Na.Alex Sonna,Dodoma
Katika kuonekana kuridhishwa na
kasi ya utendaji kazi wa Rais Dkt John Magufuli, wananchi wazalendo
wameendelea kujitokeza hasa baada ya kazi nzuri inayofanywa na Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ambapo mmoja Kati ya wananchi
wazalendo, Bw, Rashidi Kayumbo anasema Sasa ni muda mwafaka kwa Tanzania
kujengwa katika misingi ya Uzalendo.
Anasema kama atapendezwa, Rais wa
nchi Mh. Dkt John Magufuli, ampe nafasi ya kuonana nae uso kwa uso ili
Kama mwananchi mzalendo aweze kutoa ushauri wake sambamba na kuishauri
serikali katika shughuri za maendeleo.
Wakati wa mahojiano na Fullshangwe
blog, Bw. Rashidi Kayumbo amesema kuwa, imefika wakati wa kumshukuru
Mungu kwa kumpata Rais ambaye ni mzalendo na anatetea haki za wanyonge,
hivyo kuomba ridhaa ya kumuomba Mh, Dkt John Magufuli, kumpa ridhaa ya
kwenda kuonana ikulu, na yeye Kama mzalendo aweze kutoa mawazo yake ya
kizalendo.
“Nakuomba mh.Rais Dkt John Pombe
Magufuli anitunuku ya kufika Ikulu kwa ajili ya kuzifikisha hoja zangu,
lakini pia kwa Uzalendo wangu napenda kumhakikishia mhe. Rais Kuna hoja
za msingi katika kuishauri serikali ni wakati huu wa Sasa na Mimi ninayo
maeneo ya kuishauri serikali katika shughuri za maendeleo” amesema
Kayumbo.
Amebainisha Baadhi ya Mambo
aliyowahi kutoa ushauri “Mnamo mwaka 2013 Mimi militia ushauri kwa
mwandishi juu ya uliyokuwa kero katika mzani wa Kihonda Morogoro, barua
ya Wizara katika kuthamini mawazo yangu ni Na BA/307/540/02/15/2013”
“Mwaka 2014 nilipeleka maoni
yangu niliandika barua kwenda Wizara ya ujenzi nilitaka kufanya ziara
na wataalamu katika Baadhi ya barabara za jiji la Dar es saalam
kupunguza msongamano wa mahari barua Na AS/MRS/CO/VOL/38/2014 ya tarehe
12/08/2014” alisema Kayumbo.
Pia ameomba serikali kuitambua
sekta ya ugavi kwa makampuni ya ujenzi alisema sekta hiyo endapo
itatambuliwa na kuhakikisha kila mtu anayefanya kazi hizo kuwa na TIN
namba na EFD Mashine sekta hiyo unaweza kuongeza pato la Taifa kwa
kulipa Kodi hivyo aliomba serikali iitambue sklekta hiyo.
“Ningependa uwepo ulazima wa
kisheria kwa kila supplies kupatiwa mkataba wa mwandishi na kampuni au
mkandalasi anayetaka kupewa huduma ya kupatiwa matilio kwa idadi na
thamani halisi ya fedha na malipo yote yafanyike kupitia A/C za mabenki
Kama kazi nyingine zilivyo” alisema.
Amesema Mamlaka ya Mapato awe
tayari kwanza kupikwa maelezo ya Supplies kulingana na gharama halisi za
kazi Kisha serikali ipokee kiasi chake alisema endapo wazalendo Kama
yeye watapata nafasi wanauwezo wa kukomesha vyanzo vya Mapato
vilivyokuwa havijulikani na vikachangia pato la taifa.
Amesema eneo Lingine analoshauri
serikali kulifanyia kazi ni eneo la vibarua alisema vibarua wengi katika
hii nchi wanalipwa isivyositahiki kwa maeneo mengi alisema kwa nijibu
wa sheria kibarua anatakiwa kulipwa 12,500, lakini kundi hili Mara
nyingi kumekuwa likilipwa elfu 5000,6000 Hadi elf 7000 kwa siku.
Ameshauri ili kumaliza tatizo hilo
ni serikali ianzishe mfumo wa makampuni na makandarasi wote kutumia
fomu za kila siku na kwa kila kibarua ili kuona namna wanavyolipwa pia
ameshauri kuwekwa siku ya wazalendo ili kujengwa mfumo wa kizalendo.
0 comments:
Post a Comment