Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.
Anthony Mtaka akizungumza na viongozi na wadau wa elimu katika mkoawa
Simiyu katika Kikao cha Tathmini ya Matokeo ya Mtihani wa Taifa wa
kidato cha Sita mwaka 2019 na Matokeo ya Mtihani wa Mock kilichofanyika
Agosti 22, 2019 Mjini Bariadi.
Maafisa Elimu wa Wilaya, kata,
wakuu wa shule na wadau wengine wa elimu mkoani Simiyu, wakimsikiliza
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka(hayupo pichani), katika kikao
cha tathmini ya ya Matokeo ya Mtihani wa Taifa wa kidato cha Sita mwaka
2019 na Matokeo ya Mtihani wa Mock kilichofanyika Agosti 22, 2019 Mjini
Bariadi.
Maafisa Elimu wa Wilaya, kata,
wakuu wa shule na wadau wengine wa elimu mkoani Simiyu, wakimsikiliza
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka(hayupo pichani), katika kikao
cha tathmini ya ya Matokeo ya Mtihani wa Taifa wa kidato cha Sita mwaka
2019 na Matokeo ya Mtihani wa Mock kilichofanyika Agosti 22, 2019 Mjini
Bariadi.
Baadhi ya Wajumbe wa Kamati ya
Ulinzi na Usalama ya Mkoa wakifuatilia hotuba ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu,
Mhe.Anthony Mtaka(hayupo pichani), ya kufunga Kikao cha Tathmini ya
Matokeo ya Mtihani wa Taifa wa kidato cha Sita mwaka 2019 na Matokeo ya
Mtihani wa Mock kilichofanyika Agosti 22, 2019 Mjini Bariadi.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.
Anthony Mtaka akimkabidhi zawadi mmoja wa walimu walifanikisha wanafunzi
kupata alama A katika Mtihani wa Taifa wa Kidato cha Sita mwaka 2019
katika Kikao cha Tathmini ya Matokeo ya Mtihani wa Taifa wa kidato cha
Sita mwaka 2019 na Matokeo ya Mtihani wa Mock kilichofanyika Agosti 22,
2019 Mjini Bariadi.
Mwenyekiti wa Chama Cha Walimu
Mkoa wa Simiyu akichangia hoja katika Kikao cha Tathmini ya Matokeo ya
Mtihani wa Taifa wa kidato cha Sita mwaka 2019 na Matokeo ya Mtihani wa
Mock kilichofanyika Agosti 22, 2019 Mjini Bariadi.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.
Anthony Mtaka akizungumza na viongozi na wadau wa elimu katika mkoawa
Simiyu katika Kikao cha Tathmini ya Matokeo ya Mtihani wa Taifa wa
kidato cha Sita mwaka 2019 na Matokeo ya Mtihani wa Mock kilichofanyika
Agosti 22, 2019 Mjini Bariadi.
…………………………
Na Stella Kalinga, Simiyu RS
Mkuu wa mkoa wa Simiyu, Mhe
Anthony Mtaka amesema wanafunzi kidato cha nne waliopata daraja sifuri
katika mtihani wa Mkoa wa Kujipima ‘Mock’ watawekwa katika kambi maalum
ya kitaaluma na kufundishwa na walimu mahiri kwa lengo la kuwasaidia
kuongeza ufaulu na kufikia daraja la nne na kuendelea, katika mtihani
wa Taifa mwaka huu 2019.
Mtaka ameyasema hayo Agosti 22,
2019 katika kikao cha tathmini ya matokeo ya mtihani wa Mock kwa
wanafunzi wa kidato cha nne na matokeo ya mtihani wa Taifa wa kidato cha
sita mwaka 2019, ambapo mkoa wa Simiyu umekuwa miongoni mwa mikoa kumi
bora Kitaifa.
Mtaka amesema lengo la Mkoa ni
kuona wanafunzi wote waanafanya vizuri na hakuna mwanafunzi wa kidato
cha nne anapata daraja sifuri hivyo wanafunzi wote wenye daraja sifuri
na wale walipata daraja la nne alama za mwisho watawekwa pamoja na
kutafutiwa walimu mahiri ili wawasaidie kupanda kitaaluma na kupata
ufaulu mzuri.
“ Tutaweka kambi ya wanafunzi wote
waliopata sifuri kwenye mtihani wa ‘Mock’ lakini pia hata wale
waliopata daraja daraja la nne alama zinazoashiria kuelekea kwenye
sifuri, Siku sitini kabla ya mtihani wafundishwe masomo manne tu,
Civics(Uraia), Kiswahili, Kiingereza na Historia ngalau wapate alama D
ili wapate cheti; nia yetu kama mkoa ni kuona kila mwanafunzi anafanya
vizuri” alisema
Katika hatua nyingine Mtaka
amewahimiza wakuu wa shule kusimamia kwa karibu ufundishaji na
kuhakikisha katika kipindi hiki kuelekea katika mitihani wa Taifa wa
Kidato cha nne, kuongeza ufaulu kutoka nafasi ya tisa ya mwaka 2018
kwenda kwenye nafasi nzuri zaidi.
Afisa elimu wa mkoa wa Simiyu,
Mwl. Ernest Hinju amewataka wakuu wa shule na maafisa elimu kata na
wilaya kuendelea kusimamia ufundishaji ili wanafunzi waweze kufanya
vizuri na wale ambao shule zao hazikufanya vizuri waimarishe usimamizi
ili kuongeza ufaulu.
Kwa upande wake Mkuu wa Shule ya
Sekondari Itilima amezungumzia kambi maalum za kitaaluma kwa wanafunzi
wa kidato cha nne waliopata sifuri kwenye mtihani wa Mock ambao wapo
takribani 2000 kati ya wanafunzi zaidi ya 9000, kwamba zitakuwa msaada
kwao na wanatarajia kuzifanya kwa ufanisi ili mkoa uwe kati ya mikoa
tisa bora Kitaifa mwaka 2019(Single digit).
Mkuu wa mkoa ameahidi kutoa
shilingi elfu 30 kwa mwalimu katika kila alama A itakayopatikana kwenye
somo lake, shilingi milioni tano kwa shule itakayoingia kumi bora
kitaifa, Milioni tano kwa Halmashauri itakayoingia kumi bora kitaifa, na
milioni mbili kwa mwanafunzi atakayepata ufaulu daraja la kwanza
pointi saba na kuwa katika kumi bora kitaifa na ikiwa hatakuwa miongoni
mwa wanafunzi bora kitaifa atapewa shilingi milioni moja.
Mkutano wa tathimini ya matokeo ya
kidato cha sita mkoani Simiyu unawakutanisha wakuu wa shule za
sekondari,maafisa elimu wilaya ,wakurugenzi watendaji, wenyeviti wa
halmashauri za wilaya na wenyeviti wa Kamati za Elimu za Halmashauri
lengo likiwa ni kuangalia walipo na wanapoelekea katika maendeleo ya
elimu mkoani Simiyu
0 comments:
Post a Comment