Msimamizi wa Uchaguzi wa Serikali
za Mitaa, katika Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi, Eng. Wilbert Siogopi
Makala akila kiapo mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi Mwandamizi wa Mahakama
ya Wilaya ya Bariadi, Mhe. Mary Mrio(kushoto), zoezi ambalo limefanyika
Septemba 12, 2019 Mjini Bariadi na kushuhudiwa na Katibu Tawala wa Mkoa
wa Simiyu, Bw. Jumanne Sagini.
Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu,
Bw. Jumanne Sagini,(kushoto walioketi) akiwa katika picha ya pamoja na
Wasimamizi wa chaguzi wa Serikali za Mitaa baada ya wasimimizi hao
kuapishwa ya Hakimu Mkazi Mfawidhi Mwandamizi wa Mahakama ya Wilaya ya
Bariadi, Mhe. Mary Mrio(kushoto), zoezi ambalo limefanyika Septemba 12,
2019 Mjini Bariadi na kushuhudiwa na Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu,
Bw. Jumanne Sagini.
Bi . Amina Mbwambo msimamizi wa
Uchaguzi wa Serikali za Mitaa katika Halmashauri ya Wilaya ya Itilima
akizungumza kwa niaba ya wenzake mara baada ya kuapishwa ya Hakimu
Mkazi Mfawidhi Mwandamizi wa Mahakama ya Wilaya ya Bariadi, Mhe. Mary
Mrio(kushoto), zoezi ambalo limefanyika Septemba 12, 2019 Mjini Bariadi
na kushuhudiwa na Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bw. Jumanne Sagini.
Hakimu Mkazi Mfawidhi Mwandamizi
wa Mahakama ya Wilaya ya Bariadi, Mhe. Mary Mrio(kushoto) akizungumza na
wasimamizi wa Uchaguzi wa Serikali za Mitaa mara baada ya kuwaapisha
Septemba 12, 2019 Mjini Bariadi na kushuhudiwa na Katibu Tawala wa Mkoa
wa Simiyu, Bw. Jumanne Sagini.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya mji
wa Bariadi, Bw. Melkizedeck Humbe akitoa neno kwa wasimamizi wa uchaguzi
wa Serikali za Mitaa ambao waliapiswa Septemba 12, 2019 Mjini Bariadi
na Hakimu Mkazi Mfawidhi Mwandamizi wa Mahakama ya Wilaya ya Bariadi,
Mhe. Mary Mrio na kushuhudiwa na Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bw.
Jumanne Sagini.
********************************
|
Na Stella Kalinga, Simiyu RS
Wasimamizi wa Uchaguzi wa Serikali
za Mitaa utakaofanyika Novemba 24, 2019 kutoka katika Halmashauri sita
za Mkoa wa Simiyu wameapishwa Septemba 12, 2019 Mjini Bariadi, ambapo
Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bw. Jumanne Sagini amewataka wazingatie
sheria, kanuni, taratibu na miongozo katika uchaguzi huo ili kuepusha
malalamiko yasiyo ya lazima.
Sagini amesema wasimamizi hao
wanapaswa kutambua kuwa wamepewa jukumu zito ambalo linahitaji umakini
wa hali ya juu na utulivu wa akili, hivyo ni vema wakasoma na kuzipitia
tena sheria, kanuni na miongozo ya uchaguzi wa Serikali za Mitaa
walizopewa ili wazielewe na waweze kufanya kazi bila kubabaika.
“Kumbukeni kuwa Uchaguzi huu
unaweka msingi na maandalizi ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2020 hivyo ni
imani yangu kuwa kila mmoja wenu atakahakikisha anazingatia sheria,
kanuni,miongozo na taratibu zilizotolewa ili kuepusha malalamiko yasiyo
ya lazima; matarajio yangu ni kwamba mtaishi viapo mlivyoapa leo”
alisema Sagini.
Aidha, Sagini amewataka
wasimamizi hao kujiepusha na ushabiki wa kisiasa kwa kuwa wao kama
wasimamizi ni waamuzi, hivyo hawapaswi kwa namna yoyote kujihusisha na
masuala ya ushabiki wa vyama vya kisiasa, ili waaminiwe kuwa wanaweza
kutoa haki; watakaobainika kujihusisha na itikadi za kisiasa
watachukuliwa hatua za kinidhamu.
Akizungumza mara baada ya
kuwaapisha wasimamizi hao, Hakimu Mkazi Mfawidhi Mwandamizi wa Mahakama
ya Wilaya ya Bariadi, Mhe. Mary Mrio amewataka wasimamizi hao kuishi
viapo vyao na kuhakikisha wanafanya majukumu yao kwa uadilifu na kwa
mujibu wa sheria kwa sababu watakapokiuka sheria , kanuni na taratibu
wataiingiza serikali kwenye gharama.
Kwa upande wao wasimamizi wa
uchaguzi wa Serikali za Mitaa mkoani Simiyu mwaka 2019 wamesema
watahakikisha wanatekeleza wajibu na majukumu waliyopewa kwa mujibu wa
sheria, kanuni, taratibu na miongozo kama walivyoelekezwa.
“Tunashukuru kwa kuaminiwa
katika jukumu hili nyeti la Kitaifa, tunaamini kama tulivyoelekezwa kama
wasimamizi tutasimamia yale tunayopaswa tutafanye kwa mujibu wa sheria,
kanuni na taratibu na tutaviishi viapo vyetu tulivyoapa siku ya leo na
kutimiza wajibu wetu kama watumishi wa Umma” alisema Wilbert Siogopi
msimamizi wa Uchaguzi Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi.
“Tunaahidi kwamba
tutakitekeleza kiapo tulichoapa leo, tunafahamu kuwa kazi hii ngumu
lakini kama mlivyotuasa tukiamua kwa dhati kabisa tukapitia sheria,
kanuni, taratibu na miongozo ya uchaguzi tutafanya kazi inayotarajiwa”
alisema Bi . Amina Mbwambo msimamizi wa Uchaguzi wa Serikali za Mitaa
katika Halmashauri ya Wilaya ya Itilima.
Uchaguzi wa Serikali za Mitaa
unatarajiwa kufanyika Novemba 24, 2019 nchini kote ambapo katika Mkoa wa
Simiyu utahusisha Vijiji 470, Mitaa 92 na Vitongoji 2652.
0 comments:
Post a Comment