*Azitaka halmashauri nchini kuondoa urasimu, vikwazo kwa wawekezaji
WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwaamezindua
Mwongozo wa Uwekezaji wa Mkoa wa Kagera wenye lengo la kutangaza fursa
za Uwekezaji na hivyo, kukuza maendeleo ya mkoa huona ameziagiza
halmashashauri zote za wilaya nchini ziondoe urasimu na kupunguza
vikwazo kwa wawekezaji.
Waziri Mkuu ameyasema hayo leo
(Jumatano, Agosti 14, 2019) wakati akizindua Kongamano la Wiki ya Kagera
na Mwongozo wa Uwekezaji mkoani Kagera, lilifanyika Bukoba
mjini.Amewataka Watanzania wahakikishe wanachangamkia fursa za biashara
zilizopo.
Amesema Watanzania wanao uwezo wa
kutumia fursa za uwekezaji na biashara zilizopo nchini kwa kushirikiana
na taasisi za kifedha na kuwekeza katika miradi mbalimbali nchini,
badala ya kuachia fursa hizo kuchukuliwa na wageni.
Amesema azma ya Serikali ya Awamu ya
Tano inayoongozwa na Rais Dkt. John Magufuli ya kukuza uchumi kupitia
sekta ya na kufikia wa kati ifikapo mwaka 2025 itaendelea
kutekelezwa, hivyo, ametumia fursa hiyo kuwakaribisha wawekezaji wa nje
nao waje kuwekeza.
“Serikali itaendelea kusimamia
utekelezaji wa Sera ya Maendeleo Endelevu ya Viwanda Awamu ya Tatu
(2010/2020) na Mpango wa Pili wa Maendeleo wa Miaka Mitano (2015/2016
2020/2021) ambao lengo lake ni kuendeleza uchumi wa viwanda”.
Akizungumzia kuhusu maadhimisho ya
Wiki ya Uwekezaji Kagera, Waziri Mkuu amesema yamelenga kuwakutanisha
wadau wa uwekezaji, ambao ni pamoja na Wafanyabiashara kutoka ndani ya
mkoa na nchi jirani zinazozunguka Mkoa wa Kagera.
“Ni ukweli usiofichika kwamba tunahitaji
wawekezaji watakaosaidia uchumi wa mkoa huu kukua kwa kasi kupitia fursa
zilizopo kwenye nyanja za kilimo, mifugo, uvuvi, viwanda, maliasili na
utalii”.
Waziri Mkuu amesema ukuaji mzuri wa
uchumi wa mkoa utakuwa na manufaa katika kuongezeka kwa pato la
mwananchi wa Kagera, pato la mkoa na hata pato la Taifa nalo litakuwa
kwa kasi ndani ya kipindi cha muda mfupi.
Amesema mkoa wa Kagera ndiyo
unaoongoza kwa uzalishaji wa kahawa nchini, ambapo zaidi ya nusu ya
kahawa yote huzalishwa katika mkoa huo. Wastani wa uzalishaji wa kahawa
kwa mwaka ni kati ya tani 50,000 hadi tani 65,000 kutegemea na hali ya
hewa ya mwaka husika.
Hivyo, mkoa huo una fursa kubwa ya
uwekezaji kwenye viwanda vya kukoboa na kusindika kahawa.Pia mkoa wa
Kagera ni miongoni mwa mikoa michache Tanzania yenye fursa nyingi za
uwekezaji ambazo kwa namna moja au nyingine hazipatikani katika mikoa
mingine ya nchini. Miongoni mwa fursa hizo ni pamoja na soko kwani
unapakana nan chi nne za Afrika Mashariki.
“Kagera imepakana na Uganda, Rwanda,
Burundi na Kenya. Kupakana na nchi hizo zenye idadi kubwa ya watu katika
ukanda huu wanaokadiriwa kufikia takriban milioni 190 ambapo kwa mujibu
wa takwimu za mwaka 2018 ni fursa ya uwepo wa soko kubwa la bidhaa
zinazozalishwa au zinazoweza kuzalishwa katika mkoa wa Kagera”.
Kadhalika, Waziri Mkuu amesema
Serikali imeendelea kuboresha miundombinu mbalimbali ya usafiri ukiwemo
wa anga na wa barabara ili kurahisisha usafiri kutoka Bukoba makao makuu
ya mkoa wa Kagera kufika katika nchi hizo.
“Kwa mfano, umbali kutoka Bukoba hadi
Kampala ni km. 340, Bujumbura km. 550 na Kigali km. 490. Kadhalika,
itakuwa ni rahisi kufikia masoko ya nchi za Sudan Kusini pamoja na
Jamhuri ya Kidemokrasia ya Watu wa Kongo (DRC)”.
Awali, Mkuu wa Mkoa wa Kagera,
Brigedia Jenerali Marco Gaguti alisema dhamira ya kuandaliwa kwa wiki ya
uwekezaji mkoani Kagera ina lengo la kuhakikisha kwamba mkoa huo
unafanya vizuri katika sekta ya uwezekezaji na biashara, hivyo kuchangia
katika ukuaji wa pato la Taifa.
Alisema mkoa wa Kagera ni miongoni mwa
mikoa 10 ambayo inamchango mdogo katika pato la Taifa, hivyo wanataka
watoke kwenye kuchangia asilimia 3.9 hadi wafikie asilimia 10.
Kwa upande wao, viongozi mbalimbali
wakiwemo Magavana kutoka na wafanyabiashara kutoka nchi za Rwanda na
Burundi waliahidi kutumia fursa zilizopo nchini, pamoja na kuwakaribisha
wafanyabiashara na wawekezaji wa Tanzania kwenda kuwekeza katika nchi
zao.
0 comments:
Post a Comment