Waziri
wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) akiwasilisha Bungeni Jijini Dodoma azimio la
kuridhia itifaki ya Jumuiya ya Maendeleo ya nchi za kusini mwa Afrika kuhusu
kulinda hakimiliki za wagunduzi wa aina mpya za mbegu za mimea (Protocol for Protection
of New Varieties of Plants (Plant Breeders’ Rights) in southern African
Development Community-SADC) leo tarehe 11 Septemba 2019. (Picha Zote Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo)
Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) akiwasilisha Bungeni Jijini Dodoma azimio la kuridhia itifaki ya Jumuiya ya Maendeleo ya nchi za kusini mwa Afrika kuhusu kulinda hakimiliki za wagunduzi wa aina mpya za mbegu za mimea (Protocol for Protection of New Varieties of Plants (Plant Breeders’ Rights) in southern African Development Community-SADC) leo tarehe 11 Septemba 2019.
Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) akijiandaa kwa ajili ya kuwasilisha azimio la kuridhia itifaki ya Jumuiya ya Maendeleo ya nchi za kusini mwa Afrika kuhusu kulinda hakimiliki za wagunduzi wa aina mpya za mbegu za mimea (Protocol for Protection of New Varieties of Plants (Plant Breeders’ Rights) in southern African Development Community-SADC) Bungeni Jijini Dodoma leo tarehe 11 Septemba 2019.
Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo-Dodoma
Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) amewasilisha Bungeni Jijini
Dodoma azimio la kuridhia itifaki ya Jumuiya ya Maendeleo ya nchi za kusini mwa
Afrika kuhusu kulinda hakimiliki za wagunduzi wa aina mpya za mbegu za mimea
(Protocol for Protection of New Varieties of Plants (Plant Breeders’ Rights) in
southern African Development Community-SADC) leo tarehe 11 Septemba 2019.
Akizungumza
wakati wa uwasilishaji huo Waziri Hasunga amesema kuwa Chimbuko la Azimio
hilo ni Mkataba wa kuanzisha Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (Southern
African Development Community -SADC). Ibara ya 22 ya Mkataba wa SADC- (SADC
Treaty), wa mwaka 1992 ambao umebainisha umuhimu wa kuandaa Itifaki za kutoa
miongozo ya ushirikiano kwenye masuala ya maendeleo.
Alisema nchi wanachama wa SADC ziliandaa Itifaki ya SADC ya Kulinda
Hakimiliki za Wagunduzi wa Aina Mpya za Mbegu za Mimea Mwezi
Mei, 2017. Itifaki hiyo iliidhinishwa na
Mawaziri wa Katiba na Sheria wa nchi za SADC Julai, 2017 na baadae
ilithibitishwa na Baraza la Mawaziri wa Kilimo la SADC Agosti, 2017 mjini
Ezulwini, eSwatini. Lengo kuu la Itifaki hiyo ni kutoa mwongozo kuhusu kulinda
Hakimiliki za Wagunduzi wa Aina Mpya ya Mbegu za Mimea ili kuhamasisha ugunduzi
wa mbegu mpya katika Ukanda wa SADC
Mhe Hasunga amesema kuwa hadi
sasa nchi zilizosaini Itifaki hiyo ni saba (7) ikiwemo Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
ambayo ilisaini tarehe 18 Agosti, 2018 wakati wa Mkutano wa nchi wanachama wa
SADC uliofanyika Windhoeck, Namibia. Ambapo, mnamo tarehe 31 Oktoba, 2018
Baraza la Mapinduzi Zanzibar liliridhia mapendekezo ya Serikali ya Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania kuwasilisha Itifaki hiyo Bungeni ili iweze kuridhiwa.
Alisema kuwa itifaki hiyo ina
sehemu 10 ambazo ni sehemu ya kwanza
yenye Ibara 5 inabainisha malengo na mawanda (scope) ya Itifaki hiyo, Sehemu ya
Pili yenye Ibara 5 ambapo Ibara ya 7 inaweka vigezo na masharti ya kuzingatia
katika utoaji wa hakimiliki za wagunduzi wa aina mpya za mbegu za mimea, Sehemu
ya Tatu na Nne zenye Ibara kumi na nne (14) inabainisha utaratibu utakaotumika
katika utoaji wa hakimiliki za wagunduzi wa aina mpya ya mbegu za mimea na
namna ya kushughulikia maombi ya hakimiliki.
Aliongeza kuwa Sehemu ya Tano
inahusu muda wa hakimiliki iliyotolewa chini ya Itifaki ambayo itadumu kwa
miaka ishirini na tano (25) kwa mazao ya miti na jamii ya mizabibu na miaka
ishirini (20) kwa mazao mengine, Sehemu ya Sita, Saba na Nane inahusu utoaji wa
leseni na uhawilishaji wa hakimiliki hizo ambapo Ibara ya 34 inaweka masharti
kwa ajili ya uhaulishaji wa hakimiliki, na Sehemu ya Tisa na Sehemu ya Kumi inahusu
masuala ya jumla ambapo Ibara ya 43 inahusu usuluhishi wa migogoro (Dispute
settlement) na inabainisha kuwa, migogoro kati ya nchi wanachama wa SADC kuhusu
utekelezaji wa Itifaki hiyo iliyoshindwa kupata usuluhishi kwa mazungumzo,
itawasilishwa kwa Mawaziri wa Kilimo na Usalama wa Chakula wa nchi wanachama wa
SADC.
Aidha,
Mhe Hasunga amesema kuwa pamoja na mapendekezo ya kuridhiwa kwa Itifaki hiyo, Azimio
hilo linaweka sharti (Reservation) litakaloiwezesha Tanzania kutolazimika
kutekeleza masharti ya Itifaki ambayo yanaweza kuathiri maslahi ya Taifa.
Utaratibu huu unatambuliwa kimataifa kupitia Sehemu ya Pili ya Itifaki ya
Vienna Convention on the Law of Treaties uliosainiwa mwaka 1969 ambapo Tanzania
ni mojawapo ya nchi zilizoridhia kutumia Mkataba huu tangu tarehe 12 Aprili,
1974.
Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania ni miongoni mwa Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo
ya Nchi za Kusini mwa Afrika (The Southern
African Development Community -SADC) kwa mujibu wa Mkataba ulioianzisha
Jumuiya hii ambao ulisainiwa na Wakuu wa Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo
ya Nchi za Kusini mwa Afrika mnamo 1992;
MWISHO.
0 comments:
Post a Comment