
Kaimu Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri
Mkuu (Waziri Mkuu na Bunge), Parkshard Mkongwa akieleza umuhimu wa
ujumuishwaji wa masuala ya watu wenye ulemavu katika mipango na
bajeti ngazi ya wizara wakati wa kikao cha Menejimenti ya wizara hiyo
na , viongozi kutoka SHIVYAWATA na Shirika la Kimataifa la ADD, leo
jijini Dodoma, tarehe 16 Septemba, 2019, kulia kwake ni Kaimu Mkuu wa
Kitengo cha Watu wenye Ulemavu wa Ofisi hiyo, Filbert Kawemwamwa.

Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Watu
wenye Ulemavu wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Filbert Kawemwamwa. wa akieleza
umuhimu wa ujumuishwaji wa masuala ya watu wenye ulemavu katika
mipango na bajeti ngazi ya wizara wakati wa kikao cha Menejimenti ya
wizara hiyo na , viongozi kutoka SHIVYAWATA na Shirika la Kimataifa la
ADD, leo jijini Dodoma, tarehe 16 Septemba, 2019, kushoto kwake ni Kaimu
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Waziri Mkuu na Bunge), Parkshard
Mkongwa.

Baadhi ya wajumbe wa Menejimenti
ya Ofisi ya Waziri Mkuu wakifuatilia kikao cha Menejimenti ya wizara
hiyo na , viongozi kutoka SHIVYAWATA na Shirika la Kimataifa la ADD,
wakati wa kujadili namna ya ujumuishwaji wa masuala ya watu wenye
ulemavu katika mipango na bajeti ngazi ya wizara leo jijini Dodoma,
tarehe 16 Septemba, 2019.

Mwenyekiti wa SHIVYAWATA, Ummy
Ndeliyanaga, akieleza umuhimu wa ujumuishwaji wa masuala ya watu
wenye ulemavu katika mipango na bajeti ngazi ya wizara wakati wa kikao
cha Menejimenti ya wizara hiyo na , viongozi kutoka SHIVYAWATA na
Shirika la Kimataifa la ADD, leo jijini Dodoma, tarehe 16 Septemba,
2019.

Mkurugenzi wa Programu, Shirika la
Kimataifa la ADD, Rose Tesha, akieleza umuhimu wa utetezi wa pamoja wa
masula ya watu wenye ulemavu wakati wa kikao cha Menejimenti ya wizara
hiyo na , viongozi kutoka SHIVYAWATA na Shirika la Kimataifa la ADD, leo
jijini Dodoma, tarehe 16 Septemba, 2019.

Baadhi ya wajumbe wa Menejimenti
ya Ofisi ya Waziri Mkuu wakifuatilia kikao cha Menejimenti ya wizara
hiyo na , viongozi kutoka SHIVYAWATA na Shirika la Kimataifa la ADD,
wakati wa kujadili namna ya ujumuishwaji wa masuala ya watu wenye
ulemavu katika mipango na bajeti ngazi ya wizara leo jijini Dodoma,
tarehe 16 Septemba, 2019.

Mkalimani kwa kutumia lugha ya
alama, Edna James, akieleza umuhimu wa utetezi wa pamoja wa masula ya
watu wenye ulemavu wakati wa kikao cha Menejimenti ya wizara hiyo na ,
viongozi kutoka SHIVYAWATA na Shirika la Kimataifa la ADD, leo jijini
Dodoma, tarehe 16 Septemba, 2019.

Baadhi ya wajumbe wa Menejimenti
ya Ofisi ya Waziri Mkuu wakimsikiliza Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Watu
wenye Ulemavu wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Filbert Kawemwamwa. wakati wa
kikao cha Menejimenti ya wizara hiyo na , viongozi kutoka SHIVYAWATA na
Shirika la Kimataifa la ADD, wakati wa kujadili namna ya ujumuishwaji
wa masuala ya watu wenye ulemavu katika mipango na bajeti ngazi ya
wizara leo jijini Dodoma, tarehe 16 Septemba, 2019.
………………….
Serikali kupitia Ofisi ya Waziri
Mkuu (Kazi, Ajira, Vijana na Watu wenye Ulemavu) imewahakikishia watu
wenye ulemavu nchini kupitia Shirikisho la Watu wenye Ulemavu Tanzania
(SHIVYAWATA) kuwa itaendelea kujumuisha masuala ya watu wenye ulemavu
katika mipango na bajeti kwa ngazi ya Wizara ili kuweza kuhakikisha watu
wenye ulemavu wanapata huduma bora na stahiki.
Akiongea wakati wa kikao kazi
kuhusu ushawishi na utetezi pamoja na ujumuishwaji wa masuala ya watu
wenye ulemavu katika mipango na bajeti ngazi ya wizara, kilicho
washirikisha Menejimenti ya Ofisi ya Waziri Mkuu, viongozi kutoka
SHIVYAWATA na Shirika la Kimataifa la ADD, leo jijini Dodoma, tarehe 16
Septemba, 2019, Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Watu wenye Ulemavu wa Ofisi
hiyo, Filbert Kawemwamwa amebainisha kuwa lengo la kikao hicho ni
kuibua mikakati ya ujumuishaji, usimamizi na utekelezaji wa masuala watu
wenye ulemavu nchini.
“Katika kuhakikisha kuwa mipango
na bajeti ngazi ya wizara zinajumuisha masuala ya watu wenye ulemavu
tutaendelea kukutana na wizara nyingine saba za kisekta ili kuweza
kuhakikisha mipango ya maendeleo yao inaweza kuwafikia watu wenye
ulemavu hasa walio vijijini, kwa kuzingatia Sera ya Taifa ya Maendeleo
na Huduma ya Watu wenye Ulemavu ya Mwaka 20014” amesistiza Kawemwamwa
Awali akiongea katika kikao hicho
Mwenyekiti wa Shirikisho la Watu wenye Ulemavu Tanzania (SHIVYAWATA),
Ummy Ndeliyanaga, ameshukuru kwa jitihada zinazofanywa na serikali ya
awamu ya Tano, inayoongozwa na Dkt. John Pombe Magufuli katika kuboresha
huduma za msingi za watu wenye Ulemavu nchini, hata hivyo amebainisha
kuwa wanazo hoja za msukumo kumi ambazo anaamini utekelezaji wake
ukikamilika zitaboresha huduma na maendeleo kwa watu wenye ulemavu
nchini.
“Tayari serikali kupitia ofisi ya
Waziri Mkuu imeshaunda madawati ya watu wenye ulemavu katika wizara na
taasisi zake tunaomba majukumu ya maofisa hao yapitiwe upya, pia
uanzishwaji wa mchakato wa uundwaji wa mfuko wa Kitaifa wa watu wenye
Ulemavu, masuala mengine ni kuanzishwa kwa rejista ya watu wenye
ulemavu, kupitia sheria ya watu wenye ulemavu, Makakati wa ufukiwaji wa
3% ya watu wenye ulemavu kwenye kila taasisi inayo ajiri watu kuanzia
20” amesema Ndeliyanaga
Ameongeza kuwa wanaomba serikali
isisimamie ukamilishwaji wa mchakato wa uandaaji wa taarifa ya
utekelezaji wa mkataba wa umoja wa mataifa wa haki za watu wenye
Ulemavu, pamoja na kuwaelekeza waajiri wote kuandaa na kuwasilisha
taarifa ya mwaka ya hali ya ajira kwa watu wenye ulemavu katika taasisi
zao, pia ukamilshawaji wa mwongozo wa viwango vya ufikikaji wa miundo
mbinu, Mipango ya Kisekta pamoja na Baraza la ushauri la watu wenye
ulemavu kuhakikisha linafanya kazi kikamilifu.
Kwa upande wake, Mkurugenzi wa
Programu, Shirika la Kimataifa la ADD, Rose Tesha, amefafanua kuwa
shirika hilo limeamua kuunga juhudi za serikali za kuwahudumua watu
wenye Ulemavu kwa kuwezesha SHIVYAWATA kukutana na wizara za kisekta ili
kuweza kuhakikisha kuwa wanaweza kuzitetea vizuri fursa na haki za watu
wenye ulemavu hapa nchini.
Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Ajira,
Vijana na Watu wenye Ulemavu) iliundwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania kupitia Tangazo kwenye gazeti la Serikali Na.144 la mwezi
Aprili, 2016. Pamoja na majukumu mengine Ofisi hiyo inajukumu la
kusimamia utekelezaji wa sera, sheria, AMiongozo, Kanuni na Viwango vya
Ubora katika utoaji wa huduma za watu wenye ulemavu nchini.
0 comments:
Post a Comment