………………………..
Na Munir Shemweta, WANNM ARUSHA
Mkuu
wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo amewataka wajumbe wanaoshiriki kikao cha
Uimarishaji mpaka wa kimataifa kati ya Tanzania na Kenya kutumia kikao
hicho kutafuta ufumbuzi wa kudumu wa changamoto za mipaka badala ya
kushindana.
Mrisho
Gambo alitoa kauli hiyo leo tarehe 19 Agosti 2019 wakati wa kufungua
kikao cha cha muendelezo wa Uimarishaji mipaka ya kimataifa baina ya
Tanzania na Kenya kinachoendelea jijini Arusha.
Alisema,
anafarijika sana kuona utatuzi wa changamoto za mipaka ya kimataifa
kati ya Kenya na Tanzania unafanywa na nchi husika bila kushirikisha
mataifa ya nje na kusema kuwa hiyo inaonesha ni jinsi gani nchi hizo
zinavyoweza kukaa pamoja kwa kujiamini na kupata ufumbuzi wa masuala yake.
Aliwataka
wajumbe wa kikao cha nchi hizo mbili kutafuta ufumbuzi wa changamoto za
mipaka ya kimataifa kati yao kwa kukubaliana na kuzingatia tamaduni za nchi hizo sambamba na miongozo ya viongozi wa nchi husika.
Aidha,
Mkuu huyo wa mkoa wa Arusha aliwataka washiriki kudumisha pia mahusiano
ya kijamii wakati wa majadiliano yao kwa kuwa wananchi wanaoishi mipakani wana mahusiano mazuri ya kindugu na kusisitiza kuwa hali hiyo itadumisha umoja na mshikamano uliopo kati ya nchi hizo.
Naibu
Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mathias
Kabundugulu alisema kikao hicho cha siku tano ni muendelezo wa vikao vya
uimarishaji mipaka ya kimataifa katika maeneo mbalimbali ya mipakani
ikiwa na lengo la kuondoa changamoto kama ilivyoelekezwa na Umoja wa
Afrika (AU).
Kwa
mujibu wa Kabundugulu, Kikao hicho kitapokea taarifa ya ukaguzi wa
kipande cha mpaka cha kilomita 128 kutoka eneo la Ziwa Natron hadi
Namanga mkoani Arusha ambapo lengo ni kuimarisha mpaka huo hadi Tarakea
mkoani Kilimanjaro na baadaye Jasini mkoani Tanga.
Kwa
upande wake Mkuu wa Ujumbe kutoka Kenya Justa Nkoroi alisema kikao hicho
ni muhimu kwa mustakabali wa nchi za Tanzania na Kenya katika kuangalia
changamoto za alama za mipaka ya kimataifa iliyowekwa wakati wa ukoloni
na kubainisha kuwa ana imani kikao hicho kutatatua changamoto zilizopo na hatimaye kukamilisha kazi hiyo ndani ya muda uliopangwa na Umoja wa Afrika mwaka 2022.
Tayari
jumla ya Kilomita 172 kutoka ziwa Victoria hadi Loliondo mkoani Arusha
zimeimarishwa kwa kuwekwa alama (Pillars) za mipaka kati ya Tanzania na
Kenya kwa umbali wa mita zisizozidi mita 100 ili zionekanane kwa urahisi
na wananchi wanaoendesha shughuli zao katika maeneo ya mipakani.
0 comments:
Post a Comment