Na Agnes Geofrey
Serikali inaendelea kutafuta ufumbuzi wa changamoto za madereva wa malori mpakani namanga huku wamiliki wakitakiwa huku wamilik wa usafirishaji wakitakiwa kuendelea kuwapatia madereva fedha za kujikimu ili kuepukana na upotevu wa Mali zao.
Akizungumza katika kikao hicho Cha madereva na wamiliki wa malori jijini arusha, Mkuu wa wilaya longido Frank Mwaisumbe amesema kuwa changamoto ni mkwamo wa magari kutoka nchini Kenya kutokana na nchi hiyo kutoruhusu magari ya Tanzania kuingia nchini mwao ikiwa Tanzania imeruhusu.
Amesema kuwa magari yote yameombwa kuegeshwa eneo la Longido ili kuondoa msongamano eneo la namanga ambapo katika kuhakikisha usalama wa magari yenye mlipuko yametengwa kutokana na bidhaa hizo kuweza kulipuka na kuleta madhara kwa wananchi.
Hata hivyo Mkuu huyo amewataka wamiliki wa magari kutoa ushuru Mara moja katika eneo la maegesho hadi pale ufumbuzi wa changamoto hiyo utakapotolewa.
Nae mwakilishi wa wasafirishaji kanda ya kaskazini Zainabu Athuman ameiomba serikali kufanya majadiliano ya wao kupeleka bidhaa zilizopo mpakani ili kuepuka hasara zaidi kwani wanaona swala hili ni vita ya kiuchumi na sio korona.
0 comments:
Post a Comment