Rais Mstaafu Awamu ya Tatu,
Tanzania Mhe. Benjamin Mkapa, akihutubia katika Mhadhara wa Viongozi na
Wajumbe wa SADC, uliofanyika leo katika maktaba ya Chuo Kikuu cha Dar es
Salaam.
Rais Mstaafu Awamu ya Tatu,
Tanzania Mhe, akiwa katika picha ya pamoja na Mabalozi kutoka nchi
mbalimbali na Viongzi wa SADC, mara baada ya muhadhara uliofanyika leo
Agosti 15, 2019 katika maktaba ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
Rais Mstaafu Awamu ya Tatu,
Tanzania Mhe, akiwa katika picha ya pamoja na Viongozi wa Serikali ya
Wanafunzi Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) na Viongzi wa SADC, mara
baada ya muhadhara uliofanyika leo Agosti 15, 2019 katika maktaba ya
Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
Baadhi ya Washiriki wa Muhadhara
wa SADC, unaohusu masuala ya Kuongeza Ushirikiano kwa Nchi za Kusini mwa
Afrika wakifuatilia hotuba ya Rais Mstaafu Awamu ya Tatu, Tanzania Mhe,
Muhadhara huo ulifanyika leo Agosti 15, 2019 katika maktaba ya Chuo
Kikuu cha Dar es Salaam.
…………………..
Na.Mwandishi Wetu-MAELEZO.
Jumuiya ya Maendeleo ya nchi
za Kusini mwa Afrika (SADC) inatakiwa kukumbuka na kurejea kwenye Dira
na Dhima za Jumuiya hiyo ili kuweza kuimarisha, kuongeza na kuwezesha
ushirikiano wa nchi za kusini mwa Afrika kuwa katika lengo moja na
kusonga.
Hayo yalisemwa na Rais Mstaafu wa
Awamu ya Tatu, Tanzania Mhe. Benjamin Mkapa alipokuwa akizungumza leo
katika mhadhara wa wajumbe na viongozi wa SADC katika Maktaba ya Chuo
Kikuu cha Dar es Salaam.
Rais Mkapa alisema kuwa katika
kujenga uchumi ulioimara nchi hizo zinatakiwa kukumbuka Dira na Dhima ya
kuanzishwa kwa Jumuiya hiyo ya nchi za Kusini mwa Afrika ili kuweza
kuimarisha uchumi ulioendelevu; wenye kuwezesha wananchi kutoka nchi
wanachma kuwa na maisha bora.
“Naamini kuwa SADC imeweza
kuchangia kwa kiasi kikubwa kwenye muundo wa Maendeleo ya Bara la
Afrika, na suala hili linapaswa kutangazwa ili ushirikiano huu uendelee
kwa wananchi wanachama wa SADC, lakini haya yote yamesababishwa na kuwa
na Dira na Dhima ambayo inaruhusu nchi hizi kuwaza na kutekeleza mawazo
yao pamoja”, alisema Mkapa.
Kiongozi huyo Mstaafu alisema kuwa
SADC inatakiwa kukumbuka Dira ya kuanzishwa kwa Jumuiya hiyo ambayo ni
kuunganisha na kuhusianisha Utumiaji wa rasrimali zilizoko nchi
wanachama ili kuwezesha nchi hizo kujitegemea na kuimarisha uchumi wake
pamoja na maisha ya watu wake.
Mkapa alifafanua kuwa Dira hiyo
inapaswa kutekelezwa huku nchi wanachama wakikumbuka waasisi wa SADC
akiwemo Baba wa Taifa, Hayati Julius Nyerere kuwa ilikuwa ni kuungana
nakufanya kazi kwa pamoja ili kulinda rasrimali na kuwezesha wananchi
kujitegemea kwa kuisha maisha yaliyobora.
Aidha, Mkapa alisema kuwa SADC ina
dhima kubwa ya kuendeleza uchumi endelevu na ulio sawa kwa nchi
wanachama kupitia mifumo mizuri, utawala bora na kuongeza ushirikiano wa
nchi hizo, na vitu hivyo vitawezesha upatikanaji wa amani na usalama
kwa nchi wanachama pamoja na ujenzi wa miradi mbalimbali ya ushirikiano.
“Dira ya SADC ni moja na nguzo
muhimu katika utekelezaji wa miradi ya Maendeleo ikiwemo miradi ya
Nishati, Miundombinu ya usafarishaji na ujenzi wa viwanda hii yote ni
utekelezaji wa kuifanya SADC kuwa katika uchumi ulio sawa ukanda huu wa
nchi za kusini mwa Afrika”, alisema
Aliongeza kuwa Miundombinu ya nchi
za Afrika inatakiwa kuimarishwa kama mkakati wa nchi za SADC
unavyoeleza, kwa sasa SADC inatakiwa ijikite katika ujenzi wa Viwanda na
Nishati ambapo vitu hivyo vikitekelezwa SADC itasonga mbele.
Kwa upande wake Naibu Waziri Mkuu
na Waziri wa Mambo ya Nje na Uhusiano wa Namibia, Natumbo Nandi
Ndaitwah, alisema kuwa Jumuiya ya SADC inapaswa kuzingatia kumbukumbu ya
kuasisiwa kwake ili kuweza kusonga mbele katika mashirikiano ya pamoja
kwa nchi hizi.
Waziri Ndaitwah alisema kuwa
kumbukumbu ya Waasisi wa SADC itakumbukwa milele huku akiitaja Tanzania
kuwa ni moja ya Taifa ambalo limeweza kusaidiwa kwa kiasi kikubwa katika
ukombozi wa Afrika na kundwa kwa jumuiya hiyo.
“Nchi wanachama wa SADC tunapaswa
kujua kuwa Tanzania ni taifa ambalo limewezesha kwa kiasi kikubwa
kuzaliwa kwa Jumuiya hii, kwani Mwl. Nyerere aliwezesha nchi nyingi za
upande wa Kusini mwa Afrika kukombolewa na alikuja na wazo la kuunda
Jumuiya ya SADC ili nchi za kusini zipate kufanya kazi pamoja na
kuimarisha maisha ya watu wao”, Naibu Waziri Mkuu, Ndaitwah.
Waziri Ndaitwa alisema kuwa
Mwl.Nyerere ni mfano wa kuigwa kwa nchi wanachama wa SADC na anapaswa
kubaki katika kumbukumbu ili vizazi vijavyo viweze kukumbuka kuwa kuna
Mwanzilishi na mkombozi wa Nchi za Kusini mwa Afrika.
“Namshukuru Baba wa Taifa,
Mwl.Julius Nyerere, aliyetangaza kuwa, Tanzania haiwezi kuwa huru kama
Bara la Afrika halijakombolewa, nayasema haya ili tujue tulikotoka na
nani alifanya kitu gani ili tuweze kusonga mbele katika Jumuiya hii ya
Nchi za Kusini mwa Afrika”, Naibu Waziri Mkuu, Ndaitwah.
0 comments:
Post a Comment