Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa
akiweka shada la maua kwenye moja ya makaburi ya watu waliofariki dunia
katikati ajali ya moto wa lori la mafuta lililoanguka kwenye eneo la
Msamvu mjini Morogoro katika mazishi yaliyofanyika kwenye makaburi ya
Kola Hill mjini Morogoro, Agosti 11, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri
Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa
akiweka udongo kwenye kaburi la mmoja wa watu waliofariki katika ajali y
amoto wa lori la mafuta lililoanguka katikati eneo la Msamvu mjini
Morogoro, katika mazishi yaliyofanyika kwenye makaburi ya Kola Hill
mjini Morogoro, Agosti 11, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
******************
HUZUNI, simanzi, majonzi na vilio
vimetawala mjini Morogoro leo wakati Waziri Mkuu, Kassim
Majaliwaakiongoza umati wa wananchi wa Manispaa ya Morogoro, mkoani
Morogoro katika mazishi ya wananchi waliofariki dunia kutokana na ajali
ya moto wakati wakichota mafuta yaliyokuwa yakimwagika baada ya lori la
mafuta kupinduka na kusababisha vifo vya watu zaidi ya 71 huku wengine
59 wakijeruhiwa.
Mazishi hayo yameanza
kufanyika leo (Jumapili, Agosti 11, 2019) katika eneo la makaburi la
Kola Hill mjini Morogoro ambapo Waziri Mkuu amemwakilisha Rais, Dkt.
John Magufuli. Ametoa pole kwa wafiwa wote na amewaomba wananchi wawe
watulivu katika kipindi hiki cha maombolezo.
Akizungumza na wananchi katika
ibada ya kuwaombea marehemu waliofariki katika ajali hiyo iliyotokea
katika eneo la Msamvu mjini Morogoro iliyofanyika kwenye viwanja vya
hospitali ya mkoa wa Morogoro, Waziri Mkuu ametumia fursa hiyo
kuwashukuru viongozi na wadau mbalimbali kwa ushirikiano waliouonesha
wakati huu wa amajonzi.
Kufuatia ajali hiyo iliyotokea
jana saa 2 asubuhi baada ya lori lenye shehena ya mafuta ya petrol
kupinduka jirani na Kituo Kikuu cha Mabasi cha Msamvu mjini Morogoro
wakati dereva alipokuwa akijaribu kumkwepa mwendesha pikipiki. Rais Dkt,
Magufuli ametangaza siku tatu za maombolezo ya Kitaifa kuanzia jana
Jumamosi Agosti 10,2019 na bendera zote zipeperushwe nusu mlingoti.
Mazishi hayo yamehudhuriwa na
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Vijana, Kazi, Ajira na
Wenye Ulemavu, Jenista Mhagama, Waziri wa Nchi OR-TAMISEMI, Selemani
Jafo, Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Isac Kamwelwe, Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola, Waziri wa Afya, Maendeleo ya
Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu.
Wengine ni Naibu Waziri wa
Kilimo, Omary Mgumba, Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu, Naibu
Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Ashatu Kijaji pamoja na wakuu wa mikoa,
wakuu wa wilaya, wabunge, viongozi wa dini na wananchi wa mkoa wa
Morogoro.
0 comments:
Post a Comment