Waziri Mkuu Kassim Majaliwa,
akihutubia kwenye Mkutano wa Mawaziri wa Nchi za SADC wa masuala ya
Tehama, Uchukuzi, Habari na Hali ya Hewa. Septemba 19.2019. (Picha na
Ofisi ya Waziri Mkuu).
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa,
akizungumza na Mrakibu Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP), Gabriel
Mukungu, wakati akiangalia mfumo wa unaorahisisha mawasiliano kwa vyombo
vya usafiri (Traffic Information System – TIMS), kabla ya kufungua
Mkutano wa Mawaziri wa Nchi za SADC wa masuala ya Tehama, Uchukuzi,
Habari na Hali ya Hewa, uliyofanyika katika ukumbi wa Julius Nyerere
jijini Dar es salaam, Septemba 19.2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa,
akiangalia mfumo wa unaorahisisha mawasiliano kwa vyombo vya
usafiri(Traffic Information System – TIMS), kabla ya kufungua Mkutano wa
Mawaziri wa Nchi za SADC wa masuala ya Tehama, Uchukuzi, Habari na Hali
ya Hewa, uliyofanyika katika ukumbi wa Julius Nyerere jijini Dar es
salaam, Septemba 19.2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa,
akisalimiana na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania,
Injinia James Kilaba, nje ya ukumbi wa Julius Nyerere jijini Dar es
salaam, kabla ya kufungua Mkutano wa Mawaziri wa Nchi za SADC wa masuala
ya Tehama, Uchukuzi, Habari na Hali ya Hewa. Septemba 19.2019. (Picha
na Ofisi ya Waziri Mkuu).
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa,
akiangalia gari maalum la mtambo wa usimamizi wa masafa, nje ya ukumbi
wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam, kabla ya kufungua Mkutano wa
Mawaziri wa Nchi za SADC wa masuala ya Tehama, Uchukuzi, Habari na Hali
ya Hewa. Septemba 19.2019. Kulia ni Mhandisi Mwandamizi, Mamlaka ya
Mawasiliano Tanzania, Victor Kweka. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
Mwakilishi wa Katibu Mkuu SADC,
Mapalao Makuena, akizungumza kwenye Mkutano wa Mawaziri wa Nchi za SADC
wa masuala ya Tehama, Uchukuzi, Habari na Hali ya Hewa. Septemba
19.2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa,
akihutubia kwenye Mkutano wa Mawaziri wa Nchi za SADC wa masuala ya
Tehama, Uchukuzi, Habari na Hali ya Hewa. Septemba 19.2019. (Picha na
Ofisi ya Waziri Mkuu).
WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa
amesema ili kuleta maendeleo endelevu ya viwanda, kuongeza biashara na
kutengeneza ajira, nchi wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa
Afrika (SADC) zinapaswa kuwekeza katika uunganishaji na uwianishaji wa
viwango mbalimbali vya TEHAMA.
Amesema hatua hiyo itasaidia
kutatua changamoto za maendeleo ya miundombinu na muingiliano wa
mawasiliano nje ya mipaka ya nchi na kikanda. “Changamoto hizo
zinajumuisha maunganisho ya njia kuu za mawasiliano kati ya nchi jirani,
kuyafanya mawasiliano ya kikanda yabaki ndani ya kanda, maunganisho ya
kuvuka mipaka ya nchi, upangaji wa bei pamoja na uwianishaji wa
viwango.”
Waziri Mkuu ameyasema hayo leo
(Alhamisi, Septemba 19, 2019) wakati akifungua Mkutano wa Pamoja wa
Mawaziri wa SADC wa sekta ya TEHAMA, uchukuzi na hali ya hewa pamoja na
kongamano maalumu la Mawaziri, unaofanyika katika Kituo cha Kimataifa
cha Mikutano cha Julius Nyerere, jijini Dar es Salaam.
Waziri Mkuu amesema kwa kipindi
hiki, nchi wanachama zinapaswa kuhakikisha kuwa utekelezaji unalenga
katika teknolojia zinazochipukia kwenye utoaji wa huduma za posta
sambamba na kuanzisha huduma na bidhaa mpya ambazo zitakidhi mahitaji ya
sasa ya wateja na kuhamasisha biashara mtandao.
“Katika kufanikisha hili, ni
muhimu kufanya tathmini ya utekelezaji wa Mkakati wa Posta wa SADC wa
mwaka 2017-2020 ambao uliridhiwa mwezi Septemba, 2017.”
Katika hatua nyingine, Waziri
Mkuu amesema ili kufikia mtangamano wa kikanda kuhusua miundombinu ya
usafiri na usafirishaji, mkutano huo unapaswa kuzungumza namna gani nchi
wanachama zinaweza kuwianisha sera, viwango, mifumo ya sheria katika
maeneo ya barabara, reli, usafiri wa anga, usafiri wa majini, pamoja na
hali ya hewa.
Waziri Mkuu amesema kuna haja ya
kuboresha miundombinu muhimu ya usafirishaji, utaratibu wa ugavi na
usafirishaji wa vitu na huduma pamoja na kuwezesha kutoa mizigo kutoka
sehemu moja kwenda sehemu nyingine ndani ya kanda. “Hivyo, nawaomba
katika mkutano wenu mjadili maeneo haya na kuja na mapendekezo ya
suluhisho ili kutatua vikwazo mbalimbali.”
“Tanzania imeweza kuboresha
miundombinu ya bandari pamoja na mifumo ya uendeshaji ili kusaidia nchi
za SADC ambazo hazipakani na bahari nazo ni Jamhuri ya Kidemokrasia ya
Congo, Jamhuri ya Zambia, Jamhuri ya Malawi pamoja na nchi wanachama wa
Jumuiya ya Afrika Mashariki za Jamhuri za Uganda, Rwanda na Burundi.”
Waziri Mkuu amesema kuwa nchi
wanachama wa SADC zinapaswa kuboresha mifumo ya reli kwa kuzingatia
Mpango Mkakati Elekezi wa Maendeleo wa Kikanda wa mwaka 2015-2063 pamoja
na Mpango Kamambe wa Maendeleo ya Miundombinu wa Kikanda wa mwaka
2019-2023.
Amesema kati ya miradi mikubwa
inayotekelezwa hapa Tanzania, ni pamoja na ujenzi wa reli ya kisasa ya
mwendo kasi inayojengwa katika ukanda wa kati pamoja na ukarabati wa
Reli ya Tanzania na Zambia (TAZARA) ambayo inaunganisha nchi wanachama
wa SADC. “Hivyo, katika ukarabati uliofanyika wa TAZARA, umeongeza uwezo
wa reli hiyo kusafirisha mizigo kutoka tani 88,000 mwaka 2014/2015 hadi
tani 220,000 mwaka 2017/2018.”
Mkutano huo unahudhuriwa na
Mawaziri wa Sekta ya TEHAMA, Habari, Uchukuzi na Hali ya Hewa kutoka
nchi za Angola (4), Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo (2), Msumbiji (1)
Zambia (3), Afrika Kusini (2), Lethoto (1), Zimbabwe (2) na Tanzania
inawakilishwa na Mawaziri watano na Naibu Waziri Mmoja, akiwemo Waziri
wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Isack Kamwelwe ambaye ndiye
Mwenyekiti wa Mkutano huo.
0 comments:
Post a Comment