Wednesday, August 28, 2019

Stendi ya Mabasi Sumbawanga Kuwa ya Mfano Mikoa ya Nyanda za Juu kusini

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo (mwenye kaunda suti ya Kijivu) akiwa pamoja na wajumbe wa kamati ya Ulinzi na usalama Mkoa viongozi pamoja na wataalamu wengine wakikagua jengo kuu la stendi ya mabasi Sumbawanga linaoendelea kujengwa katika eneo la katumba azimia Sumbawanga Mjini.
Mhandisi wa Manispaa Suleiman Mziray (T-shirt ya Zambarau) akitoa maelezo ya uzio unaozunguka stendi ya Mabasi Sumbawanga Kwa Mkuu wa Mkoa na Kamati ya ulinzi na Usalama pamoja na viongozi na wataalamu wengine waliofika kukagua ujenzi wa stendi hiyo.
…………………..
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh.Joachim Wangabo amewataka wananchi wa Mji wa Sumbawanga pamoja na wakandarasi wa ujenzi wa stendi ya mabasi katika mji wa Sumbawanga kutohujumu miundombinu ya eneo hilo na badala yake wasaidie kuimarisha ulinzi na wakandarasi kujenga kwa uzalendo ili kituo hicho kiweze kuwa nembo ya mkoa wa Rukwa.
Amesema kuwa hajawahi kuona ndani ya jengo lastendi kukiwa na vyumba vya kulala wageni, migahawa, mabanda ya mamalishe, sehemu ya kuegeshea bodaboda na bajaji pamojana mabasi na kufananisha eneo hilo na kiwanda kwakutarajiwa kuzalisha ajira kwa wananchi wa mkoa wa Rukwa.
“Stendi hii katika Manispaa ya Sumbwanga itakuwani nembo ya Mkoa wa Rukwa, Sisi Wana Rukwa tutajivunia sana hii stendi , stendi ambayo sijaona popote ambapo kuna vyumba vya kulala ndani ya stendi, iko hapa, kuna ‘restaurant’ kuna mabanda ya mama lishe kuna sehemu ya bodaboda, bajaji, kuna mabasi, kuna kila aina ya mambo inajitosheleza, hiki kitakuwa nikama kiwanda kidogo maana kitaajiri watu wengi sana hapa, wale wanaojenga hapa wasihujumu miundombinu hii,” Alisema.
Ameyasema hayo leo tarehe 28.8.2019 alipotembelea stendi hiyo ya mabasi yam ji wa Sumbawanga iliyoanza kujengwa mwanzoni mwa mwezi wa tano mwaka 2019 na kutarajiwa kumalizika mwezi Disemba mwaka huu akiwa ameambatana na Kamati ya ulinzi na Usalama ya Mkoa, Mkuu wa Wilaya ya Sumbawanga pamoja na Wataaalamu wengine kutoka Ofisi ya mkuu wa Mkoa na Manispaa ya Sumbawanga.
Akitoa taarifa ya ujenzi huo Mhandisi wa Manispaa ya Sumbawanga Suleimani Mziray alisema kuwa kutokana na ufinyu wa fedha stendi hiyo itajengwa kwa awamu mbili na mpaka sasa ujenzi huo umefikia asilimia 40 na bado mkandarasi anaendelea na ujenzi na kuongeza kuwa katika jengo hilo kutakuwa na eneo la kuwahifadhi abiria zaidi ya 400 watakaokuwa wakisubiri safari zao za nje na ndani ya mkoa.
“Kutokana na Ufinyu wa fedha ujenzi wa kituo cha mabasi eneo la katumba Azimio utafanyika kwa awamu mbili ambapo mpaka sasa kazi zimekwishafanyika kwa asilimia 40 na bado inaendelea kwenye maeno tofauti kulinngana na Mkataba, jengo Kubwa litakuwa nae neo kwaajili ya kusubiria abiria ambalo litakuwa na uwezo wa kubeba abiria 400,” Alisema
Aidha Msimamizi wa ujenzi huo kwa upande wa Mkandarasi Said Rajabu Mbelwa ameongeza kuwa ili kufika kwenye ghorofa ya kwanza ya jengo hilo kutakuwa na Lifti ili kuwasaidia walemavu na wale ambao afya zao haziruhusu kutumia ngazi “Hapa kuna Lifti ambayo itatumika kwaajili ya Walemavu n ahata ukiwa mgonjwa kwasababu itakuwa siyo rahisi kupita kwenye ngazi ya kupanda kwa mguu kama una matatizo ya afya, kwahiyo imewekwa kwaajili ya walemavu na watu amba afya zao si nzuri sana,” Aliongezea.
Hadi kufikia hatua hiyo mkandarasi SUMRY ENTERPRISES LTD tayari ameshalipwa Shilingi Bilioni 1.72 ambayo ni sawa na asilimia 28.89 ya Shilingi bilioni 5.95 ambayo ni gaharama ya ujenzi wa stendi hiyo, ambayo inategemewa kuwa na vyumba vya kulala waheni, vymba maalumu vya kufanyia mazoezi(Gym), kituo cha polisi, sehemu ya migahawa mikubwa na mama lishe na sehemu za kuegeshea Baiskeli, Bodaboda, Bajaji, Teksi na mabasi yanayosafirisha abiria ndani ya Mkoa na nje ya Mkoa.

No comments:

Post a Comment