Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania Mhe. Kassim M. Majaliwa akiagana na Kamishna Mkuu wa
Shirika la Kuhudumia Wakimbizi Duniani (UNHCR) Bw Filippo Grandi mara
baada ya kumalizika kwa mazungumzo baina yao kuhusu wakimbizi waliopo
Tanzania. Mazungumzo hayo yamefanyika Yokohama, Japan.
……………………
SERIKALI ya Tanzania itaendelea
kushirikiana na Shirika la Kuhudumia Wakimbizi la Umoja wa Mataifa
(UNHCR) katika kutatua changamoto zinazotokana na uwepo wa wakimbizi
nchini pamoja na kutafuta suluhu ya kudumu kwenye nchi zao ili wakimbizi
hao waweze kurejea makwao kuendelea na shughuli za maendeleo.
Kauli hiyo imetolewa na Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa leo (Ijumaa, Agosti 30, 2019) katika mazungumzo
yake na Kamishna Mkuu wa UNHCR, Bw. Filippo Grandikwenye Kituo cha
Maonyesho cha Yokohama nchini Japan baada ya kuhitimishwa kwa Mkutano wa
Saba wa Kimataifa wa Tokyo kuhusu Maendeleo ya Afrika (Tokyo International Conference on African Development – TICAD 7).
Katika mazungumzo hayo, Waziri
Mkuu amesisitiza umuhimu wa UNHCR kuisaidia mikoa inayokaliwa na
wakambizi kutokana na kuharibiwa kwa mazingira. “Hata hivyo Serikali ya
Tanzania itaendelea kushirikiana na UNHCR kuimarisha ulinzi wa maeneo ya
wakimbizi ili wananchi wa maeneo hayo waendelee kuishi kwa amani na
utulivu.”
Kwa upande wake, Kamishna Mkuu
wa Shirika la Kuhudumia Wakimbizi la Umoja wa Mataifa (UNHCR), Bw.
Filippo Grandi amesema amefurahishwa na utayari wa Serikali ya Tanzania
katika kupokea wakimbizi na usikivu wa Rais Dkt. John Magufuli katika
kushughulikia changamoto za wakimbizi.
Waziri Mkuu yupo nchini Japan
akimwakilisha Rais Dkt. John Magufuli kwenye Mkutano wa Kilele wa Saba
wa Kimataifa wa Tokyo kuhusu Maendeleo ya Afrika (Tokyo International Conference on African Development – TICAD 7) ambao umehitimishwa leo.
Waziri Mkuu ameambatana na
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika ya Mashariki, Profesa
Palamagamba Kabudi na viongozi mbalimbali kutoka Serikali ya Muungano
wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
0 comments:
Post a Comment