Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimina na Mkurugenzi
Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshuhulikia Wanawake
Duniani(UN WOMAN) Bibi. Hodan Addou wakati Bibi Addou alipofika Ofisini
kwa Makamu wa Rais Ikulu Jijini Dar Es Salaam leo Agost 14,2019 kwa
ajili ya kumshukuru Makamu wa Rais kwa kuweza kuimarisha Ulizi wa Masoko
kwa kuzuwia Utumikishaji wa Wanawake na watoto Masokoni ambapo pia
amesema Shirika hilo kwa kushirikiana na Benki ya Dunia wameandaa Warsha
itakayozungumzia kuhusu Wanawake kuweza kutambua hali zao kwenye suala
zima la Biashara.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Mkurugenzi
Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshuhulikia Wanawake Duniani
(UN WOMAN) Bibi. Hodan Addou wakati Bibi Addou alipofika Ofisini kwa
Makamu wa Rais Ikulu Jijini Dar Es Salaam leo Agost 14,2019 kwa ajili ya
kumshukuru Makamu wa Rais kwa kuweza kuimarisha Ulizi wa Masoko kwa
kuzuwia Utumikishaji wa Wanawake na watoto Masokoni ambapo pia amesema
Shirika hilo kwa kushirikiana na Benki ya Dunia wameandaa Warsha
itakayozungumzia kuhusu Wanawake kuweza kutambua hali zao kwenye suala
zima la Biashara. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
………………..
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, amelitaka Shirika la
Umoja wa Mataifa linaloshuhulikia Wanawake Duniani (UN WOMAN) kuandaa
Tathmini ya kinchi kuhusiana na Kongamano la Beijing.
Amesema ni Vyema kuwepo na
uwezekano wa kuweza kuandaa Tathmini ya uhakika itakayoweza kuonesha
hali halisi ya Idadi ya Wanawake waliopo katika Nafasi mbalimbali za
Kiuongozi hususan kwenye Baadhi ya Mashirika na Taasisi Binafsi.
Makamu wa Rais ameyasema hayo leo
Agost 14, 2019 Ofisini kwake Ikulu Jijini Dar Es Salaam wakati
alipokutana na kuzungumza na Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Umoja wa
Mataifa linaloshuhulikia Wanawake Duniani (UN WOMAN) Bibi Hodan Addou.
Aidha Makamu wa Rais amelishukuru
Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshuhulikia Wanawake Duniani (UN
WOMAN) kwa kuendelea kuweza kutoa fursa katika nyanja mbalimbali za
Kijamii na kimaendeleo kwa Wanawake Duniani na kulitaka Shirika hilo
kuendelea kuzidi kutoa fursa hizo kwa Wanawake Hususan kwenye sekta za
Kilimo.
Nae Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la
Umoja wa Mataifa linaloshuhulikia Wanawake Duniani Bibi Hodan Addou
aliyeambatana na Bw. Denis Maro Biseko Mwakilishi wa Benki ya Dunia hapa
Nchini, amemshukuru Mhe. Makamu wa Rais kwa kuweza kuimarisha Ulizi wa
Masoko kwa kuzuwia Utumikishaji wa Wanawake na watoto Masokoni. Ambapo
pia amesema Shirika hilo kwa kushirikiana na Benki ya Dunia wameandaa
Warsha itakayozungumzia kuhusu Wanawake kuweza kutambua hali zao kwenye
suala zima la Biashara.
0 comments:
Post a Comment