Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi akisoma majina ya viongozi
mbalimbali walioteuliwa ama waliobadilishwa vituo na Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli Ikulu jijini
Dar es salaam leo Septemba 20, 2019
PICHA NA IKULU
*********************************
Rais Magufuli amefanya mabadiliko
ambapo, Mkuu wa Wilaya ya Tarime Charles Kabeho, amehamishiwa wilaya ya
Chato na Mkuu wa Wilaya ya Chato Msafiri Mtemi amehamishiwa Wilaya ya
Tarime.
Rais John Magufuli memteua Lowata
Sanare kuwa Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, pia amemteua Musa Masele kuwa Mkuu
wa Wilaya ya Malinyi mkoani Morogoro.
Rais Dkt Magufuli ameteua Mabalozi
12 ambao wataiwakilisha Tanzania katika nchi mbalimbali. Uteuzi huo
unatokana na vituo hivyo ama kuwa wazi, Mabalozi kumaliza muda wao,
kustaafu au kurejeshwa nyumbani ambapo watapangiwa kazi nyingine.
Modestus Kipilimba, aliyekuwa
Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Usalama wa Taifa (TISS), ameteuliwa kuwa
Balozi. Kituo chake cha kazi kitatangazwa baadae.
Majina kamili ya Mabalozi walioteuliwa ni
1. Mohamed Mtonga
2. Dkt. Jilly Maleko
3. Dkt. Benson Bana
4. Meja Jen. (Mst), Anselimu Bahati
5. Prof. Emmanuel Mbennah
6. Maimuna Tarishi
7. Meja Jen. (Mst) Gaudence Milanzi
8. Ali Jabir Mwadini
9. Dkt Modestus Kipilimba
10. Jestas Nyamanga
11. Prof. Dr. Kennedy Gaston
12. Mhandisi Aisha Amour
0 comments:
Post a Comment