METDO Tanzania

METDO Tanzania

Friday, September 20, 2019

RAIS DKT.MAGUFULI AMTUMBUA RC MOROGORO

Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi akisoma majina ya viongozi mbalimbali walioteuliwa ama waliobadilishwa vituo na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli Ikulu jijini Dar es salaam leo Septemba 20, 2019
PICHA NA IKULU
*********************************
Rais Magufuli amefanya mabadiliko ambapo, Mkuu wa Wilaya ya Tarime Charles Kabeho, amehamishiwa wilaya ya Chato na Mkuu wa Wilaya ya Chato Msafiri Mtemi amehamishiwa Wilaya ya Tarime.
Rais John Magufuli memteua Lowata Sanare kuwa Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, pia amemteua Musa Masele kuwa Mkuu wa Wilaya ya Malinyi mkoani Morogoro.
Rais Dkt Magufuli ameteua Mabalozi 12 ambao wataiwakilisha Tanzania katika nchi mbalimbali. Uteuzi huo unatokana na vituo hivyo ama kuwa wazi, Mabalozi kumaliza muda wao, kustaafu au kurejeshwa nyumbani ambapo watapangiwa kazi nyingine.
Modestus Kipilimba, aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Usalama wa Taifa (TISS), ameteuliwa kuwa Balozi. Kituo chake cha kazi kitatangazwa baadae.
Majina kamili ya Mabalozi walioteuliwa ni 1. Mohamed Mtonga 2. Dkt. Jilly Maleko 3. Dkt. Benson Bana 4. Meja Jen. (Mst), Anselimu Bahati 5. Prof. Emmanuel Mbennah 6. Maimuna Tarishi 7. Meja Jen. (Mst) Gaudence Milanzi 8. Ali Jabir Mwadini 9. Dkt Modestus Kipilimba 10. Jestas Nyamanga 11. Prof. Dr. Kennedy Gaston 12. Mhandisi Aisha Amour
Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com