WAZIRI wa Nchi,Ofisi ya
Rais,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe.Seleman Jafo,akizungumza
katika maadhimisho ya siku ya vijana Duniani yaliyofanyika jijini Dodoma
leo ambapo amewataka vijana hao kutunza amani ya nchini.
Mwakilishi Mkazi wa Shirika la
Umoja wa Mataifa la Idadi ya Watu Duniani (UNFPA) Jacqueline
Mahon,akitoa taarifa katika maadhimisho ya siku ya vijana Duniani
yaliyofanyika jijini Dodoma
Naibu Katibu Mkuu,Wizara ya
Vijana,Sanaa,Utamaduni na Michezo,Zanzibar,Amour Hamil
Bakari,akizungumza na washiriki katika maadhimisho ya siku ya vijana
Duniani yaliyofanyika jijini Dodoma.
Msanii wa bongofleva Kala
Jeremiah,akitoa burudani pamoja na washiriki katika maadhimisho ya siku
ya vijana Duniani yaliyofanyika jijini Dodoma.
Sehemu ya washiriki wa maadhimisho ya siku ya vijana Duniani yaliyofanyika jijini Dodoma.
WAZIRI wa Nchi,Ofisi ya
Rais,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa,Seleman Jafo akiwa katika
picha ya pamoja na baadhi ya vijana katika maadhimisho ya siku ya vijana
Duniani yaliyofanyika jijini Dodoma
.WAZIRI wa Nchi,Ofisi ya
Rais,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa,Seleman Jafo akiwa katika
picha ya pamoja na viongozi katika maadhimisho ya siku ya vijana Duniani
yaliyofanyika jijini Dodoma.
………………..
Na.Alex Sonna,Dodoma
WAZIRI wa Nchi,Ofisi ya
Rais,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa,Mhe.Seleman Jafo amewataka
vijana kutochezea amani ya Nchi na Badala yake wawe Mabalozi Wazuri wa
kutunza na kuenzi amani hiyo kwani ni Tunu kwa Taifa la Tanzania.
Waziri Jafo amesema hayo leo
jijini Dodoma katika maadhimisho ya siku ya vijana duniani ambapo
amesema amani iliyoasisiwa na Marais wa Tanganyika na Zanzibar ni vigumu
kuirejesha ikipotea hivyo vijana ni nguzo Muhimu wa Kuitunza amani
hiyo.
“Waasisi wa Taifa letu ,Julius
Kambarage Nyerere na Aman Karume walipambana sana na walitumia gharama
kubwa kuhakikisha amani ya nchi yetu inapatikana na tukajipatia Uhuru
,kilichobaki ni kirahisi sana ni kuiendeleza ,kuienzi na kuitunza amani
ya Nchi Yetu kwani ikipotea kuirudisha ni vigumu sana ,na wenye wajibu
na nguvu kubwa wa kuinza ni ninyi vijana “amesema Jafo.
Katika hatua nyingine Waziri Jafo
amewataka vijana waliopewa nafasi za Madaraka kufanya kazi na kuacha
maigizo ili waache historia ya Taifa la Tanzania.
Waziri Jafo amesema ni vyema kwa vijana waliopewa dhamana ya kuliongoza taifa kuwajibika vyema kuwahudumia Wananchi .
Pia amewataka kuchangamkia fursa
ya mikopo ambayo imekuwa ikitolewa na Halmashauri ambapo amedai kwa sasa
kina mama ndio wamekuwa wakichangamkia fursa hiyo.
“Igeni mfano wangu mimi
simwangushi Rais,bajeti ya nchi zaidi ya asilimia 20 inatoka
kwangu,vijana mkipewa nafasi fanyeni kazi.Usikubali ukiwa kama kijana
lazima uache alama ili wakukumbuke,kijana sio sifa kukaa kiti kirefu
halafu unasema kunyweni mpaka mikono idondoke, acha alama wekeni mifano
kwa watu wengine,”amesema .
“Vijana acheni maigizo fanyeni
kazi ya kuwasaidia Watanzania fanya kazi kwa ajili ya kuwahudumia
watu,fanya kazi yako itangazike,tukifanya maigizo hatuwezi kulisaidia
Taifa letu.Niwaombe vijana wenzangu tupambane,”amesema.
Jafo amesema vijana ambao wamepewa fursa wasivunje matumaini ya vijana wenzao.
Amewataka vijana kuchangamkia
fursa ya mikopo inayotolewa katika Halmashauri mbalimbali nchini huku
akidai kwamba wanawake wamekuwa wakijitokeza kwa wingi.
“Bado ni changamoto,lazima
tuangalie namna ya kurejesha mikopo wengi wanaorejesha ni kina
mama,vijana wanaokopa kurejesha ni shida,”alisema Jafo.
Jafo amewataka vijana kulima
kilimo cha kisasa kwani kimekuwa na faida kubwa ambapo alidai ekari moja
ikipandwa vizuri inaweza kutoa mazao mengi.
“Ukiamua kufuga kuku wa mayai
10,000 ambao kila siku wanatoa trei 300 kwa shilingi 7000 ina maana kila
siku wana uwezo wa kupata milioni moja.Vijana naomba niwaambie
badilishaneni mawazo,wekezeni katika ujasiriamali,”alisema.
Aidha,Jafo aliwataka vijana ambao
watajadiliana katika kikao hicho kufanya tathmini ya yale
watakayokubaliana nayo na kisha wanayapeleke Serikalini.
“Tumepata fursa ya kukutana bahati
nzuri kutoka katika mikoa yote nawaomba mfanye tathmini ya mambo yote
na yale mtakayokubaliana yaleteni Serikalilini na tutayafanyia kazi.
“Zamani kulikuwa na kauli mbiu
vijana ni taifa la kesho kauli hiyo tumeitoa na kwa sasa vijana ni taifa
la leo,vijana sasa mnaweza kupewa fursa na mkapewa nafasi mkazitendea
haki.
Jafo amesema wana kila sababu ya kujadiliana kuhusu elimu kwani imekuwa ni daraja la kuweza kufikia mafanikio.
“Kumbukeni tuna kila sabbau ya
kujadili ajenga ya elimu, tuna kila sababu ya kuboresha elimu yetu bila
elimu vijana wa sasa hatuwezi kupasua tuna kila sababu ya kuitafakari
elimu yetu.Niwaombe sana lazima vijana wa kitanzania tujikite katika
elimu.
Aidha,Jafo amewataka vijana kujitambua kwa kuhakikisha wanakuwa na uzalendo wa kununua bidhaa zinazozalishwa na vijana.
“Tuna agenda kubwa tupambane na
adui wa roho mbaya kuna vijana wengine wana roho mbaya wapo kuwakwamisha
kwanza tupendane,bidhaa hizo zote kama tutanunua tutaenda mbali kwani
vijana ni timu kubwa,”amesema.
Kwa Upande wake,Naibu Katibu
Mkuu,Wizara ya Vijana,Sanaa,Utamaduni na Michezo,Zanzibar,Amour Hamil
Bakari,amesema Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali
ya Mapinduzi Zanzibar zitaendelea kuchukua juhudi kuhakikisha vijana
wanapata kazi pamoja na kufanya kazi zenye staha.
“Serikali zinaendelea kuchukua
juhudi kuhakikisha vijana wetu wanapata kazi zenye staha pamoja na
changamoto ya ajira.Niwakumbushe vijana kuendelea kulinda amani iliyopo,
suala la kudumisha muungano wetu hili halina mjadala na sisi
tutaendelea kuwakumbusha vijana kuhakikisha wanalinda muungano kwa nguvu
zote,”amesema.
Naye,Mwakilishi Mkazi wa Shirika
la Umoja wa Mataifa la Idadi ya Watu Duniani (UNFPA)Jacqueline Mahon
amesema vijana wanatakiwa kusaidiwa kwenye mambo mbalimbali.
Pia amesema elimu ni Msingi wa
Maendeleo endelevu kwa vijana ndio maana maadhimisho ya vijana duniani
mwaka 2019 imelenga zaidi kuimarisha elimu kwa vijana na UNFPA imekuwa
ikijikita zaidi kutatua changamoto mbalimbali za vijana ikiwa ni pamoja
na changamoto ya elimu na Ajira Kwa Vijana.
Hivyo Madam Mahon amesema UNFPA
ina mkakati Kabambe wa kuwawezesha vijana kwa kushirikiana na Mashirika
mbalimbali ya Tanzania na ya Kimataifa huku akizungumzia mkutano Mkubwa
wa Vijana utakaofanyika jijini Nairobi nchini Kenya na kuwaasa vijana
kujitokeza kwa wingi kwani vijana ni chachu muhimu kwa Maendeleo ya
nchi.
Akitoa neno la Shukrani kwa niaba
ya vijana,Maadam Sophia Mbeyela ameshukuru serikali pamoja na asasi za
kiraia kwa kujali vijana wa rika zote na aina zote wakiwemo wenye
ulemavu na kusema kuwa wao kama vijana wenye ulemavu hawaachwi nyuma
kwani ulemavu si ugonjwa.
Awali Afisa Maendeleo ya Jamii
,Idara kuu ya vijana jiji la Dodoma Mfungo Daniel Manyama ambaye
alikuwa mwakilishi wa Afisa vijana Mkoa wa Dodoma , amewaasa vijana
kuchangamkia Fursa ya Zao la Zabibu pia kuunga mkono vijana
wenzao kununua zao hilo ili kuinua
uchumi wa vijana huku Mkuu wa Chuo Mipango na Maendeleo ya Vijijini
,Prof.Hozen Mayaya akiwataka vijana kuwa na Fikra pevu.
Siku ya Umoja wa Mataifa ya Vijana
imeratibiwa na Shirika la Umoja wa Mataifa Tanzania UN na kuongozwa na
Shirika la Umoja wa Mataifa la Idadi ya Watu UNFPA ,kwa kushirikiana na
Mashirika ya Umoja wa Mataifa Tanzania UNICEF,UNESCO,UNIC na ILO pamoja
na Serikali ya Jamhuri wa Muungano wa Tanzania mkoa wa Dodoma na Asasi
zisizo za Kiserikali.
0 comments:
Post a Comment