Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa
akitazama mahali ambapo lori la mafuta lilipinduka na kushika moto
hatimaye kusababisha vifo vya watu 69 kwenye eneo la Msamvu mjini
Morogoro wakati alipotembelea eneo hilo, Agosti 11, 2019. (Picha na
Ofisi ya Waziri Mkuu).
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa
akizungumza na waombolezaji wakati aliposhiriki katika maandalizi ya
kutambua miili na maziko ya watu 69 waliofariki dunia katika ajali ya
lori la mafuta lililopinduka na kushika moto katika eneo la Msamvu mjini
Morogoro. Alizungumza na waombolezaji hao kwenye viwanja vya hospitali
ya mkoa wa Morogoro, Agosti 11, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Baadhi ya waombolezaji
wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipozungumza baada ya
kushiriki katika maadalizi ya kutambua miili na mazishi ya watu 69
waliofariki dunia katika ajali ya lori la mafuta lililopinduka na
kushika moto kwenye eneo la Msamvu mjini Morogoro. Alizungumza na
waombolezaji hao kwenye viwanja vya hospitali ya mkoa wa Morogoro,
Agosti 11, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa
akizungumza na baadhi ya Mawaziri na viongozi wa mkoa wa Morogoro
walioshiriki katika maandalizi ya kutambua miili na maziko ya watu 69
waliofariki dunia katika ajali ya lori la mafuta lililopinduka na
kushika moto kwenye eneo la Msamvu mjini Morogoro. Alikuwa kwenye
viwanja vya hospitali ya mkoa wa Morogoro, Agosti 11, 2019. Kutoka
kushoto ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais TAMISEMI, Selemani Jafo, Waziri
wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu,
Mwenyekiti wa CCM wa Mkoa wa Morogoro, Innocenti Kalogelisi, Waziri wa
Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye
Ulemavu, Jenista Mhagama, Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi
Lugola, Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Dkt. Stephene Kebwe, Waziri wa Ujenzi,
Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi, Isack Kamwelwe na kulia ni Naibu
Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Ashatu Kijaji. (Picha na Ofisi ya
Waziri Mkuu)
0 comments:
Post a Comment