi nchini
kwa lengo la kuwawezesha vijana kupata ujuzi wa kutosha ambao
utakaowasaidia kufanya shughuli zenye tija na zitakazowawezesha
kujikwamua kuichumi.
“Programu hii ya Kilimo cha kisasa
kupitia teknolojia ya Kitalu Nyumba ni sahihi kwa vijana kwa kuwa aina
hiyo ya kilimo kitawahamasisha vijana ambao ndio nguvu kazi ya Taifa
kupenda na kushiriki kwa wingi kwenye kilimo cha aina hiyo,” alisema
Mhagama
Alieleza kuwa mradi huo ulikusudia
kutekelezwa kwenye Halmashauri zote nchini ambapo awamu ya kwanza
imefanikiwa kuwafikia vijana katika Mikoa 12 na Halmashauri 83 walioweza
kupata ujuzi na stadi za kazi ikionesha jitihada za Serikali katika
kutatua changamoto ya jira kwa vijana.
“Jumla ya vijana 100 katika kila
halmashauri wameweza kujifunza kati yao vijana 20 wamejifunza namna ya
kujenga vitalu nyumba na vijana 80 wamejifunza shughuli za kilimo katika
kitalu nyumba,” alisema Mhagama
Aliongeza kuwa mradi huo
umewajengea vijana hamasa katika kujishughulisha kwenye kilimo kwa kuwa
wataweza kulima katika eneo dogo na kupata mazao kwa wingi ambayo
wataweza kuuza nje ya nchi ama kwenye viwanda vilivyopo nchini.
“Sehemu kubwa ya mazao
mtakayozalisha kwenye vitalu nyumba kama vile Mbogamboga, Matango,
Nyanya, Hoho ni rahisi kupata soko nje ya nchi na kilimo cha aina hiyo
akisubiri msimu huu ni wa kupanda mazao fulani,” alisema Mhagama
Aidha Waziri Mhagama alitoa
maagizo kwa viongozi wa Halmashauri zilizonufaika na mradi huo
kuhakikisha wanasimamia ipasavyo shughuli zinazoendelea, ikiwemo
kuwapatia vijana fursa za mitaji kupitia Mikopo ya halmashauri itakayo
wawezesha vijana kutengeza vitalu nyumba vyao binafsi sambamba na
kuwahamasisha kuanzisha viwanda vidogo vitakavyokuwa vinazalisha
malighafi zitokanazo kwenye vitalu nyumba hivyo.
“Halmashauri zote zilizonufaika na
mradi huu zihakikishe zinatengeneza mfumo madhubuti utakao hakikisha
mradi huo unakuwa endelevu pamoja na kuwahamasisha vijana wengi ili
waweze kunufaika na mafunzo hayo,” alisisitiza Mhagama.
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya
Chemba, Mhe. Simon Odunga aliahidi Mhe. Waziri kusimamia ipasavyo mradi
huo ikiwemo kuwawezesha vijana na kuwahamasisha vijana wengine kushiriki
kwa wingi kwenye teknolojia hiyo ya Kilimo cha Kitalu nyumba.
“Tutaunga mkono jitihada za
Serikali katika kuwawezesha vijana, tunaahidi kutunza mradi huu ili
kusaidia wananchi wa chemba kuweza kunufaika nao,” alisema Odunga
Naye mmoja wa vijana walionufaika
na mafunzo hayo Bw. Juma Ramadhani alisema kuwa mafunzo hayo yamekuwa
chachu kwao na yatawasaidia kuondokana na umaskini kwa kuwa wameweza
kujifunza njia bora za kilimo.
“Tunamshukuru Mhe. Rais, Dkt. John
Magufuli kwa kutuletea mradi huu inaonesha namna Rais wetu
anavyotupigania vijana, tunahaidi kutumia ujuzi tuliopata kuwaelimisha
vijana wenzetu ili na wao waweze kunufaika pia,” alisema Ramadhani
Katika ziara hiyo Waziri wa Nchi,
Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira
na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama aliweza kutembelea na kukagua
maendeleo ya mafunzo kwa vijana kupitia Teknolojia ya kilimo cha Kitalu
Nyumba (Green House) katika Wilaya ya Chemba na Kondoa.
0 comments:
Post a Comment