Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akihtubia mbele ya mgeni
wake Rais wa Jamhuriya Afrika Kusini Cyril Ramaphosa katika mkutano
baina ya Wafanyabiashara wa Tanzania na Ujumbe wa Wafanyabiashara toka
Afrika kusini uliofanyika katika kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha
Julius Nyerere (JNICC) Jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuriya Afrika Kusini
Cyril Ramaphosa katika mkutano baina ya Wafanyabiashara wa Tanzania na
Ujumbe wa Wafanyabiashara toka Afrika kusini uliofanyika katika kituo
cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC) Jijini Dar es
Salaam huku mwenyeji wake Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akimsikiliza.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya
pamoja na mgeni wake Rais wa Jamhuri ya Afrika Kusini Cyril Ramaphosa na
Mawaziri wa Serikali ya Tanzania na Afrika kusini mara baada ya
kumalizika kwa mkutano baina yaWafanyabiashara wa Tanzania na Ujumbe wa
Wafanyabiashara toka Afrika kusini uliofanyika katika kituo cha
Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC) Jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na mgeni wake Rais wa
Jamhuri ya Afrika Kusini Cyril Ramaphosa wakisalimiana mwenyekiti wa
Kigoda cha Mwalimu Nyerere Mzee Joseph Butiku mara baada ya kumalizika
kwa mkutano baina ya Wafanyabiasharawahao.
………………………………………………………..
Rais Magufuli, amesema hakuna
uchaguzi mwingine katika kuhakikisha Afrika inaondokana na unyonge zaidi
ya kuungana katika mapambano ya kiuchumi.
Rais Magufuli amesema “Udugu na
muungano wetu utakuwa hauna maana ikiwa tutashindwa kufikia lengo hili
la kukua kiuchumi. Tuendelee kuwa pamoja kwa sababau historia yetu
inafanana,” .
Rais Dk. John Magufuli amesema
hayo akiwa na mgeni wake Rais Cyril Ramaphosa wakati wa jukwa la
baishara kati ya wafanyabiashara kutoka nchi za Afrika Kusini na
Tanzania katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere
(JNICC), jijini Dar es Salaam leo ambapo amesisitiza kuwa hakuna
kinacheweza kuzuia Afrika kuwa na maendeleo.
Rais Magufuli alisema, zaidia ya
asilimia 70 ya uzalishaji katika nchi za Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa
Afrika (SADC) bidhaa zinakwenda Afrika Kusini. Alisisitiza, bidhaa
nyingi zinakwenda Afrika Kusini ikiwemo mbogamboga na matunda, nafaka,
vinywaji, mpira na huduma za usafiri.
Rais Magufuli amebainisha kuwa ,
Afrika Kusini ni nchi ya pili kwa uwekezaji nchini ambapo kwa mwaka jana
2018 mauzo katika biashara baina ya Tanzania na Afrika Kusini
yameongezeka kwa zaidi ya asilimia 5.3,” alisema.
“Sekta ya viwanda inazidi
kuongeza urafiki huu, hata hivyo uzalisihaji wetu katika taifa la
Tanzania bado uko chini. Kama taifa tunaamini tunahuisha uwekezaji wa
viwanda ambavyo vinaongeza thamani katika bidhaa zetu ambazo
zinasafirishwa zikiwa ghafi na kupunguza bidhaa kutoka Ulaya,”
ameongeza:
“Afrika Kusini ni ya 13 kwa
uwekezaji nchini, takwimu zinaonyesha uhusiano wetu katika uchumi ni
mkubwa, maendeleo haya yanaonyesha urafiki wetu wa kibiashara, kiuchumi,
kijamii na kisiasa unaimarisha uwekezaji huu.
“Tanzania ni ya pili kwa idadi ya
mifugo baada ya Ethiopia barani Afrika, tunahitaji kutumia vema fursa
hii kuchakata mazao ya mifugo, vilevile kutumia bidhaa zitokanazo na
samaki kutoka kwenye bahari, mito na mabwawa. Lengo la msingi ni kuwa na
bidhaa zetu na kuacha kusafirisha bidhaa ghafi ambapo pia tutakuwa
tunasafirisha ajira.”
Hivyo, amemuasa Rais Ramaphosa kutumia fursa hiyo kuleta wawekezaji katika viwanda vya dawa na vifaa tiba.
“Niwakumbushe kitu kimoja tu,
katika sekta ya utalii ni eneo zuri kwa uwekezaji nchini, Tanzania ni ya
pili kwa ukubwa katika utalii duniani. Tunazidi kuongeza mbuga za
taifa, tunawekeza katika hoteli, kambi za kupumzika na utalii wa
kihistoria. Nawaomba mkipata muda mtembelee vivutio vyetu si kwa
kujifurahisha tu lakini pia kuangalia maeneo mapya ya uwekezaji,”
alisema.
Rais Magufuli amekuwa mkali kwa
watu wanaosambaza uongo kuwa Tanzania si sehemu salama kwa wawekezaji.
Amesema huo ni uongo unapasa kupuuzwa kwani Tanzania inasifika kwa amani
na utulivu wa kisiasa.
Rais Ramaphosa amesema
“Mlitufunza, mlituunga mkono kwa njia nyingi na kutusaidia kiasi
kikubwa, tunashukuru kwa dhati. Hii ndio sababu muunganiko wetu si wa
kihistoria tu bali wa damu. Kujitoa kwenu muhanga na kutuunga mkono
katika mapambano ndio maana leo Afrika Kusini imekuwa huru,” alisema.
Rais Cyril Ramaphosa alisema
ameongeza kuwa Tanzania na Afrika Kusini ina urafiki wa miaka mingi,
hakuna maneno ya kueleza kwa namna ilivyowasaidia wakati wa kuhangaika,
wakati wa kipindi kigumu.
“Afrika katika miaka ijayo
itakuwa na idadi kubwa ya watu hadi kufikia bilioni moja, mahitaji
yataongezeka vilevile. Mahitaji ya kijamii pia yataongezeka kwa kila
raia”.Amesema Rais Ramaphosa.
Jamii ya wafanyabiashar Afrika
Kusini wanafikia asilimia 70, maana yake fursa hii hatutaiacha. Tuna
kampuni zaidi ya 208 hapa Tanzania ambapo kuna waajiriwa zaidi ya
21,000.
“Huu ndio wakati wa kuimarisha
viwanda na uwekezaji, inawezekana tulifanikiwa kuondoa changamoto
tulizokuwa nazo awali, lakini ili kufanya hivyo lazima tuondoe vikwanzo
katika ufanyaji biashara.
Jambo kubwa kwa waafrika ni
kuendeleza uchumi wa ndani ambao unasaidia kukuza biashara, bara la
Afrika lina changamoto nyingi lakini fursa zilizopo ni nyingi pia.
Tunaiona Afrika kama bara linalokua kwa kasi na sisi tupo tayari, kwa
kuwa sisi ndio tutakaokuwa wa kwanza kukuza na kuliongoza bara hili,
lazima tuwe tayari kwa mabadiliko haya.
0 comments:
Post a Comment