METDO Tanzania

METDO Tanzania

Saturday, June 13, 2020

WASAIDIZI WA KISHERIA MKOANI ARUSHA WABORESHA MBINU ZA UTOAJI ELIMU YA KISHERIA

Na Agnes Geofrey

Wasaidizi wa Kisheria mkoa wa Arusha wameanza kutumia mbinu za kutoka elimu juu ya msaada wa kisheria kwa kujirekodi na kusambaza katika vijiji kupia CD, flash, vipaza sauti pamoja na kutumia mitandao ya simu kutokana ugonjwa wa Corona

Akizungumza na waandishi wa Habari Afisa ufuatiliaji na tasmini  Elibahati Maturo kutoka taasisi ya utafiti na usaidizi wa kisheria  katika mkutano wa majadiliano ya pamoja katika kutatua changamoto ya kushindwa kuwafikia wananchi kutokana ugonjwa huo ambapo amesema kuwa mbinu hizo zitawasaidia kufikisha elimu na kuepusha mikusanyiko unaweza kusambaza maambukizi.

Bwana Maturo ameeleza kuwa  kulitokea sintofahamu katika utoaji wa elimu msaada wa sheria kwa jamii kutokana na Corona kwani awali wasaidizi wa kisheria walifanya kazi hiyo kupitia mikusanyiko mbalimbali jambo ambapo liliwasaidia baadhi ya wanajamii kufahamu haki zao na kuepuka migogoro.

Kwa upande wake Hamza Abubakari Katibu wa taasisi ya Taswira ya haki kutoka Halmashauri ya Meru ameeleza kuwa katika jamii kuna migogoro mingi ambayo inatokana na ukosefu wa elimu ya kisheria ambapo kwa sasa kila kata Kuna msaidizi wa kisheria na wanawashirikisha viongozi wa serikali kwanzia ngazi ya kijiji hadi wilaya katika kuwafikia walengwa.

Hata hivyo mradi huo wa kutoa msaada wa kisheria ulianza may 2016 na unatarajiwa kumalizika september 2020 kwa ufadhili wa shirika la utoaji wa huduma za kisheria (LSF)  ambapo mkutano huo umewakutanisha wasaidizi wa kisheria kutoka  halmashauri ya Meru na Wilaya ya Arusha
Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com