Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim
Wangabo (mwenye kaunda suti ya Kijivu) akiwa pamoja na wajumbe wa kamati
ya Ulinzi na usalama Mkoa viongozi pamoja na wataalamu wengine
wakikagua jengo kuu la stendi ya mabasi Sumbawanga linaoendelea kujengwa
katika eneo la katumba azimia Sumbawanga Mjini.
Mhandisi wa Manispaa Suleiman
Mziray (T-shirt ya Zambarau) akitoa maelezo ya uzio unaozunguka stendi
ya Mabasi Sumbawanga Kwa Mkuu wa Mkoa na Kamati ya ulinzi na Usalama
pamoja na viongozi na wataalamu wengine waliofika kukagua ujenzi wa
stendi hiyo.
…………………..
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh.Joachim
Wangabo amewataka wananchi wa Mji wa Sumbawanga pamoja na wakandarasi wa
ujenzi wa stendi ya mabasi katika mji wa Sumbawanga kutohujumu
miundombinu ya eneo hilo na badala yake wasaidie kuimarisha ulinzi na
wakandarasi kujenga kwa uzalendo ili kituo hicho kiweze kuwa nembo ya
mkoa wa Rukwa.
Amesema kuwa hajawahi kuona ndani
ya jengo lastendi kukiwa na vyumba vya kulala wageni, migahawa, mabanda
ya mamalishe, sehemu ya kuegeshea bodaboda na bajaji pamojana mabasi na
kufananisha eneo hilo na kiwanda kwakutarajiwa kuzalisha ajira kwa
wananchi wa mkoa wa Rukwa.
“Stendi hii katika Manispaa ya
Sumbwanga itakuwani nembo ya Mkoa wa Rukwa, Sisi Wana Rukwa tutajivunia
sana hii stendi , stendi ambayo sijaona popote ambapo kuna vyumba vya
kulala ndani ya stendi, iko hapa, kuna ‘restaurant’ kuna mabanda ya mama
lishe kuna sehemu ya bodaboda, bajaji, kuna mabasi, kuna kila aina ya
mambo inajitosheleza, hiki kitakuwa nikama kiwanda kidogo maana
kitaajiri watu wengi sana hapa, wale wanaojenga hapa wasihujumu
miundombinu hii,” Alisema.
Ameyasema hayo leo tarehe
28.8.2019 alipotembelea stendi hiyo ya mabasi yam ji wa Sumbawanga
iliyoanza kujengwa mwanzoni mwa mwezi wa tano mwaka 2019 na kutarajiwa
kumalizika mwezi Disemba mwaka huu akiwa ameambatana na Kamati ya ulinzi
na Usalama ya Mkoa, Mkuu wa Wilaya ya Sumbawanga pamoja na Wataaalamu
wengine kutoka Ofisi ya mkuu wa Mkoa na Manispaa ya Sumbawanga.
Akitoa taarifa ya ujenzi huo
Mhandisi wa Manispaa ya Sumbawanga Suleimani Mziray alisema kuwa
kutokana na ufinyu wa fedha stendi hiyo itajengwa kwa awamu mbili na
mpaka sasa ujenzi huo umefikia asilimia 40 na bado mkandarasi anaendelea
na ujenzi na kuongeza kuwa katika jengo hilo kutakuwa na eneo la
kuwahifadhi abiria zaidi ya 400 watakaokuwa wakisubiri safari zao za nje
na ndani ya mkoa.
“Kutokana na Ufinyu wa fedha
ujenzi wa kituo cha mabasi eneo la katumba Azimio utafanyika kwa awamu
mbili ambapo mpaka sasa kazi zimekwishafanyika kwa asilimia 40 na bado
inaendelea kwenye maeno tofauti kulinngana na Mkataba, jengo Kubwa
litakuwa nae neo kwaajili ya kusubiria abiria ambalo litakuwa na uwezo
wa kubeba abiria 400,” Alisema
Aidha Msimamizi wa ujenzi huo kwa
upande wa Mkandarasi Said Rajabu Mbelwa ameongeza kuwa ili kufika kwenye
ghorofa ya kwanza ya jengo hilo kutakuwa na Lifti ili kuwasaidia
walemavu na wale ambao afya zao haziruhusu kutumia ngazi
“Hapa kuna Lifti ambayo itatumika kwaajili ya Walemavu n ahata
ukiwa mgonjwa kwasababu itakuwa siyo rahisi kupita kwenye ngazi ya
kupanda kwa mguu kama una matatizo ya afya, kwahiyo imewekwa kwaajili ya
walemavu na watu amba afya zao si nzuri sana,” Aliongezea.
Hadi kufikia hatua hiyo mkandarasi
SUMRY ENTERPRISES LTD tayari ameshalipwa Shilingi Bilioni 1.72 ambayo
ni sawa na asilimia 28.89 ya Shilingi bilioni 5.95 ambayo ni gaharama ya
ujenzi wa stendi hiyo, ambayo inategemewa kuwa na vyumba vya kulala
waheni, vymba maalumu vya kufanyia mazoezi(Gym), kituo cha polisi,
sehemu ya migahawa mikubwa na mama lishe na sehemu za kuegeshea
Baiskeli, Bodaboda, Bajaji, Teksi na mabasi yanayosafirisha abiria ndani
ya Mkoa na nje ya Mkoa.
0 comments:
Post a Comment