Katibu Mtendaji wa Balaza la
Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC) Bi. Beng’I Issa akizungumza
na Vijana wa Mkoa wa Ruvuma kuhusu Programu ya Mafunzo ya Ujasiriamali
na Usimamizi wa Biashara wakati wa ufunguzi wa mafunzo hayo katika Mkoa
wa Ruvuma, Agosti 10, 2019.
Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa
Ruvuma Bw. Hakimu Mafuru akizungumza na vijana walioshiriki katika
mafunzo hayo ya ujasiriamali yaliyofanyika katika mkoa huo. (Kulia) ni
Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Songea Bw. Philliph Beno.
Baadhi ya vijana
wanaojishughulisha na shughuli za kiuchumi wakifuatilia maelezo ya
Katibu Mtendaji wa Balaza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi
(NEEC) Bi. Beng’I Issa (hayupo pichani) alipokuwa akielezea kuhusu
Programu ya Mafunzo ya Ujasiriamali.
Sehemu ya wajasiriamali
wanaomiliki biashara wakifuatailia maelezo ya Katibu Mtendaji wa Balaza
la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC) Bi. Beng’I Issa (hayupo
pichani) alipokuwa akifungua mafunzo hayo katika mkoa huo.
Meneja wa Ufuatiliaji na Tathmini
Bi. Flora Kajela akielezea kuhusu malengo ya Programu ya Mafunzo ya
Ujasiriamali wakati wa ufunguzi wa mafunzo hayo yaliyofanyika katika
Mkoa wa Ruvuma.
Mchumi Mkuu kutoka Ofisi ya
Waziri Mkuu, Bw. Daudi Sailasi akielezea kuhusu programu ya kuongeza
ujuzi kwa vijana inayoratibiwa na ofisi hiyo wakati wa ufunguzi wa
mafunzo ya Ujasiriamali na Usimamizi wa Biashara yaliyofanyika katika
Mkoa huo. (Kulia) ni Katibu Mtendaji wa Balaza la Taifa la Uwezeshaji
Wananchi Kiuchumi (NEEC) Bi. Beng’I Issa.
Mwezeshaji kutoka Balaza la Taifa
la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC), Bw. Lucas Mafuru akitoa mada
kuhusu uchambuzi wa ushindani na mikakati ya masoko kwa wajasiriamali
(hawapo pichani).
Afisa Maendeleo ya Vijana kutoka
Ofisi ya Waziri Mkuu, Bw. Eliakim Mtawa akitoa mada kuhusu vihatarishi
vya biashara na namna ya kuvikabili kwa wajasiriamali walioshiriki
mafunzo hayo.
Mmoja wa Wajasiriamali Bw.
Richard Mpagala akielezea kuhusu mbinu anazotumia kuendesha biashara
yake alipokua amejifunza kuhusu masuala ya mapato na matumizi katika
usimamizi wa biashara.
Bi. Pudencia Msangawale akionesha
bidhaa anazotengeza na akielezea mbinu anazotumia kutafuta masoko ya
bidhaa zake katika eneo lake la biashara.
Katibu Mtendaji wa Balaza la
Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC) Bi. Beng’I Issa (katikati)
akiwa kwenye picha ya pamoja na wawezeshaji wa mafunzo ya Ujasiriliamali
kutoka kwenye Ofisi hiyo, Ofisi ya Waziri Mkuu na Taasisi za Umma.
Katibu Mtendaji wa Balaza la
Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC) Bi. Beng’I Issa (katikati)
akiwa kwenye picha ya pamoja na wajasiriamali walioshiriki mafunzo hayo
ya ujasiriamali na usimamizi wa biashara.
……………………………………………………..
Na; Mwandishi Wetu
Vijana Mkoa wa Ruvuma wamefurahia
fursa ya mafunzo ya ujasiriamali na usimamaizi wa biashara yaliyotolewa
na Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC) kwa
kushirikiana na Ofisi ya Waziri Mkuu ambayo yatawawezesha vijana hao
kukuza na kurasimisha shughuli zao za kiuchumi.
Akifungua Mafunzo hayo Katibu
Mtendaji wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi Bi. Beng’I
Issa alieleza kuwa mafunzo hayo ya ujasiriamali ni muhimu sana na
yanalenga kuwawezesha vijana wanaomiliki biashara wanapata mbinu za
kuendeshaji na kusimamia biashara zao.
“Mafunzo haya ya ujasiriamali
yameleta tija kwa vijana na wameweza kujiajiri kwa kufanya shughuli
mbalimbali za kiuchumi zenye faida,” alisema Issa
Alieleza kuwa vijana wanapaswa
kuchangamkia fursa hizo zinapojitokeza ili waweze kuunganishwa na fursa
za mitaji na mitandao ya huduma za biashara, pia kuwajengea uwezo wa
kufanya shughuli zao za kiuchumi kwa kujiamini na kuweza kuweza kupata
faida.
“Vijana mnapaswa kutambua ninyi
ndio nguvukazi ya Taifa, hivyo kuwa wabunifu ni jambo la msingi katika
biashara zenu mkitambua fursa mlizonazo ili muweze kushindana katika
biashara,” alisema Issa
Akibainisha aina ya mafunzo ya
ujasiriamali watakayopatiwa vijana hao yakiwemo masuala ya uchambuzi wa
masoko, dhana ya ujasiriamali, uchambuzi wa mahitaji ya mteja, kutambua
ushindani wa soko, mkakati na uendeshaji biashara, utambuzi wa masoko,
usimamizi wa fedha, vihatarishi vya biashara na namna ya kuvikabili,
usimamizi wa biashara na rasilimali watu, urasimishaji wa biashara na
vyanzo vya mitaji.
Aliongeza kuwa Programu hii ya
mafunzo ya ujasiriamali kwa vijana itawawezesha kutambua mapungufu
waliyonayo na kutumia mwanya huo kuangalia fursa walizo nazo katika
ushindani wa biashara zao.
“Ni muhimu vijana mkawekeza
katika biashara mnazozimudu kimtaji, kiusimamizi kwa ushindani na
kufanya maamuzi sahii,” alieleza Issa
Alieleza kuwa kila Mkoa una fursa
zinazoweza kutumiwa na wajasiriamali katika kujiendeleza kiuchumi,
vijana wanatakiwa kuchangamkia fursa hizo ili waweze kunufaika kwa njia
mbalimbali.
Alifafanua kuwa Ofisi yake
imekuwa ikiendesha mafunzo ya aina hii kwa kushirikiana na wadau
mbalimbali ikiwemo Taasisi za Umma, Wadau wa Mendeleo, Sekta binafsi na
jamii kwa ujumla.
“Zaidi ya Vijana 10,000 wameweza
kufikiwa na programu mbalimbali za mafunzo ikiwemo Kijana jiajiri, Ajira
yangu, Kliniki ya vijana wahitimu wa vyuo vya elimu ya juu, mifuko ya
uwezeshaji na watoa huduma,” alisema Issa
Aidha, alitoa shukrani zake kwa
Ofisi ya Waziri Mkuu kwa kuona haja ya kuwekeza kwa vijana kwa kuwapatia
ujuzi ili waweze kujiajiri, kuajiri na kuchangia katika pato la taifa.
Kwa Upande wake, Kaimu Katibu
Tawala wa Mkoa wa Ruvuma Bw. Hakimu Mafuru amewahimiza vijana wa Mkoa
huo kuchangamkia fursa za mafunzo kama hayo yanayotolewa na Serikali
pamoja na wadau mbalimbali kwa kuwa yatawawezesha kujitambua na
kujisimamia wenyewe na kuongeza tija kwenye biashara zao.
Mmoja wa Vijana walioshiriki
katika Mafunzo hayo, Bi. Pudencia Msangawale alieleza kuwa mafunzo hayo
yatajibu changamoto ambazo wamekuwa wakikumbana nazo kama wajisiriamali
ikiwemo masuala ya ujuzi, maarifa, kurasimisha biashara, namna bora ya
kuhudumia wateja na utafutaji wa masoko.
“Ninawashukuru Ofisi ya Waziri
Mkuu pamoja na Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi kwa elimu
waliyotupatia yametuwezesha kujitambua, kuwa wabunifu, waaminifu na
kuweza kujisimamia katika biashara,” alisema Msangawale.
Mafunzo hayo yanaratibiwa na
Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC) kwa kushirikiana
na Ofisi ya Waziri Mkuu ambayo yatafanyika katika Mikoa nane (8) ya
Tanzania Bara ikiwemo Dodoma ambapo tayari yamekisha fanyika, Ruvuma,
Geita, Mwanza, Lindi, Mbeya, Tanga na Arusha.
0 comments:
Post a Comment