METDO Tanzania

METDO Tanzania

Wednesday, August 14, 2019

WAZIRI MKUU KUWA MGENI RASMI SIKU YA KIMATAIFA YA VIJANA

Meneja Program ya vijana na Maendeleo kutoka UNFPA- Tanzania Dkt.Majaliwa Marwa,akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati akitoa taarifa ya maadhimisho ya miaka 20 ya siku ya kimataifa ya vijana kwa mwaka 2019 ambapo mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa yatakayofanyika jijini Dodoma.
Afisa habari na uhusiano wa shirika la kazi Duniani kwa Dar es Salaam Bw.Magnus Minja,akizungumza na waandishi wa habari kuelekea siku ya maadhimisho ya miaka 20 ya siku ya kimataifa ya vijana kwa mwaka 2019 yatakayofanyika jijini Dodoma.
Afisa habari Umoja wa Mataifa kwa Tanzania (UN) Bi. Stella Vuzo ,akitoa taarifa kwa waandishi wa habari kuhusu siku ya maadhimisho ya miaka 20 ya siku ya kimataifa ya vijana kwa mwaka 2019 yatakayofanyika jijini Dodom
Afisa mawasiliano UN kwa Tanzania kushoto ,Warren Bright ,akiongea jambo kwa waandishi wa (habari hawapo pichani) katika katika maadhimisho ya miaka ishirini (20)ya siku ya kimataifa ya vijana kwa mwaka 2019 ambayo yatafanyika Jijini  Dodoma.
……………..
Na.Alex Sonna,Dodoma
WAZIRI Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa, anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika maadhimisho ya miaka ishirini (20)ya siku ya kimataifa ya vijana kwa mwaka 2019 ambayo yatafanyika Jijini  Dodoma.
Akitoa taarifa kwa wanahabari  Meneja program ya vijana na maendeleo kutoka UNFPA- Tanzania Dkt Majaliwa Marwa, amesema katika maadhimisho yanayowezeshwa na UNFPA, UNESCO, ILO na UNIC yanalengo la kuhakikisha vijana wanajengewa uwezo na kuwa na ubunifu mbalimbali.
Amesema maadhimisho hayo yatashirikisha vijana zaidi ya mia tano(500) kutoka Tanzania bara na visiwani na kwa mwaka huu wamejikita zaidi katika kutilia mkazo kuhusu elimu kwa vijana.
“Mwaka huu ni maadhimisho ya ishirini ya siku ya vijana kimataifa na mwaka huu tumejikita katika elimu ili kuwajengea vijana uwezo na kuwa wabunifu kuweza kujitegemea, dhamira Tanzania  iliyopendekezwa kuelekea 2030 Tanzania ya viwanda boresha elimu kwa ajiri ya maendeleo ya vijana” amesema.
Aidha amebainisha baadhi ya shughuri ambao zitafanyika jijini Dodoma ikiwa ni katika kudhimisha siku hiyo katika maeneo mbalimbali Jijini Dodoma.
“Tarehe 15 tutakuwa na kongamano litakuwa na maada mabalimbali likihusisha ubunifu na afya ya uzazi kwa vijana, na siku ya pili kutakuwa na tamasha litakuwa katika eneo la Chang’ombe eneo  lenye mkusanyiko wa vijana wengi na kutakuwa na burudani nyingi” amesema. 
Kwa upande wake mwenyekiti wa Shirika la RESLESS DEVELOPMENT, chini ya mradi  wa Kijana wajibika  kwa mkoa wa Dodoma, Ridhiwani Juma, amesema wao kama wenyeji wameweza kuratibu na kuhakikisha hata vijana wenye mahitaji maalumu nao wanakuwa sehemu ya mmaadhimisho hayo.
Muwakilishi wa vijana ambaye ni katibu Afriyan Tanzania, Seif Ibrahimu amesema kundi la vijana linakabiliwa na tatizo la ukosefu wa ajira kwa kiasi kikubwa.
Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com