Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri
Mkuu anayeshughulikia Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu
Mhe. Jenista Mhagama akipokea taarifa kutoka kwa Msimamizi wa Ujenzi wa
Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF), Bw. Suleiman Salmin kuhusu
miradi ya ujenzi inayotekelezwa na mfuko huo wakati wa ziara yake ya
kukagua miradi hiyo.
Msimamizi wa Ujenzi wa Mfuko wa
Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF), Bw. Suleiman Salmin (kushoto)
akielezea jambo kuhusu hatua iliyofikiwa katika ujenzi wa jengo la
hoteli ya nyota tano (5) inayojengwa na Mfuko huo, Jijini Mwanza.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri
Mkuu anayeshughulikia Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu
Mhe. Jenista Mhagama akitoa maelezo kwa watendaji wa Mfuko wa Taifa wa
Hifadhi ya Jamii (NSSF) alipotembelea kwa lengo la kukagua na kujionea
hatua za awali zilizofikiwa katika utekelezaji wa miradi hiyo.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri
Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista
Mhagama akitazama jengo mmoja wapo linalojengwa na Mfuko wa Taifa wa
Hifadhi ya Jamii (NSSF) wakati ziara yake ya kukagua na kujionea hatua
zilizofikiwa katika utekelezaji wa miradi hiyo.
PICHA ZOTE NA OFISI YA WAZIRI MKUU
(KAZI, VIJANA, AJIRA NA WENYE ULEMAVU)
……………….
Na; Mwandishi Wetu
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri
Mkuu anayeshughulikia Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu
Mhe. Jenista Mhagama ameagiza watendaji wa Mifuko ya hifadhi ya Jamii
yaani Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) na Mfuko
wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) kuwa wabunifu katika kuwekeza kwenye
vitega uchumi vyenye kuleta tija na inayochochea maendeleo ya Taifa.
Kauli hiyo ameitoa wakati wa ziara
yake Jijini Mwanza alipokuwa akikagua Miradi mbalimbali inayotekelezwa
na Mifuko hiyo ya Hifadhi ya Jamii ili kujionea hatua zilizofikiwa
katika utekelezaji.
Alieleza kuwa kuwekeza katika
miradi yenye tija ni jambo muhimu kwa kuwa miradi hiyo italeta maendeleo
endelevu yatakayochangia katika ukuaji wa pato la taifa na ustawi wa
mkoa huo.
“Mwanza ni miongoni mwa Mikoa
yenye fursa nyingi za kibiashara kutokana na sehemu kubwa ya mkoa huo
kuzungukwa na ziwa viktoria, hivyo kurahisisha ukanda huo kufikiwa kwa
urahisi na soko la Afrika Mashariki,” alisema Mhagama.
Alifafanua kuwa ubunifu katika
kutekeleza shughuli za mifuko ni pamoja na kutafuta masoko ya vitenga
uchumi ya miradi hiyo kwa kuangalia fursa zilizopo kwenye kanda ya ziwa.
Aliongeza kuwa fursa ni pamoja na
ujenzi wa daraja la Busisi litakalopita ziwa viktoria, Mbuga ya Wanyama
ya Burigi pamoja na shughuli za uchimbaji madini zilizopo katika mkoa
huo.
Katika Ziara hiyo Waziri Mhagama
aliweza kutembelea linapojengwa Soko la Madini katika Jengo la
Kibiashara la Rock City Mall. Pia alitembelea jengo la PSSSF Mwanza na
alipata fursa ya kukagua shughuli za uwekezaji katika jengo hilo
zinazoendeshwa na wawekezaji wazawa katika Hoteli ya Gold Crest.
0 comments:
Post a Comment