Katibu Mkuu Wizara ya
Mifugo na Uvuvi anayeshughulikia sekta ya Uvuvi Dk. Rashidi
Tamatama,akizungumza na wadau wakati wa warsha ya uzinduzi wa zoezi la
kupitia na kuandaa mpango mpya kabambe wa uvuvi uliofanyika leo jijini
Dodoma
Muwakilishi kutoka
shirika la FAO Bw.Fred Kafeo,akisoma taarifa wakati wa warsha uzinduzi
wa zoezi la kupitia na kuandaa mpango mpya kabambe wa uvuvi uliofanyika
leo jijini Dodoma.
Mkurugenzi wa Uvuvi
wizara ya Mifugo na Uvuvi Bw.Emmanuel Bulayi,akiongea na wadau wakati
wa warsha uzinduzi wa zoezi la kupitia na kuandaa mpango mpya kabambe wa
uvuvi uliofanyika leo jijini Dodoma.
Katibu Mkuu Wizara ya
Mifugo na Uvuvi anayeshughulikia sekta ya Uvuvi Dk. Rashidi
Tamatama,akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) mara baada
ya kuzindua warsha wa zoezi la kupitia na kuandaa mpango mpya kabambe
wa uvuvi uliofanyika leo jijini Dodoma.
Kaimu Meneja Mkuu
Shirika la Uvuvi Tanzania TAFICO Bi. Esther Mulyila wakati wa warsha ya
uzinduzi wa zoezi la kupitia na kuandaa mpango mpya kabambe wa uvuvi
uliofanyika leo jijini Dodoma.
Katibu Mkuu Wizara ya
Mifugo na Uvuvi anayeshughulikia sekta ya Uvuvi Dk. Rashidi Tamatama
akiwa katika picha ya pamoja na wadau baada ya kuzindua warsha ya
uzinduzi wa zoezi la kupitia na kuandaa mpango mpya kabambe wa uvuvi
uliofanyika leo jijini Dodoma.
…………………………….
Na.Alex Sonna,Dodoma
SERIKALI imesema iko
katika michakato wa kulifufua Shirika la Uvuvi la Taifa (TAFICO) ambalo
litajiwekeza katika uvuvi wa samaki kwenye ukanda wa bahari kuu.
Hayo yamebainishwa
na Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi anayeshughulikia sekta ya Uvuvi
Dk. Rashidi Tamatama wakati wa warsha ya uzinduzi wa zoezi la kupitia
na kuandaa mpango mpya kabambe wa uvuvi.
Amesema malengo ya
serikali ya kuifufua TAFICO inatarajia kuwa na tija kubwa kutokana na
mipango iliyopo katika kuiendeleza sekta hiyo.
“Mipango yetu ni
kuhakikisha hii sekta unakuwa na serikali inafanya michakato ya kuifufua
TAFICO na Mambo mazuri yanakuja” amesema Dkt Tamatama.
Amebainisha mpango
mpya kabambe wa uvuvi unaelekeza sekta kusimamia, kuhifadhi na kulinda
ili sekta hiyo itoe mchango mkubwa kwenye lishe kwa mtu moja moja na
usalama wa chakula na kuelekeza sekta ili itoe mchango kwa uchumi,
Amesema mpango
uliozinduliwa mwaka 2002, ulimalizika mwaka 2015 na mafanikio ya mpango
ule upande wa pwani kuna maboresho makubwa ya uvuvi wakati wa mradi
uliojenga mialo nyingi na kukopesha zana za kuvulia vikundi mbalimbali
vya uvuvi, pia kuna mradi mwingine wa benki ya dunia.
Kwa upande wake
kaimu Meneja Mkuu wa TAFICO, Ester Mulyila, amesema Shirika hilo
linatazamiwa kufufuliwa hivi karibuni na menejimenti ya kufufua shirika
hilo waliteuliwa kuanza taratibu za kufufua shirika.
Amesema TAFICO
ilianzishwa 1974 wakati wa serikali ya awamu ya kwanza, ili kuendeleza
shughuli za uvuvi makao makuu Dar es salaam na ilifanya kazi Pwani yote
ya Tanzania kuanzia Tanga,mpaka Mtwara ziwa Victoria.
Lingine ni
Tanganyika Nyasa kubwa mpaka mwaka 1996 ikijihusisha na uvuvi hasa wa
kambamiti ilikuwa na meli, viwanda vya kutengeneza mashua za mbao na
chuma, mitambo ya kuzalisha barafu, maghara ya kuhufadhia samaki.
Amebainisha mwaka
2008 wizara ya maliasili na utalii ilikuwa na dhamana ya uvuvi iliuza
vitu vinavyohamishika kwa taratibu za serikali msajili wa hazina, lakini
mali zisizohamishika zilibaki viwanja na majengo vilibaki kwa matumizi
ya serikali.
Serikali ya awamu
hii.imeongeza nguvu ya kutaka kufufua shirika waraka wa baraza la
mawaziri imeelekeza shirika hilo kufufuliwa, lengo kuwezesha serikali
kunufaika na raslimaliza zake za uvuvi hasa zilipo uchumi wa bahari kuu
una ukubwa wa eneo la kilomita za mraba 223,000 ikiwa ni sawa na robo
ya Tanzania nchi kavu.
0 comments:
Post a Comment