1."Chama cha Mapinduzi ndicho Chama ndio
chenye ilani inayotekelezwa na ni wajibu wetu kufuatilia na kukagua utekelezaji
wa ilani Hiyo nafasi hawana chama chochote isipokuwa Chama cha Mapinduzi"
-Ndg. Polepole
2.
"Zamani tukishashinda uchaguzi tunapotea hatufuatilii, Mara hii ilani
imesema ni lazima tufuatilie utekelezaji wa Ilani wa CCM kuhakikisha yale
yaliyoahidiwa yanatekelezwa"-Ndg.Polepole
3."Tutawapeleka
Chuo cha uongozi wa Mwl Nyerere ,Viongozi wote
ndani ya Serikali na Chama wafahamu nini maana ya utumishi wa umma ,
nini maana ya utu, nini maana ya haki, nini maana ya utii na unyenyekevu".
-Ndg.Polepole
4."Niombe
rai kwa viongozi wa Chama na Serikali,
wasitoe kauli zinazoashiria uvunjifu wa sheria na Amani" -Ndg.Polepole
5."Kuomba
msamaha si suala la maelekezo, ni suala la utashi , kama kuna mtu amehisi
kukosea, ni hiari yake kuomba msamaha au kutokuomba msamaha"- Ndg Polepole
6."Chama
chetu kinaongozwa na katiba, kanuni na
taratibu zilizowekwa , sio dhambi kiongozi yoyote kufanya ziara ila utaratibu
wa ndani ya Chama ufuatwe-Ndg Polepole
7. Cyprian Musiba hatumwi na Chama cha
Mapinduzi, Kauli za CCM, zinatolewa na mimi katibu wa itikadi na uenezi wa
Chama cha Mapinduzi. Ila Musiba kama mtu yeyote ana uhuru wa kuweka hadharani
maoni yake bila kuvunja sheria za Nchi - Ndg. Polepole
8.
"Asilimia 70 ya wapiga kura ni CCM, ni vigumu kupata mtu ambaye hana
unasaba na CCM kusimamia uchaguzi, umewekwa utaratibu wa kula kiapo wakati wa
kusimamia uchaguzi kuachana na unasaba wa kisiasa"- Ndg. Polepole
9.
"Chama cha Mapinduzi Tunakiri kusema kazi tumeipiga na tunaenda kueleza
kwa wananchi kazi nzuri tumeifanya na hatuna hofu hata
kidogo tutaibuka na ushindi wa kishindo kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa
2019" - Ndg. Polepole
10.
"Kuna watu walibeza tulipokamata mchanga wa dhahabu, naomba rai wajitokeze
hadharani kumuomba radhi kwa Rais magufuli kwani sasa rasmi kampuni ya ACACIA
imekufa duniani na Barrick Gold wamekubali kufanya kazi kwa sheria na kanuni za
Tanzania" - Ndg Polepole
0 comments:
Post a Comment