Msajili wa Mashirika Yasiyo ya
Kiserikali Bi. Vickness Mayao akizungumza na vyombo vya habari leo
Jijini Dodoma kwa ajili ya kutoa mwelekeo wa zoezi la uhuishaji
Mashirika amabayo awali yalijisajili chini ya Sheria nyingine.
Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini WAMJW
…………….
Na Mwandishi Wetu Dodoma.
Wizara ya Afya Idara Kuu Maendeleo
ya Jamii imetoa muda zaidi wa zoezi la usajili na uhuhishaji wa
Mashirika Yasiyo ya Kiserikali ambayo awali yalijisajili kwa Sheria ya
Makampuni, Bodi ya Wadhamini na sheria ya Jumuiya za Kiraia chini ya
Wizara ya Mambo ya Ndani ambazo kwa sababu tofouti hazijakamilisha zoezi
la uhuishaji kwa mujibu wa Sheria no. 3 ya mwaka 2019.
Akizungumza na vyombo vya habari
leo jijini Dodoma Msajili wa NGOs Nchini Bi. Vickness Mayao amesema
kimsingi kazi hii inahusu yale mashirika ambayo hayajakamilisha zoezi la
kuhuisha vyeti vyao kwa mujibu wa Sheria na Wizara imeona ni vyema
kuendelea na zoezi hilo baada ya kuwa imefanya hivyo katika Kanda tano
hapa nchini.
“Tunaendelea na zoezi la usajili
huu ambao kisheria unakamilika tarehe 30 Augusti 2019 kama Sheria no.3
ya mwaka 2019 inavyoelekeza ili kutoa nafasi zaidi kwa Mashirika
yaliyosalia ambayo kwa namna moja au nyingine bado hayajakamilisha
usajili wake na ifikapo mwisho wa mwezi huu kila Shirika litabaki katika
Sheria yake”. Aliongeza Bi. Mayao.
Aidha Bi. Mayao amesema kuwa Ofisi
ya Msajili wa NGOs tayari imetoa orodha ya awali ya Mashirika ambayo
yameondolewa kwenye Daftari la Msajili wa Mashirika Yasiyo kuwa ya
Kiserikali ambayo pia yanatakiwa kuhamia katika Sheria nyingine
akiongeza kuwa orodha hiyo tayari imewekwa kwenye tovuti ya Msajili wa
NGOs.
Bi. Mayao ametaja idadi ya
Mashirika hayo kuwa ni 158 na inatarajia kuongezeka kadili zoezi la
kuyatambua Mashirika hayo linavyoendelea na kusisitiza kuwa orodha
iliyopo ni ya wali na kuyataka Mashirika hayo kufanya haraka kuhuisha
usajili wao kama Sheria mpya inavyosema kwani kushindwa kufanya hivyo
maana yake shirika husika litakuwa limefutwa.
Msajili wa NGOs ameongeza kuwa
zoezi la uhuishaji limefanikiwa kwa asilimia 85 baada ya kuwa
limefanyika katika kanda tano ikiwemo Kanda ya Ziwa, Kanda ya Kati ,
Kanda ya Kaskazini, Pwani na Nyanda za Juu Kusini na sasa zoezi hili
linaendelea mjini Dodoma kwa ajili ya Mashirika ambayo bado yamesalia na
zoezi hili linaendelea kwa kushirikiana na wale wanaosimamia Sheria
nyingine.
Zoezi la uhuishaji Mashirika
linafanyika kwa miezi miwili kwa mujibu wa Sheria no.3 ya mwaka 2019 na
tayari limekamilika katika Kanda tano lakini linaendelea kukamilika
Jjini Dodoma ili kutoa fursa ya ziada kwa Mashirika ambayo bado
hajakamilisha zoezi la uhuishaji usajili kwake kabla ya kuondolewa
usajili kama takwa la kisheria lilivyo katika Sheria hiyo.
0 comments:
Post a Comment