METDO Tanzania

METDO Tanzania

Thursday, August 29, 2019

VAN DIJK NDIYE MWANASKA BORA ULAYA, AWAANGUSHA MESSI NA RONALDO


KLABU ya Liverpool imetamba kwenye tuzo za wanasoka bora wa Shirikisho la Soka Ulaya (UEFA) usiku wa leo mjini Monaco, Ufaransa huku beki wake, Virgil Van Dijk akiwaangusha Lionel Messi na Cristiano Ronaldo. Beki Mholanzi, Van Dijk amewashinda Messi na Ronaldo katika tuzo ya Mwanasoka Bora wa Mwaka wa Kiume Ulaya baada ya kutoa mchango mkubwa kwa Liverpool kutwaa taji la Ligi ya Mabingwa mwezi Juni mjini Madrid. Van Dijk anarithi tuzo hiyo kutoka kwa Luka Modric wa Croatia na Real Madrid, ambaye naye aliichukua kwa Ronaldo aliyekaa nayo miaka miwili mfululizo akiwa Bernabeu. Mwaka 2015 tuzo hiyo ilichukuliwa na Messi kutoka kwa Ronaldo aliyeitwaa akiwa bado Real Madrid mwaka 2014.

Beki Mholanzi, Virgil Van Dijk akiwa ameshika tuzo zake mbili leo 

WASHINDI WALIOPITA TUZO YA MWANASOKA BORA WA ULAYA

2018 - Luka Modric (Real Madrid)
2017 - Cristiano Ronaldo (Real Madrid)
2016 - Cristiano Ronaldo (Real Madrid)
2015 - Lionel Messi (Barcelona)
2014 -  Cristiano Ronaldo (Real Madrid)

Naye kipa namba moja wa Liverpool, Allison ameshinda tuzo ya Mlinda Mlango Bora wa msimu wa 2018-19 wa UEFA, kufuatia mafanikio yake msimu uliopita Anfield.
Kiungo Mholanzi, Frenkie de Jong ameshinda tuzo ya Kiungo Bora baada ya kuiwezesha Ajax kufika Nusu Fainali msimu uliopita.
Nyota wa Barcelona, Messi akafanikiwa kuondoka na tuzo ya Mshambuliaji Bora wa UEFA baada ya kufunga mabao 12 katika mechi 10 za msimu uliopita.
Naye nyota wa England na Lyon, Lucy Bronze akafanikiwa kushinda tuzo ya Mwanasoka Bora wa Kike wa UEFA.
Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com