katibu Mkuu ofisi ya Rais Tawala
za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI)anayeshughulikia Afya Dk.Doroth
Gwajima,akizungumza na viongozi akiwataka wasaidie kuwahamasisha
wananchi kujiunga na bima ya afya ya jamii ya CHF iliyoboreshwa
alipotembelea Zahanati ya kijiji cha Chiboli wilayani Chamwino mkoani
Dodoma kushuhudia utekelezaji wa kuandikisha Kaya katika mfumo huo.
Muuguzi wa Zahanati ya kijiji cha
Chiboli ,Shija Makeja,akielezea jinsi wanavyoshirikiana na uongozi
uliopo katika kuhamasisha wananchi kujiunga na bima ya afya ya jamii ya
CHF iliyoboreshwa kushoto ni katibu Mkuu ofisi ya Rais Tawala za Mikoa
na Serikali za Mitaa (TAMISEMI)anayeshughulikia Afya Dk.Doroth
Gwajima,akimsikiliza
Meneja mradi wa HPSS Tuimarishe afya, Ally Kebby Abdallah,akizungumzia Azma ya Serikali ni kutengeneza
mfumo wa bima ya afya ya CHF iliyoboreshwa ni kuona mwananchi
anatambuliwa lakini pesa anayochangia irudi kwenye kituo
katibu Mkuu ofisi ya Rais Tawala
za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI)anayeshughulikia Afya Dk.Doroth
Gwajima,akiangalia kibao kinachoonesha ratiba ya kazi katika Zahanati
ya kijiji cha Chiboli wilayani Chamwino mkoani Dodoma alipotembelea
kushuhudia utekelezaji wa kuandikisha Kaya katika mfumo wa bima ya afya
ya CHF iliyoboreshwa.
katibu
Mkuu ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
(TAMISEMI)anayeshughulikia Afya Dk.Doroth Gwajima,akiwahamasisha
wananchi wa kijiji cha Chiboli wajiunge na bima ya afya ya CHF
iliyoboreshwa ili wafurahie huduma bora alipotembelea Zahanati ya
kijiji cha Chiboli wilayani Chamwino mkoani Dodoma kushuhudia
utekelezaji wa kuandikisha Kaya katika mfumo wa bima ya afya ya CHF
iliyoboreshwa.
katibu Mkuu ofisi ya Rais Tawala
za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI)anayeshughulikia Afya Dk.Doroth
Gwajima,mkazi wa kijiji cha Chiboli anayetumia bima ya afya ya CHF
iliyoboreshwa jinsi inavyookoa maisha ya familia yake pindi anapopata na
tatizo
…………………..
Na.Alex Sonna,Chiboli
Serikali imewataka
viongozi wa serikali za Mitaa a vijiji nchini kusaidia kuhamasisha
wanachi kujiunga na bima ya afya ya jamii ya CHF iliyoboreshwa ili
waondokane na adha pindi wanapokuwa hawana fedha za mkononi kulipia
matibabu.
Haya yamebainishwa
na katibu mkuu ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
(TAMISEMI)anayeshughulikia Afya Dk.Doroth Gwajima alipotembelea Zahanati
ya kijiji cha Chiboli wilayani Chamwino mkoani Dodoma kushuhudia
utekelezaji wa kuandikisha Kaya katika mfumo huo.
Amesema suala la
kuhamasisha wanachi kujiunga na bima ya afya ya jamii CHF iliyoboreshwa
siyo jukumu la wataalam wa afya peke yao kwani wanaotakiwa kulisimamia
ni viongozi wa vijiji ambao ndiyo waliokaribu na watu.
“Hili suala la watu
kujiunga na bima hii ya afya ya jamii ya CHF iliyoboreshwa ni suala la
kushirikishana hawa viongozi wa vijiji kama mwenyekiti wa kijiji na
afisa mtendaji wa kijiji ndiyo wenye watu na wenye mikutano ya hadhara
ambayo ajenda hii wataifikisha kwa njia rahisi”amesema Dk. Gwajima.
Pia Dk. Gwajima
amesema kuwa kama viongozi wa serikali za vijiji watakuwa na ushirikiano
na wataalamu wa vituo vya afya nchini wataweza kuibeba ajenga hiyo kwa
kuifikisha kwa wanachi na kuweza kuziandikisha kaya zote nchini katika
mfumo huo wa CHF iliyoboreshwa.
Kwa upande wake
Muuguzi wa Zahanati hiyo Shija Makeja,amesema kuwa kupata mafanikio ya
kuwa na idadi kubwa ya wanachama wa bima ya afya ya jamii CHF
iliyoboreshwa kumetoka na kushirikiana kwa karibu na viongozi wa
serikali ya kijiji.
Amesema kutokana na
kuhudumia idadi kubwa ya watu wanaotumia CHF iliyoboreshwa wameweza
kupata fedha za kujiendesha na kuondokana na changamoto za ukosefu wa
madawa ambao awali ulikuwa kikwazo.
Nae Meneja mradi wa
HPSS Tuimarishe afya, Ally Kebby, amesema kuwa azma ya serikali ni
kutengeneza mfumo wa bima ambao mwanachi atatambuliwa na pesa
anayochangia itarudi kwenye kituo.
Mradi wa HPSS
Tuimarishe afya unafadhiriwa na shirika la maendeleo na ushirikiano la
Uswisi kwa kushirikana na serikali ya Tanzania ambao umechangia katika
kuunda mfumo wa kutendea kazi wa IMIS na kutoa mafunzo kwa waandikishaji
waratibu na wasimazi wa CHF iliyoboreshwa nchini.
0 comments:
Post a Comment