Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe Kangi Lugola akizungumza na wandishi wa habari (hawapo pichani) ofisini kwake jijini Dodoma kuhusu hali ya kiusalama nchini
………………
Na.Alex Mathias,Dodoma
Waziri wa Mambo ya ndani ya Nchi Mhe.Kangi Lugola amemtahadharisha na Kumwonya Mwanaharakati huru Cyprian Musiba kuacha kuwaaminisha watanzania kuwa Serikali inamtumia.
Hayo ameyasema jijini Dodoma Wakati akizungumza na Waandishi wa Habari ofisini kwake amesema kuwa Mwanaharakati Cyprian Musiba serikali haimtumii na mambo yake hayabarikiwi na Serikali bali ni matakwa yake binafsi.
“Kuna mwanaharakati huru Musiba anawadanganya watanzania kuwa serikali ina mtumia mpaka baadhi ya viongozi mbalimbali na Watanzania inafikia hatua ya kumwogopa,nataka kuwafahamisha watanzania serikali haimtumii endapo ataendelea kujigamba namna hiyo serikali itamchukulia hatua za kisheria”Amesema Lugola.
Lugola amesema kuna baadhi ya Watanzania wakiwemo viongozi mbalimbali wamekuwa wakiaminishwa na Mwanaharakati huyo kuwa serikali inamtumia ambapo amesema hayo ni maneno yasiyokuwa ya kweli.
Hivyo Serikali kupitia Wizara ya Mambo ya ndani imesema endapo Mwanaharakati huru Cyprian Musiba ataendelea kuvuka mipaka kwa kuwaaminisha watanzania kuwa anatumiwa na serikali ,serikali itamchukulia hatua kali za kisheria.
Hata hivyo Aidha,Lugola amewatahadharisha baadhi ya watu ambao wamekuwa wakitumia majina ya viongozi na Mitandao kutapeli watu wengine ambapo amesema Serikali imejipanga kukabiliana na tatizo hilo.
0 comments:
Post a Comment