
Leo Septemba 17, 2019 Naibu Spika Dkt.
Tulia Ackson amezindua rasmi tawi la Wakereketwa wa Umoja wa Wanawake wa CCM
Tanzania (U.W.T) Kata ya Ruanda, mkoani Mbeya.
Tawi hilo limezinduliwa ikiwa ni
sehemu ya uimarishaji wa Chama Cha Mapinduzi Mkoani Mbeya na katika eneo hilo la
Ruanda pia ni Wafanyabiashara wa soko dogo la Darajani tawi la Mkapa.
Akizungumza wakati akifungua Tawi
hilo la wakareketwa wa UWT Kata ya Ruanda Dkt Tulia ameahidi kuwasaidia
kuboresha miundombinu iliyo mibovu katika soko hilo pamoja na kuwawezesha
kupata mikopo yenye riba nafuu ili kuwawezesha kuendeleza biashara zao kwa
ufanisi mkubwa.
“Ndugu zangu wamesoma risala hapa yenye
changamoto kubwa mbili ambazo ni pamoja na ubovu wa miundombinu haswa katika
kipindi cha mvua, niwaahidi kwamba tutasaidiana kuezeka vizuri eneo hili ili
kuondoa changamoto hiyo” Alikaririwa Dkt Tulia na kuongeza kuwa
“Changamoto ya pili imetajwa ni
kukosekana kwa mikopo yenye riba nafuu, nitawaagiza wafanyakazi wa taasisi ya
Tulia Trust waje hapa ili waweze kuwasikiliza, kuwashauri na kuwawezesha kupata
hiyo mikopo ili msipate tena kikwazo chochote cha kuwawezesha kufanya biashara
zenu”- Alisema
MWISHO
0 comments:
Post a Comment