Mkurugenzi wa Kilimo, Chakula na
Maliasili wa jumuiya hiyo Domingos Gove akizungumza na waandishi wa
habari za mikutano ya SADC inayoendelea jijini kwenye ukumbi wa Julius
Nyerere jijini Dar es salaam leo.
………………………………………………………..
JUMUIYA ya Maendeleo ya Nchi za
Kusini mwa Afrika (SADC)imesema ipo kwenye mkakati wa kuanzisha mfuko wa
kilimo wa kanda kwa ajili ya kusaidia nchi wanachama wa jumuiya hiyo.
Hayo yamesemwa leo Agosti 11, 2019 jijini Dar es Salaam na
Mkurugenzi wa Kilimo, Chakula na Maliasili wa jumuiya hiyo Domingos Gove
wakati anazungumza na waandishi wa habari za mikutano y SADC
inayoendelea jijini.
“Kwa sasa tupo katika mkakati wa
kuanzisha mfuko wa kilimo wa pamoja wa kikanda ambao lengo ni
kuhakikisha tunasaidiana katika chakula kwa nchi za SADC,” amesema Gove.
Amefafanua katika mkakati huo pia watahakikisha kunakuwa na
miundombinu itakayofanikisha nchi wanachama zinajikita kwenye kilimo kwa
ajili ya kupata chakula cha kutosha kwa nchi zao.
Mkurugenzi huyo wa Kilimo,Chakula
na Maliasili ameongeza kuwa kwenye mfuko huo ambao utaanzishwa kwa nchi
za SADC utahakikisha kunakuwa na usambazaji wa mbegu bora zisizo na
magonjwa , upatikanaji wa soko kwa malighafi zinazohusika kwenye suala
la kilimo.
Pia amesema mikakati mingine ni kuongeza ushindani na uzalishaji
wa nafaka pamoja na kuhakikisha kunakuwa na sera ya kulinda usalama wa
chakula.
“Tumejipanga kuhakikisha kupitia
mfuko huo wa kilimo tunazalisha chakula kwa wingi na pale ambapo nchi
mojawapo itakuwa na tatizo la uhaba wa chakula basi tunasaidia kupeleka
chakula kutoka kwenye nchi zenye chakula cha ziada,”amesema.
Ameongeza vyakula ambavyo vitazalishwa pamoja na mambo mengine
vitazingatia suala la lishe kuhakikisha walaji wanakuwa na afya njema na
imara kwa ajili ya kushiriki kikamilifu katika kuleta maendeleo kwa
nchi wanachama.
Wakati huo huo jumuiya hiyo
imeeleza namna amavyo imejipanga katika kuhakikisha nchi za jumuiya hiyo
zinakuwa na miundombinu yenye uhakika.
Ambapo kwenye eneo hilo
Mwenyekiti wa Kamati ya Habari, Matangazo na Machapisho ya Kamati Ndogo
ya Kamati Kuu ya SADC Zamarad Kawawa ametumia nafasi hiyo kueleza namna
ambavyo Serikali ya Tanzania ilivyoweka mkazi katika ujenzi wa
miundombinu.
“Tanzania tuko vizuri, katika
eneo hilo, ukienda bandarini, viwanja vya ndege , reli, na barabara kote
kumeimarika kwa kiwango kikubwa,”amesema Kawawa ambaye pia nia
Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Habari(MAELEZO).
Mwenyekiti wa Kamati ya Habari,
Matangazo na Machapisho ya Kamati Ndogo ya Kamati Kuu ya SADC Zamarad
Kawawaakiwa katika mkutano huo kulia ni Barbara Lopi Mkuu wa
Mawasiliano na Uhusiano SADC.
Barbara Lopi Mkuu wa Mawasiliano
na Uhusiano SADC akizungumza na kutoa ratiba ya mikutano mbalimbali
inayoendelea jijini Dar es salaam.
Innocent Mbrundula Ofisa Mawasiliano na Uhusiano SADC akifafanua jambo katika mkutano huo.
Picha zikionesha waandishi wa
habari kutoka vyombo mbalimbali wakifuatilia mkutano huo uliofanyika leo
kwenye ukumbi wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam.
0 comments:
Post a Comment