METDO Tanzania

METDO Tanzania

Friday, September 20, 2019

DKT.MAHENGE:ONGEZEKO LA JOTO DUNIANI HUCHANGIWA NA SHUGHULI ZA BINADAMU



D:\HABARI SEPT.18\MAHENGE.jpg
Na.Faustine Gimu Galafoni,Dodoma.

Imeelezwa kuwa sababu kubwa ya ongezeko la joto kwenye uso wa Dunia ni shughuli ambazo zinafanywa na  Binadamu.
Hayo yamesemwa na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt Binilith Saatano Mahenge wakati akifungua mkutano uliowashirikisha kamati ya kudumu ya Bunge, Viwanda Biashara na mazingira kuhusiana na mabadiliko ya tabia ya nchi katika kuelekea  siku ya Amani Duniani ambayo huadhimishwa kila mwaka ifikapo September 21.
Mahenge
Aidha, amesema  chanzo kikubwa cha wakulima na wafugaji kinatokana na upungufu wa malisho,upungufu wa maji uliotokana na uharibifu wa mazingira ambao uliongeza kasi ya joto katika uso wa Dunia .
Mahenge
Kwa upande wake Clara Mkenya ambaye ni Mratibu Mwakilishi wa shirika la Mazingira la umoja wa Mataifa amesema mabadiliko ya tabia ya nchi na changamoto za kimazingira zimeendelea kuwa halisi kila wakati kuanzia kwa mototo mpaka mtu mzima.
Clara
Akizungumza kwa Niaba ya wabunge Makamu Mwenyekiti wa kamati ya Mazingira na Viwanda Masoud Ally Khamis amesema ziko athari nyingi ambazo zimekuwa zikijitokeza na hiyo ni kutokana na Mabadiliko ya Tabia ya Nchi.
Ally
Maadhimisho ya siku ya Amani Duniani yanakwenda sambaba na kauli mbiu isemayo ‘’hatua zinazotumika kukabiliana na mabadiliko ya tabia ya nchi kwaajili ya kuhakikisha  amani’’
Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com