Mkurugenzi wa Sekritarieti ya SADC
(Miundombinu), Bi.Rosemary Makoena, akizungumza na Waandishi wa Habari
(hawapo pichani), kuhusu utekelezaji wa mpango mkakati wa kuboresha
miundombinu katika Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika-SADC, mkutano
ulifanyika katika Kituo cha Mikutano cha kimataifa Julius Nyerere Jijini
Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Sekritarieti ya SADC
(Viwanda na Biashara), Bwana. Calicious Tutalife, akizungumza na
Waandishi wa Habari (hawapo pichani), kuhusu utekelezaji wa mpango
mkakati wa kuboresha biashara katika Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa
Afrika-SADC, mkutano ulifanyika katika Kituo cha Mikutano cha kimataifa
Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi WA Sekritarieti ya SADC
(Ulinzi na Usalama), Bwana. Jorge Cardoso, akizungumza na Waandishi wa
Habari (hawapo pichani), kuhusu historia ya ukombozi wa nchi za kusini
mwa Afrika kuwekwa kwenye mitaala ya wanafunzi wa elimu ya msingi,
mkutano ulifanyika katika Kituo cha Mikutano cha kimataifa Julius
Nyerere Jijini Dar es Salaam.
…………………..
Na.Paschal Dotto-MAELEZO
SEKRITARIETI ya Miundombinu ya
Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini Mwa Afrika (SADC) inajikita
katika kuimarisha na kuboresha miundombinu ya usafirishaji kwa kufanya
ukarabari na kuhuisha sekta hiyo hususani sekta ya Bandari, Reli na
Anga.
Akizungumza na Waandishi wa Habari
Jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Wa Sekritarieti ya SADC Miundombinu
Bi.Rosemary Makoena amesema kuwa hakuna Maendeleo pasipokuwa na
uimarishwaji wa sekta hiyo, ili kuhakikisha kuwa nchi wanachama
wanaunganishwa na sekta hiyo kufanya biashara katika ukanda wao.
Ameongeza kuwa Miundombinu
unayopigiwa chapuo kwenye utekelezaji wa Mpango Mkakati wa Miaka 5 ni
pamoja na Miundombinu ya Usafirishaji ambayo imebeba dhamira kubwa
kwenye kuimarisha mawasiliano ya kibiashara baina ya nchi wanachama.
“Katika Mpango Mkakati wa
2015-2020 kwa nchi wanachama wa SADC tunaangalia zaidi kwenye
utekelezaji na uangalizi wa miradi ya uimarishwaji wa miundombinu ya
kusafirisha bidhaa.Mpango mkakati huo unalenga kuimarisha Sera
mbalimbali ikiwemo ile ya uendelezwaji na ukarabati wa Bandari (SADC Corridors of 2008) ya ukanda wetu wa kusini mwa Afrika”, Amesema Makoena.
Aidha, mpango huo wa SADC unalenga
zaidi kwenye kusaini, kutekeleza na kuendeleza Sheria itakayozileta
pamoja nchi wanachama katika kuendeleza sehemu za lango la usafirishaji
wa majini. Hii itawezesha wananchi kwenye nchi hizo kufanya biashara kwa
urahisi bila vikwazo vyovyote.
Akisisitiza jambo hilo amasema
kuwa mpango huo unaendana na makubaliano ya wanachama walioko katika
lango ya bandari mbalimbali zilizoko katika ukanda huo wa kusisni mwa
Afrika. Ikianzia bandari ya Mtwara, Dar es Salaam, Trans-Kalahari, Central Beira na Nacala ambapo wanachama wataweke kanuni kulingana na makubaliano yao ya usafirishaji yalifanyika chini ya Memorandum of Unederstanding For South-North amasema Makoena.
Alisema kuwa katika kuimarisha
sekta hiyo ya usafirishaji wa majini, nchi wanachama walioko kwenye
lango la bandari wanaweka kanuni, lengo, katiba na namna ya kuungana
katika kuendeleza miradi ya ujenzi na ukarabati wa bandari hizo, ili
kuboresha na kuhakikishi zinakuwa imara zaidi kwa kupokea mzigo ya
kutosha.
“katika kutekeleza na kuhakikisha
kuwa sekta hii inaimarika azma kubwa tuliyonayo sisi kama Sekritarieti
ya Miundombinu ni kuboresha na kuhuisha sekta hii ili iweze kufanya kazi
kwa ufanisi na uhakika zaidi. Sekritarieti inaendelea na mpango mkakati
wa mwaka 2012-2021 na kuungwa mkono na Jumuiya ya Ulaya-EU ambao wako
tayari kusaidia kuimarisha miundombinu katika nchi wanachama wa SADC”,
Amesema Makoena.
Katika Mpango mkakati huo
Sekritarieti ya Miundombinu inalenga zaidi katika kuimarisha na kuweka
kanuni tisa (9) za pamoja kwa wanachama ikiwemo Udhibiti wa Uendeshaji
wa magari ya mizigo barabarani, viwango na vipimo vya magari ya mizigo
na mizani ya kupima magari yote, kwani kanuni hizo ni muhimu kwa usalama
wa barabara na bidhaa.
Pia, Machi mwaka 2018 SADC
ialisaini makubaliano ya Sheria ya usafirishaji wa kuvuka mipaka
miongoni mwa nchi wanachama inayojulikana kama Cross-Border Road Transporter-Regulator Forum (CBRT-RF). Ambayo inafanyakazi pamoja na Transport and Transit Facilitation Program (TTFP) yenye kazi ya kusimamia mambo ya usafirishaji yote hayo ni kuhakikisha Sekta ya usafirishaji inakuwa imara katika Jumuiya hiyo.
Makoena aliongeza na kusema kuwa
sekta ya usafirishaji kwa upande wa Anga inaimarishwa ili kuwezesha
kuwepo na ndege kubwa za mizigo katika ukanda huo wa kusini mwa afrika.
Kwani usafiri wa anga ni moja wapo ya kichocheo muhimu katika
kutekeleza ujenzi wa viwanda.
Hivyo, Sekritarieti ya Miundombinu inatekeleza hilo kwa kuanzisha Taasisi ya masuala ya usalama wa usafiri wa Anga (SADC Aviation Safety Organization,SASO) inayoshughilikia masuala ya usafiri wa anga katika nchi wanachama wa Jumuiya hiyo.
Pamoja na hayo, SADC miundombinu
inaendelea na utekelezaji wa ukarabati na ujenzi wa Reli katika Nchi
wanachama ili kuimarisha na kulinda usalama wa barabara, kwani mizigo
mizito itakuwa inasafarishwa kwa njia ya treni na kuepuka uharibu wa
barabara.
Akimalizaia Makoena alisema kuwa
katika sekta ya Nishati SADC inajivunia utekelezwaji wa Mradi Mkubwa wa
Ujenzi wa Bwawa la Umeme la Mto Rufiji nchini Tanzania,ambapo wanachama
wa SADc watafaidika na umeme huo.
“Tunajivunia mradi huu, siyo SADC
tu haya Jumuiya ya Afrika Mashariki-EAC, na tunakubaliana na kumuunga
mkono kwa uongozi na mafanikio makubwa kwa Rais wa Sasa wa Tanzania
katika utekelezaji wa mradi huo, tunahitaji kufanikisha hili kwa sababu
tunahitaji Miundombinu hii. Amesema Makoena
0 comments:
Post a Comment