Naibu Waziri wa Maliasili na
Utalii, Mhe. Constantine Kanyasu akiwa na kamati ya Ulinzi na usalama ya
Wilaya ya Gairo akiangalia huku akizungumza kwenye miti iliyopangwa kwa
ajili ya kuchoma mkaa mara baada ya kufanya ziara katika Hifadhi ya
Msitu wa Kumbulu kujionea miti iliyokatwa kinyume na sheria katika
Hifadhi hiyo wilayani Gairo mkoani Morogoro.
Naibu Waziri wa Maliasili na
Utalii, Mhe. Constantine Kanyasu akizumgumza na wananchi wa kijiji cha
Kumbulu wakati akitatua mgogoro wa ardhi uliodumu kwa muda wa miaka 10
ambapo aliwataka wananchi waache kuharibu msitu huo wa hifadhi.
Naibu Waziri wa Maliasili na
Utalii, Mhe. Constantine Kanyasu akikabidhiwa kabrashana Mkuu wa wilaya
ya Gairo, Siriel Mchembe lenye vielelezo vya mgogoro wa ardhi kuanzia
mwaka 2008 hadi mwaka huu mbele ya wananchi wa kijiji cha Kumbulu
wilayani Gairo mkoani Morogoro
Mkuu wa wilaya ya Gairo, Siriel
Mchembe akizungumza na wananchi wa kijiji cha kabla Naibu Waziri wa
Maliasili na Utalii, Mhe, Constantine Kanyasu kuzungumza na wananchi hao
kuhusu mgogori kati ya Wananchi na Msitu wa Hifadhi ya Kumbulu.
Naibu waziri wa Maliasili na
Utalii, Mhe. Constantine Kanyasu (kulia) akiwa na Mkuu wa wilaya ya
Gairo, Mhe, Siriel Mchembe (kushoto) wakiwa ndani ya kibanda ambacho
kimejengwa ndani ya Msitu wa Hifadhi ya Kumbulu uliopo wilayani Gairo
mkoani Morogoro. Msitu huo unaosimamiwa na Halmashauri ya wilaya ya
Gairo ambao umevamiwa na baadhi ya wananchi ambayo imeharibiwa kwa
kiasi kikubwa na baadhi ya wananchi.
**************
Naibu Waziri
wa Maliasili na Utalii, Constantine Kanyasu ametatua mgogoro wa ardhi
uliodumu kwa muda wa miaka 10 kati ya wanakijiji wa Kumbulu na msitu
wa Hifadhi ya Kumbulu unaosimamiwa na Halmashauri ya wilaya ya Gairo
kwa kushirikiana na Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS)
Mhe. Kanyasu
amesema mgogoro huo wa ardhi ulianza mwaka 2009 baada ya kijiji hicho
kupanga matumizi bora ya ardhi ambapo kutokana na baadhi ya viongozi wa
kijiji hicho kutokuridhia uamuzi huo na kuanza kuwachochea wananchi
kuendesha shughuli za kibinadamu ndani ya msitu huo.
Kufuatia hali
hiyo, Kanyasu ameagiza kamati iliyosheheni wataalam mbalimbali ambayo
ilikwisha undwa na wilaya ya Gairo igawe upya maeneo hayo kwa kuzingatia
idadi ya watu katika kijiji hicho kwa kuongeza eneo la kilimo kutoka
ekari 1,000 hadi ekari 2,314 kwa kulimega eneo la msitu wa hifadhi
wenye ukubwa wa ekari 5,500 hadi 5000 ili eneo hilo litumike kwa ajili
ya kilimo.
Aidha, Kanyasu
ameagiza eneo la malisho lipunguzwe kutoka ekari 1,641 hadi ekari 1,000
ili ekari 641 iweze kutumika kwa ajili ya kilimo.
Ameyatoa maagizo hayo wakati akizungumza na wananchi wa kijiji cha Kumbulu wilayani Gairo katika mkoa wa Morogoro.
Kutokana na
malalamiko hayo ya wananchi, Kanyasu aliwaeleza wananchi hao kuwa
mpango wa matumizi bora ya ardhi uliofanyika mwaka 2008 ulibainika
kuwa na kasoro kwa vile baadhi ya wananchi walichukua ardhi kubwa na
kuna wengine walichukua na kuiuza na kuna wengine walihamia kijijini
hapo kwa ajili ya kutafuta ardhi.
Akizungumzia
kuhusu ugawaji huo wa ardhi kwa kila kaya, Mhe. Kanyasu amesema
kijiji hicho kina kaya 642 hivyo kila kaya itagawiwa ekari mbili na
hivyo kufanya jumla ya ekari 1,284 kati ya ekari 2,314.
Awali, mpango
huo wa matumizi bora ya ardhi ulitenga eneo la misitu wa hifadhi ekari
5,500, eneo la kilimo ekari 1,000 pamoja na eneo la malisho la ukubwa
wa ekari 1, 600 lakini bado viongozi wa kijiji hicho licha ya
kushirikishwa katika mpango huo waliendelea kuwahamasisha wananchi
kuvamia misitu huo kwa madai kuwa hawayatambui maamuzi hayo.
Aidha, Mhe.
Kanyasu amesema kwa vile Msitu huo wa Hifadhi unapakana na vijiji vitatu
ni vyema na vijiji viwili mbali na kijiji cha Kumbulu kama navyo vina
uhitaji ya ardhi viwasilishe maombi yao ili kupunguza migogoro.
Katika hatua nyingine, Mhe, Kanyasu amezionya kaya hizo zitakazopata ardhi ziendeleze ardhi hiyo la sivyo zitanyang’anywa.
Pia, Kanyasu
amevionya vikundi vya watu wenye maslahi binafasi ndani ya kijiji hicho
viache tabia ya kuchochea migogoro ya ardhi la sivyo Serikali
haitasita kuvichukulia hatua kali za kisheria.
Kwa upande wake
Mkuu wa wilaya ya Gairo, Siriel Mchembe Amewataka wananchi hao kutoa
ushirikiano kwa Kamati hiyo wakati itakapokuwa ikitekeleza majukumu yake
ili kila kaya iweze kupata ardhi kwa ajili ya kilimo
‘’Lazima mpate
ardhi ya kilimo lakini ni muhimu pia kutunza miti iliyopo kwa vile bila
miti hakuna kilimo kwa sababu miti inasidia kuleta mvua. Alisisitiza
Mchembe
Naye, Mbunge wa
Gairo, Ahmed Shabiby amewataka wananchi hao wakati wakisubili kugawiwa
maeneo kwa ajili ya kilimo wajiepushe na ukataji miti ovyo katika msitu
wa Hifadhi ya Kumbulu.
‘’ Kwa wale
wanaotaka kukata miti kwa ajili ya kuchoma mkaa kwa ajili ya kuupeleka
sokoni ni lazima mfuate sheria, hata ukitaka kuukata miti uliopo
nyumbani kwako lazima uombe kibali kwa mamlaka inayohusika.’’
Alisisitiza Shabiby
0 comments:
Post a Comment