Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Tiba ya Mifupa MOI, Dkt.Respicious Boniface akizungumza na Waandishi wa Habari (hawapo pichani), kuhusu mafanikio ya Taasisi hiyo kwa miaka minne ya Serikali ya Awamu ya Tano,Mkutano ulifanyika katika Ukumbi wa Idara ya Habari-MAELEZO Jijini Dar es Salaam.
*************************************
Na Mwandishi Wetu,
TAASISI ya Tiba
ya Mifupa, Upasuaji wa Ubongo na Mishipa ya Fahamu (MOI) katika kipindi
cha miaka minne ya Serikali ya Awamu ya Tano imeokoa kiasi cha Tsh.
Bilioni 38.4 zilizotakiwa kutumika kwa ajili ya kusafirisha wagonjwa
43,200 nje ya nchi kwa ajili ya kupata huduma za matibabu ya upasuaji wa
kibingwa.
Hayo
yamebainishwa leo Ijumaa (Novemba 22, 2019) Jijini Dar es Salaam na
Mkurugenzi Mtendaji wa MOI, Dkt. Dkt Respicious Boniface na kuongeza
kuwa katika kipindi cha miaka minne ya Utawala wa Serikali ya Awamu ya
Tano, Taasisi hiyo imeendelea kuimarisha na kuboresha huduma mbalimbali
za afya kwa wananchi.
Dkt. Respicious
anasema kutokana na maboresho na kuimarika kwa huduma ya afya, Taasisi
ya MOI ndani ya kipindi cha miaka minne imeweza kufanya upasuaji kwa
wagonjwa 43,200 waliofanyiwa upasuaji wa kibingwa na hivyo kuokoa
maisha ya Watanzania wengi na pesa za Serikali ambazo zingetumika
kupeleka wagonjwa nje ya nchi kwa matibabu.
‘Gharama za
matibabu za wagonjwa hao kwa ndani ya nchi zilikuwa Tsh Bilioni 16.5 na
kama wagonjwa hao wangepelekwa nje ya nchi kwa matibabu, jumla ya Tsh
Bilioni 54.9 zingetumika, na hivyo kuifanya taasisi kuokoa kiasi cha Tsh
Bilioni 38.4 ambazo zitatumika kwa shughuli nyingine za maendeleo’’.
Aliongeza kuwa
Taasisi hiyo katika kipindi cha miaka minne iliyopita imeweza kupokea
kiasi cha Tsh. Bilioni 16.5 kwa ajili ya kukamilisha miradi mbalimbali
ikiwemo jengo jipya la MOI pamoja na ununuzi wa vifaa tiba vya kisasa
ambavyo vimeweza kuleta mageuzi na maboresho ya huduma za afya katika
Taasisi hiyo.
Akitolea mfano,
Dkt. Respicious anasema katika fedha hizo zilizotolewa na Serikali,
taasisi hiyo iliweza kuongeza idadi ya vitanda kutoka 150 hadi 350 kwa
wagonjwa wa kawaida, na kufanya kutowepo na mgongjwa anayelala chini kwa
sasa, sambamba na kuongeza idadi ya vitanda kwa wagonjwa wanaohitaji
uangalizi maalum kutoka vitanda 8 hadi 18.
Aidha Dkt.
Respicious anasema kuwa pia katika fedha hizo, Taasisi hiyo imeweza
kuongeza vyumba vya upasuaji kutoka vyumba 6 hadi 9, kuongeza vyumba 32
vya wagonjwa binafsi vya daraja la juu pamoja na kuongeza chumba cha
upasuaji kwa mgonjwa bila kulazimika kulala hospitali.
Kuhusu vifaa Dkt.
Respicious anasema, katika fedha hizo, pia Taasisi ya MOI iliweza
kununua mashine mpya za kutolea dawa za usingizi, mashine za kisasa za
Radiolagia zikiwemo MRI, CT-Scan, Digital X-Ray, CR X-ray, Portable
X-ray, Ultra Sound 2, ECHO na ECG, ununuzi wa mashine mbili mpya za
kisasa za vipimo vya maabara.
Akifafanua zaidi,
Dkt. Respicious anasema kutokana na maboresho hayo, Taasisi hiyo ndani
ya kipindi cha miaka mine imeweza kufanya upasuaji kwa wagonjwa 43,200
waliofanyiwa upasuaji wa kibingwa na hivyo kuokoa maisha ya Watanzania
wengi na pesa za Serikali ambazo zingetumika kupeleka wagonjwa nje ya
nchi kwa matibabu.
‘Mbinu hii
imesaidia kuongeza idadi ya wagonjwa wa upasuaji kutoka 400-500 kwa
mwezi hadi kufikia 700-900 kwa mwezi, na idadi ya wagonjwa hao
waliofanyiwa upasuaji wa kibingwa ni pamoja na kubadilisha nyonga (900),
kubadilisha magoti (870), upasuaji wa mfupa wa kiuno (618), watoto
wenye vichwa vikubwa na mgongo wazi (2,070)’’ alisema Dkt. Respicious.
Aidha Dkt.
Respicious anasema Taasisi ya MOI pia imeanzisha huduma mpya ikiwemo
huduma ya upasuaji wa magoti/mabega kwa njia ya matundu ambapo hadi sasa
wagonjwa 800 wamefanyiwa upasuaji pamoja na huduma ya upasuaji wa
kuondoa vivimbe vya mishipa ya damu kwenye ubongo ambapo wagonjwa watano
pia wamefanyiwa upasuaji huo.
Anaitaja huduma
nyingine kuwa ni pamoja na uanzishwaji wa wodi maalum ya kulazwa na
kufanyiwa upasuaji siku hiyo hiyo, ambapo wagonjwa 355 wamefanyiwa
upasuaji na kufanya upasuaji wa uti wa mgongo kwa kupitia tundu dogo,
ambapo hadi sasa wagonjwa 120 wamefanyiwa upasuaji.
‘Huduma hizi
mpya, zimeiwezesha Taasisi kupunguza kwa kiasi kikubwa rufaa za wagonjwa
nje ya nchi, ambapo kwa sasa kwa magonjwa ya Neurosurgies asilimia 95
tunafanya hapa na upasuaji wa mifupa asilimia 98 tunafanya hapa pia’’
alisema Dkt. Respicious
Kuhusu huduma ya
tiba mtandao, Taasisi hiyo kupitia Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii,
Jinsia, Wazee na Watoto imejenga chumba maalum ambapo madaktari katika
sehemu mbalimbali za nchi watatuma picha za X-ray/CT-Scan zitakazosomwa
na madaktari bingwa wa radiolojia na majibu yatarudishwa kwa daktari
aliyeomba kwa muda mfupi.
Aidha katika
katika eneo la mafunzo, Dkt. Respicious anasema katika kipindi cha miaka
minne ya Uongozi wa Rais Dkt. John Magufuli, jumla ya madaktari bingwa
50 wa mifupa wamehitimu mafunzo, ukilinganisha na madaktari 7
waliohimtimu katika kipindi cha miaka mine iliyotangulia.
0 comments:
Post a Comment