METDO Tanzania

METDO Tanzania

Saturday, June 13, 2020

TAARIFA KWA UMMA KWA WAKAZI WA HALMASHAURI YA ARUSHA KUHUSU UBORESHAJI WA DAFTARI LA AWALI LA WAPIGAKURA

Na Agnes Geofrey

Tume ya taifa ya uchaguzi kupitia ofisi ya afisa mwandikishaji ambae ni mkurugenzi wa Halimashauri ya jiji la Arusha, imewatangazia wananchi kuwa itaweka wazi daftari la awali la wapiga Kura kwa siku nne kuanzia tarehe 17hadi20 mwaka huu , Katika vituo vilivyotumika wakati wa uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura.

Akitoa taarifa juu ya maelekezo ya uhitimishaji wa uwekaji  wazi daftari Hilo afisa mwandikishaji MSAIDIZI ngazi ya jimbo la Arusha mjini Msena Bina Amesema zoezi Hilo litahusisha watu wote waliojitokeza kujiandiksha mwaka 2015 nakuboresha taarifa zao huku akiongeza kuwa uandikishaji huo utazingatia taratibu zote juu ya kujikinga na gonjwa hatari la corona.

Aidha  Afisa uchaguzi jiji la Arusha Namnyaki Wilfredi Amesema bado Kuna changamoto ya wapigakura takribani 45 ambao picha zao bado hazijaonekana nakuwataka wahusika watakaokosa taarifa zao  kufika shule ya msingi meru ili kushughulikiwa kuanzia tarehe ya uwekaji wazi wadaftari Hilo,kwani wapo kwenye kikao hicho kwa ajili ya kutoa taratibu na maelekezo juu ya daftari Hilo.
Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com