****************
Baada ya Mfumo wa Kupokea
Malalamiko ya Wananchi dhidi ya utendajikazi wa watumishi wa Umma
kuonyesha mafanikio makubwa ambapo hadi sasa umekamilika 99% na
unatarajiwa kuzinduliwa Rasmi mwishoni mwa mwezi huu, sasa Mkuu wa Mkoa
wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda amewaita tena Wataalamu wa ICT kufika
ofisini kwake kwaajili ya Kuunda Mfumo wa Kusajili ndoa zote
zilizofungwa kwa lengo la kuwalinda wanawake dhidi ya Wanaume walaghai
wenye mchezo wa kutoa ahadi ya kuoa na mwisho wa siku wanaingia mitini.
RC Makonda amesema mfumo huo
utasajili ndoa zote zilizofungwa kidini ikiwemo za Kikristo,Kislamu na
zile zilizofungwa Kiserikali pamoja na kuchukuwa taarifa za Idadi ya
watoto ndani ya ndoa.
Aidha RC Makonda amesema lengo la
jitiada zote hizo ni kumlinda mwanamke dhidi ya Matapeli wa Mapenzi
ambao wamekuwa na mchezo wa kuwachezea kinadada kwa kuwaahidi kuwa
watawaoa na pindi wanapopata kile wanachokitaka wanaingia mitini jambo
linalowaumiza wanawake na kupelekea baadhi yao kutaka kujiua, kupunguza
ufanisi wa kazi na pia wengine kujikuta wanawachukia wanaume bila sababu
yoyote.
Pamoja na hayo RC Makonda amesema
mpango huo pia unalenga kuzilinda ndoa zilizofungwa zisivunjike jambo
litakalosaidia ustawi bora wa familia.
Mhe. Makonda amesema Mpango huo
haulengi kuwatetea wanawake pekee bali hata wanaume waliowahi
kuwagharamikia wanawake kwa kuwasomesha, kuwajengea nyumba, biashara na
kuwapatia magari wanayo haki ya kurudishiwa gharama walizotumia.
0 comments:
Post a Comment